URAIS 2020 Lissu awapa masharti magumu Chadema

Joto la kuwania Urais mwaka huu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limeanza kupanda ambapo taarifa mpya zinadai Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Bara, Tundu Lissu anapewa nafasi kubwa ya kukiwakilisha chama hicho kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu. Kwa kufahamu uhitaji huo, inadaiwa kuwa Lissu tayari kaweka masharti magumu kwa chama chake […]

Joto la kuwania Urais mwaka huu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limeanza kupanda ambapo taarifa mpya zinadai Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Bara, Tundu
Lissu anapewa nafasi kubwa ya kukiwakilisha chama hicho kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu.

Kwa kufahamu uhitaji huo, inadaiwa kuwa Lissu tayari kaweka masharti magumu kwa chama chake ili aweze kukiwakilisha kwenye kinyang'anyiro cha urais mwaka huu.

Mtoa taarifa mmoja kutoka ndani ya Chadema amedokeza kwamba Lissu ameweka sharti la kulipwa Sh. bilioni 3
kwanza ndiyo akubali kukiwakilisha Chadema kwenye uchaguzi mkuu. Tanzanite limedokezwa kwamba pamoja
na sharti hilo la Lissu kuonekana kama ni tishio la uchumi wa chama, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe yupo mstari wa mbele wa kumshawishi Lissu achukuwe fomu ya kuwania urais mwaka huu hata kama chama hakitafikia dau hilo.
Lissu ameweka sharti hilo kwa sababu anajua wazi kwamba hata akisimama kugombea urais hawezi kufua dafu kwa
Rais Dkt. John Magufuli ambaye atasimama kutetea mhula wa pili wa urais.

Lissu ameweka sharti hilo ili kujichukulia chake mapema, si unajua tena mambo yalivyo ndani ya chama, kila kitu ni
kwa hiyo naye bora achukue chake kama kweli chama kinamhitaji.

Pia huu ni mtihani kwa chama ndio maana Mwenyekiti wetu Mbowe ameamua kumpambania najua zitapatikana tu hizo fedha tumalizane naye ili atuwakilishe. Tunamng’ang’ania Lissu agombee walau
anaweza kuonyesha upinzani kwa JPM lakini tofauti na yeye sijaona," kilisema
chanzo cha habari.
Inadaiwa Mbowe amekuwa akikutana na watu wake wa karibu mara kwa mara kwa ajili ya kujadili ni kada yupi anafaa kukiwakilisha Chadema kwenye uchaguzi huku jina la Lissu likiwa tayari limeishatawala vikao vyao.

Gazeti hili lilimtafuta Lissu ili athibitishe madai hayo lakini hakupatikana kupitia mawasiliano yake ya simu.
Hata hivyo jitihada mbalimbali za kumpata Lissu bado zinaendelea.
Kwa upande wake Mbowe ameonyesha dhamira ya dhati ya kumbeba Lissu kwanye kinyang'anyiro cha urais mwaka huu.
Mbowe ambaye hivi karibuni amekipitisha chama kwenye chujio kubwa la uongozi huku akimuweka Lissu kwenye nafasi ya umakamu mwenyekiti bara amekuwa na hesabu kali za kuhakikisha chama kinapatamgombea mwenye mvuto ndani ya Chadema.
Mbowe alitumia nguvu kubwa kwenye uchaguzi wa ndani uliomalizika mwishoni mwaka jana na kufanikiwa kutetea kiti chake kwa kupata kura 886 sawa na asilimia 93.5 huku mshindani wake Cecil Mwambe akipata kura 59 sawa na asilimia 6.2. Katika uchaguzi wa mwaka 2014, Mbowe alipata kura 789 sawa na asilimia 97.3.
Kurejea kwa Mbowe kwenye kiti hicho kulienda sanjari na kumuweka Lissu kwenye timu yake ya kuiongoza Chadema.

0 comments

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh