Zitto anenepesha virusi Chadema

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ananenepesha virusi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),ili kukidhoofisha chama hicho, Fahari Yetu imeelezwa. Habari kutoka kwa kada wa Chadema ambaye ni mmoja wa watu wanaofanya vikao na Zitto Kabwe zinaeleza kuwa lengo la mbunge huyo wa Kigoma Mjini ni kuwatumia baadhi ya makada wenye ushawishi […]

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ananenepesha virusi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),ili kukidhoofisha chama hicho, Fahari Yetu imeelezwa.
Habari kutoka kwa kada wa Chadema ambaye ni mmoja wa watu wanaofanya vikao na Zitto Kabwe zinaeleza kuwa lengo la mbunge huyo wa Kigoma Mjini ni kuwatumia baadhi ya makada wenye ushawishi kuwashawishi wanachama wenye nguvu kujiunga na ACT-Wazalendo.

“Sisi kwenye vikao vyetu tumeazimia kuwashawishi wanachama wote wa Chadema ambacho ni chama changu, wenye ushawishi na nguvu ndani ya maeneo fulani fulani kuondoka na kujiunga na ACT.” Alisema.Aliongeza kuwa “Lengo la kufanya hivyo ni kutaka kuvunja nguvu za Chadema hasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ili ACT-Wazalendo kiwe chama kikuu cha upinzani kwa kuwa na wabunge wengi kuliko Chadema.”

Kada huyo aliendelea kusema kuwa hadi hivi sasa tayari wameanza kufanikiwa kwani baadhi ya wale ambao waliokuwa wanawataka wamesfahanya nao mazungumzo na wameonyesha nia ya kuondoka Chadema.

0 comments

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh