Wanawake wasema Oktoba 2020 Magufuli anatosha

Umoja wa wawanawake wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) (UWT) Wilaya ya Ukerewe waahidi kumuunga mkona Mwe- nyekiti wa CCM taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muun- gano Dkt John Pombe Magu- fuli kushinda uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo Spelancia Naga- bona wakati […]

Umoja wa wawanawake wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) (UWT) Wilaya ya Ukerewe waahidi kumuunga mkona Mwe- nyekiti wa CCM taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muun- gano Dkt John Pombe Magu- fuli kushinda uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo Spelancia Naga- bona wakati wa hafla ya kupokea baiskeli 59 za we- nyeviti na makatibu wa Ju- muiya hiyo wa Kata 25 za Jimbo la Wilaya ya Ukerewe zilizotolewa na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mwanza Kemilembe Lwota na kukabidhiwa mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la UWT Wilaya.
Mwenyekiti Nagabona ali- waeleza wajumbe wa Baraza hilo kuwa baiskeli hizo zi- takabidhiwa kwa kila Mwe- nyekiti na katibu wa Jumuiya hiyo wa Kata zote 25 ili ku- wasaidia usafiri wa kuwafikia wanachama wa ngazi za matawi na kuhamasisha wa- nanchi ili kuwachagua wag- ombea watakaopitishwa na CCM kugombea Ubunge na Udiwani huku wakihakikisha wanampigia debe Rais Dkt Magufuli achaguliwe tena kuliongoza taifa kwa miaka mitano mingine.
Alieleza kuwa Rais Dkt. Magufuli ametekeleza ahadi ya majisafi na kuboresha vi- tuo vya afya na Hosptali ya Wilaya vinatoa huduma bora kwa wananchi sanjari na kui- malisha usafiri ndani ya ziwa Victoria hudusani kisiwa ki- kubwa cha Ukerewe na Uka- ra pia kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata elimu bure ikiwemo sekond- ari, hivyo nijambo la kujivu- nia kumchagua tena Rais na wawakilishi wa wananchi ambao ni Mbunge na Madi- wani wa CCM bila shaka yoyote.
Nagabona alisema wa- nanchi wa Wilaya ya Uk- erewe walifanya ushabiki na wakakosea kuuchagua upin- zani kwa miaka nane ambapo mambo yalikuwa hayaendi kabla ya Mbunge Joseph Mkundi aliyesoma alama za nyakati na kurejea CCM kwa kuwa alijua jeshi kubwa la wanawake wa Wilaya ya Ukerewe limejipanga kureje- sha Jimbo kutoka upinzani hata hivyo wamejipanga kuhakikisha vitongoji, vijiji, Kata, Jimbo na Rais wote wa- natoka CCM kwa ushindi wa kishindo.
“Nikupongeze Mbunge Lwota kwa kutekeleza ahadi yako yakutusaidia usafiri ili kuhakikisha kazi za Jumuiya zinaimalika na kuwafikia wa- nachama ikiwemo kuongeza wanachama wapya wa Ju- muiya yetu na Chama lakini pia kuisemea miradi mbalim-
bali iliyotekelezwa na serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi na ahadi za viongozi ikiwemo wabunge na madiwani,” alisema.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mwanza, Kemilem- be Lwota akikabidhi baiskeli hizo alisema ametekeleza ahadi ya kutoa usafiri kwa viongozi wa Jumuiya hiyo ngazi ya Kata katika Wilaya zote ambazo Jografia za ku- wafikia wanachama zinaka- biliwa na inachangamoto ya usafiri.
“Niliwaahidi kupitia kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya Mkoa leo nimekabidhi bais- keli 59 kwa ajili ya matumizi ya usafiri lakini pia nimetoa mabati 100, mbao 100 na mi- fuko 50 ya saruji ili kukamil- ishwa kwa mradi wa ujenzi wa jengo la kitegauchumi la Jumuiya Wilaya ya Ukerewe ili kujiingizia fedha zitakazo- saidia kuendeleza Jumuiya pia nimetoa mashuka 200 na vitanda Jumuiya Hospitali ya Wilaya iliyopo Mji wa Nansio sanjali na kuipatia Jumuiya mradi wa pikipiki kuwasaidia kuingiza fedha za uendeshaji shughuli za kila siku,” alise- ma Lwota.
Mbuge Lwota amewa- hakikishia wanachama wa CCM, Jumuiya hiyo na wa- nanchi kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt John Magufuli mzalendo utaen- delea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na
kuhakikisha huduma bora zinapatikana kupitia sekta zote hiyo waendelee kuiunga mkono CCM na serikali ku- fika malengo na taifa liweze kufikia uchumi wa kati na upatikanaji huduma bora za kijamii.
“Wanawake ni jeshi kubwa hivyo tujipange sawa sawa kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ili kuendelea kuongoza taifa na kuhakikisha raslimali za taifa zinawanufaisha watanzania wote na kupatikana maen- deleo yatakayoambatana na huduma bora za kijamii chini ya Rais Dkt Magufuli in- awezekana na mumemuona mzalendo amekuwa akip- ambana kutekeleza miradi mikubwa kwa fedha za kodi yetu,” alisema.
Kwa upande wake Mwe- nyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Ally Mambile alimpongeza Mbunge Lwota kwa kujitolea kusaidia baiskeli ambazo watazitumia kwa usafiri len- go ikiwa ni kutafuta kura za wagombea wa CCM mwezi Oktoba lakini pia zitaweze- sha jeshi kubwa la wanawake kufika maeneo mbalimbali kuwafikia wananchi na ku- waomba wawamchague Rais Dkt Magufuli, Wabunge na Madiwani.
“Niwahase viongozi wa UWT Wilaya na Kata kuzitu- mia baiskeli hizi kuhakikisha malengo yanafikiwa ikiwemo
kuongeza wanachama na ku- pata ushindi wa kimbunga zaidi ya uhuu wa serikali za Mitaa ambapo tumefanya vizuri na kauli mbiu yetu Wilaya ya Ukerewe ni CCM 2020 ni Rais Dkt Magufuli, Mbunge na Madiwani Kata zote 25 mali ya CCM,” alise- ma.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Boniphace Magembe aliwahakikishia viongozi na wanachama wa CCM kuwa serikali imejipanga kuhakiki- sha amani na utulivu wakati wa michakato ya kura za maoni na kampeni za Uch- aguzi mkuu kwa wagom- bea kunadi sera zinafanyika bila vurugu na watakaoleta uchochezi na uvunjifu wa am- ani watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na hawata mfumbia macho mtu ama kikundi cha watu wachache watakaoandaliwa kuvuruga amani maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Uke- rewe, Joseph Mkundi (CCM), aliwashukuru viongozi na wanachama kumpokea al- ipoamua kurejea CCM na kuwa bega kwa bega ku- hakikisha maendeleo yana- patikana ikiwemo kutekele- zwa kwa miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta za majisafi, elimu, barabara, umeme, kilimo cha kisasa, ufugaji wa tija, usafiri kulin- gana na jiografia ya visiwa vyetu hivyo tuhakikishe Rais Dkt Magufuli anapeta kwa

0 comments

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh