POLISI WILAYANI IGUNGA,MKOANI TABORA WAMSHIKILIA MFANYAKAZI WA HOSPITALI ANAYETUHUMIWA KUIBA DAWA ZA ARV

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora,Kamishna Msaidizi, Barnabas Mwakalukwa alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alithibitisha kushikiliwa kwa Francisi Malesa huku akisema kwamba kwa sasa hawezi kuzungumzia suala lolote kwani bado wanaendelea kumhoji ili kubaini idadi na thamani ya dawa alizoiba.

JESHI la polisi wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora linamshikilia mfanyakazi wa Hospitali ya wilaya ya Igunga,kitengo cha ugawaji wa dawa,Francis Mlesa (33) kwa tuhuma za wizi wa dawa mbali mbali zikiwemo za ARV.

Akithibitisha kushikiliwa kwa mfanyakazi huyo mbele ya waandishi wa Habari Ofisini kwake,Afisa Tarafa ya Igunga, Shadrack Kalekayo alisema tukio hilo lilitokea dis,24,mwaka huu saa moja na nusu usiku baada ya mlinzi wa zamu katika Hospitali hiyo kumshitukia mfanyakazi huyo baada ya kumuona akiwa amefunga makasha mawili ya dawa kwenye baiskeli yake.

Aidha afisa tarafa huyo alifafanua kwamba mfanyakazi huyo anashikiliwa na jeshi la polisi na kwamba ameshauagiza uongozi wa Hospitali kumchukulia hatua za kinidhamu mfanyakazi huyo wakati taratibu zingine zikiendelea.

Stars Custom Position

Performance
Design Quality
Code Readability
Speed Booster
Search Engine
Summary
State Department spokeswoman Marie Harf played down the notion that there are as many as 100,000 Russian troops now bordering Ukraine.
4.1

Kwa upande wake mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Kasembe Bundala Nangale aliweka bayana kuwa siku ya tukio hilo alikuwa akitoka kumwangalia,Chaula Nangale ambaye ni dada yake aliyekuwa amelazwa katika Wodi namba 3 katika Hospitali hiyo akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua,tumbo na mgongo,ndipo alipofika mlango wa geti la kutoka alimuona Mlesa akiwa amefunga kasha mbili kwenye baiskeli.

“Alisisitiza pia kuwa ndipo kabla hajatoka aliulizwa na mlinzi wa zamu kuwa anapeleka wapi dawa hizo alizokuwanazo,ambapo naye alijibu kwamba anakwenda kuziteketeza kwa moto kwani muda wa matumizi wa dawa hizo ulikuwa umeisha.

“Mimi nilishuhudia mlinzi akimuhoji mtumishi huyo hata hivyo alijibu kuwa dawa hizo anakwenda kuziteketeza kwa moto kwani muda wake wa matumizi ulikuwa umekwisha”.alisisitiza shuhuda huyo.”

Hata hivyo Kasembe aliweka bayana kuwa baada ya mfanyakazi huyo kutoa jibu hilo ndipo mlinzi alipomwamuru kufungua dawa hizo ili wazione,ambapo baada ya kufungua kasha moja, ilipogundulika kuwa zilikuwa dawa za ARV na baada ya hapo mtumishi huyo alifanikiwa kutoroka nazo baada ya mlinzi kuzidiwa na watu wanaopita katika geti hilo.

Kwa mujibu wa Kasembe baada ya kuona mtumishi huyo amekimbia ndipo alipotoa taarifa katika ofisi ya TAKUKURU wilaya ya Igunga na ndipo Mkuu wa TAKUKURU,Francis Nzuakuu alifika Hospitalini hapa na kuanza kumsaka mfanyakazi huyo bila mafanikio.

Akizungumzia tukio hilo,mlinzi aliyekuwa zamu katika Hospitali hiyo,Rushinangeme Paulo alisema mfanyakazi huyo alimkamata na dawa hizo akidai kuwa zimeisha muda wake na kwamba baada ya kuzichunguza aligundua kuwa muda wake wa matumizi ulikuwa bado haujaisha,na ndipo alitimua mbio huku akiwa na dawa hizo na kwenda kusikojulikana.

Mlinzi huyo hata hivyo alisema dis,26,mwaka huu ndipo walipofanikiwa kumpata mfanyakazi huyo na alipofikishwa katika uongozi wa Hospitali hiyo,alikiri kuiba kasha mbili za dawa hizo na lengo lilikuwa kwenda kuziteketeza kwa moto

Alibainisha pia kwamba baada ya kikao hicho ndipo Uongozi wa Hospitali ukiongozwa na Mganga mkuu wa wilaya Igunga,Deus Rutha walimpeleka mfanyakazi huyo katika Kituo cha Polisi Igunga.

Wakizungumza na kituo hiki,baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Afya wanaofanya kazi katika Hospitali ya wilaya ya Igunga na ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao gazetini walisema kuwa dawa alizoiba mfanyakazi huyo,amekuwa akiwauzia wafanyabiashara wa ng’ombe kwa ajili ya kunenepesha mifugo yao.

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Deos Rutha alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo kuhusu aina ya dawa,kiasi na thamani iliyoibiwa na mfanyakazi,alikanusha kupelekwa kwa mfanyakazi wa Hospitali hiyo Kituo cha Polisi kwa tuhuma za wizi wa dawa na kwamba Hospitali yake iko salama.

Akizungumzia tukio hilo,Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Igunga,Francis Nzuakuu alisema yeye alipigiwa simu na raia mwema kuwa kuna mtumishi ameiba dawa Hospitali ya wilaya na ametoroka nazo na ndipo alipofika kwenye eneo la tukio na kuanza kumsaka mfanyakazi huyo bila mafanikio.

Alisema baada ya kumkosa mfanyakazi huyo ndipo alimwagiza Mganga Mkuu wa wilaya ya Igunga,Deus Rutha kumsaka hadi kumpata mfanyakazi huyo na ndipo dis,26 walifanikiwa kumpata na tayari yupo mahabusu kituo cha polisi.

Naye Mkuu wa wilaya ya Igunga John Mwaipopo alikiri kuwepo kwa tukio hilo la mtuhumiwa kushikiliwa na jeshi la polisi na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa watumishi wa idara zote kufanya kazi kwa uadilifu na kujiepusha na vitendo kama hivyo kwani serikali haitamfumbia macho mtumishi yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya wizi wa dawa za serikali.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora,Kamishna Msaidizi, Barnabas Mwakalukwa alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alithibitisha kushikiliwa kwa Francisi Malesa huku akisema kwamba kwa sasa hawezi kuzungumzia suala lolote kwani bado wanaendelea kumhoji ili kubaini idadi na thamani ya dawa alizoiba.

You may also like

2 comments

 1. Alexander Jones 6 years ago

  President Barack Obama on Friday urged Russia to stop “intimidating” Ukraine and to pull its troops back to “de-escalate the situation.” He told CBS that the troop buildup may “be an effort to intimidate Ukraine, or it may be that [Russia has] additional plans.”

  Reply Like Dislike
  1. Inna Goodman 6 years ago

   Pentagon officials say they believe there could be close to 50,000 Russian troops bordering the former Soviet republic and inside Crimea, recently seized and annexed by Moscow. That estimate is double earlier assessments, and means Russian President Vladimir Putin could order a lighting strike into Ukrainian territory with the forces already in place.

   Reply Like Dislike
Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh