Kagera Sugar yamtandika Yanga

Na Mwandishi wetu MABINGWA wa kihistoria Yanga jana wamechezea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mtanange uliopigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam. Katika dakika ya 13 mshambuliaji wa Kagera Sugar, Mhilu alifungua akaunti ya mabao dakika ya 13 kwa kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango Farouk Shikalo. Yanga ikiwa […]

Na Mwandishi wetu

MABINGWA wa kihistoria Yanga jana wamechezea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mtanange uliopigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika dakika ya 13 mshambuliaji wa Kagera Sugar,
Mhilu alifungua akaunti ya mabao dakika ya 13 kwa kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango Farouk Shikalo.

Yanga ikiwa chini ya nahodha wao Haruna Niyonzima kwenye mchezo wa leo ilimshuhudia kiungo wao Mohamed Issa ‘Mo Banka’ akiwapunguzia kasi dakika ya 44 baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa kucheza faulo kwa wachezaji wa Kagera Sugar.

Kipindi cha kwanza Yanga walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0 walijipanga kurejea kupindua meza kipindi cha pili mambo yakazidi kuwa magumu kwani Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime ilimzidi ujanja Luc Eymael ambaye ni mara yake ya kwanza kukaa kwenye benchi la ufundi akipokea kijiti cha Mwinyi Zahera.

Bao la pili kwa Kagera Sugar lilifungwa dakika ya 66 kupitia kwa Ally Ramadhan aliyemalizia pasi ya Abdallah Siseme na msumari wa mwisho ulipachikwa kwa kichwa dakika ya 89 na kuifanya Yanga kushindwa kutumia dakika nne za nyongeza kupata bao la kufutia machozi.

You may also like

0 comments

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh