Watu sita wapoteza maisha kwa ajali Dodoma

Watu sita wamefariki papohapo na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali ya basi dogo aina ya Toyota Coaster kugongana na lori aina ya Mitsubishi Fuso katika eneo ambalo wakazi wanasema limekuwa na ajali za mara kwa mara.

WATU sita wamefariki papohapo na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali ya basi dogo aina ya Toyota Coaster kugongana na lori aina ya Mitsubishi Fuso katika eneo ambalo wakazi wanasema limekuwa na ajali za mara kwa mara.

Ajali hiyo ilitokea juzi usiku mita chache kabla ya kufika kituo cha mwisho Nzuguni ambako basi hilo lilikuwa likienda kutoka eneo la Sabasaba..

Abiria walikuwa kwenye basi hilo wamesema lilikuwa katika mwendo wa taratibu, lakini lori lililokuwa katika mwendo wa kasi likahamia upande wao barabarani na kusababisha ajali hiyo.”

Mganga mfawidhi wa mkoa, Dk Ernest Ibenzi alisema walipokea miili ya watu sita pamoja na majeruhi wengi, lakini akasema waliolazwa walikuwa 12 wakati wengine walichunguzwa na kuruhusiwa.

“Kati ya miili hiyo, watatu ni wanaume na mwili mmoja ni wa mama mtu mzima, wale wagonjwa tunaendelea kuwahudumia na hali zao si mbaya sana. Tuendelee kuwaombea,” alisema Dk Ibenzi.”

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto hakupatikana mara moja kuzungumzia tukio hilo .”

Mmoja wa watu waliokuwepo kwenye gari lililopata ajali,Zahoro Stephen alisema kilichowasaidia kutoka salama ni ujasiri wa dereva wa Coaster na Mungu, vinginevyo wangekwisha wote.”

Stephen, ambaye ni muuza matunda katika soko la Sabasaba, alisema ajali ilitokea wakiwa katika mwendo mdogo kwa kuwa walikuwa wamekaribia kufika kona ya kuingia kituo cha mwisho..

“Alisema basi hilo liliondoka kituo cha Sabasaba likiwa limejaza abiria, lakini walishuka kadri lilivyokuwa linakaribia Nzuguni na wakati wa ajali kulikuwa na watu wapatao 20.”

Mfanyabiashara huyo ambaye alipoteza kijana wake anayeitwa Omar Mdira (16) alisema alishuhudia lori likiwa na mwendo mkali na lilihama upande wake kwenda walikokuwa na kuwagonga, likifumua eneo la juu la bodi ya gari yao.

“Lakini historia ya ajali za mara kwa mara katika eneo hilo si nzuri. Ajali ya mwisho eneo hilo ilitokea Oktoba 24 wakati mwendesha pikipiki, Charles Kanyopaa (45) mkazi wa Nzuguni alipopoteza maisha baada ya kugongwa na gari. Mita chache kutoka eneo hilo, mwishoni mwa 2016 ilitokea ajali iliyohusisha gari dogo lililokuwa likiendeshwa na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania.”

Related Posts

You may also like

2 comments

 1. Alexander Jones 6 years ago

  President Barack Obama on Friday urged Russia to stop “intimidating” Ukraine and to pull its troops back to “de-escalate the situation.” He told CBS that the troop buildup may “be an effort to intimidate Ukraine, or it may be that [Russia has] additional plans.”

  Reply Like Dislike
  1. Inna Goodman 6 years ago

   Pentagon officials say they believe there could be close to 50,000 Russian troops bordering the former Soviet republic and inside Crimea, recently seized and annexed by Moscow. That estimate is double earlier assessments, and means Russian President Vladimir Putin could order a lighting strike into Ukrainian territory with the forces already in place.

   Reply Like Dislike
Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh