WAKAZI KALIUA WAPANDA MITI 37,000 KUOKOA MAZINGIRA

Mkazi wa kijiji cha Ugunga Juma Bwandu alisema zoezi hilo ni utekelezaji wa agizo la serikali ya awamu ya tano la kuhakikisha kila mtu anashiriki kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti ya kutosha ili kuwa na kilimo endelevu.

JUMLA ya miti 37,000 imepandwa na wakazi wa vijiji vya Ugunga na Ufukutwa vilivyoko katika wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora ikiwa ni mkakati wa kuokoa mazingira katika maeneo yao.

Wakazi hao ambao hujishughulisha na kilimo cha tumbaku, mahindi na mpunga walisema kuwa wamechukua hatua hiyo ili kurudisha uoto wa asili katika ardhi yao na watahakikisha kila mkazi anashiriki kikamilifu.

Walisema vitendo vya ukataji miti kwa ajili ya shughuli za kilimo cha tumbaku na ufugaji vimeathiri kwa kiasi kikubwa mazingira na ardhi imeanza kupoteza rutuba kutokana na shughuli hizo.

Mkazi wa kijiji cha Ugunga Juma Bwandu alisema zoezi hilo ni utekelezaji wa agizo la serikali ya awamu ya tano la kuhakikisha kila mtu anashiriki kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti ya kutosha ili kuwa na kilimo endelevu.

“Bwandu alisema kuwa hadi sasa wakazi wa kijiji hicho wameshapanda miti 37,000 na vyama vya wakulima vilivyoko katika kijiji hicho vya Ugunga na Usaguzi vimeshapanda miti zaidi ya 50,000 katika mashamba yao.”

Pentagon officials say they believe there could be close to 50,000 Russian

Mkazi huyo ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Msingi Ugunga alisema kila chama kimenunua ekari zisizopungua 20 kwa ajili ya kupanda mitina kila kimoja kinatarajiwa kupanda miti isiyopungua 60,000.

Kwa upande wake Hemed Athuman mkazi wa Kijiji cha Ufukutwa alisema wamewekeana utaratibu na kila mkazi (mkulima au mfugaji) atatakiwa kupanda miti isiyopungua 550 na viongozi wa kijiji watakuwa wanapita kukagua ili kuhakikisha zoezi linatekelezwa.

Naye Mwakilishi wa Kampuni ya JTI inayojishughulisha na ununuzi wa zao la tumbaku katika mkoa wa Tabora Chrispin Mchafu alisema katika kuunga mkono agizo la serikali la kuhifadhi mazingira kampuni hiyo inatarajia kupandamiti mil 2.”

Pentagon officials say they believe there could be close to 50,000 Russian

Mchafu alibainisha kuwa miti hiyo itapandwa katika vijiji vyote ambako Kampuni hiyo iliingia mkataba wa kununua tumbaku yao na asilimia 18 ya miti hiyo itagharamiwa na Kampuni huku asilimia 82 ikigharamiwa na vyama vya msingi.

Aidha alifafanua kuwa JTI itaotesha miche ya miti na kuigawa kwa wakulima na vyama vya msingi ili waweze kuipanda na itasimamia uanzishwaji wa mashamba ya miti na ustawi wake kwa kipindi cha miaka 2 kabla ya kukabidhi vyama husika.

You may also like

2 comments

 1. Alexander Jones 6 years ago

  President Barack Obama on Friday urged Russia to stop “intimidating” Ukraine and to pull its troops back to “de-escalate the situation.” He told CBS that the troop buildup may “be an effort to intimidate Ukraine, or it may be that [Russia has] additional plans.”

  Reply Like Dislike
  1. Inna Goodman 6 years ago

   Pentagon officials say they believe there could be close to 50,000 Russian troops bordering the former Soviet republic and inside Crimea, recently seized and annexed by Moscow. That estimate is double earlier assessments, and means Russian President Vladimir Putin could order a lighting strike into Ukrainian territory with the forces already in place.

   Reply Like Dislike
Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh