Kangi Lugola aangukia pua..

Rais Dkt. John Magufuli amewatumbua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye kwa kusaini mkataba wa hovyo Pia Naibi Waziri wa Wizara hiyo Hamad Masauni na Katibu Mkuu Meja Jenerali Jacob Kingu wamemuanikia barua ya kujiuzulu nyazifa zao jambo ambalo Rais […]

Rais Dkt. John Magufuli amewatumbua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye kwa kusaini mkataba wa hovyo
Pia Naibi Waziri wa Wizara hiyo Hamad Masauni na Katibu Mkuu Meja Jenerali Jacob Kingu wamemuanikia barua ya kujiuzulu nyazifa zao jambo ambalo Rais alililidhia.
Rais Dkt. Magufuli alichukua hatua hiyo jana wakati akizindua nyumba 12 za makazi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kuchukua uamuzi huo Rais Dkt. Magufuli aliweka wazi sababu za kuchukua hatua hiyo kuwa ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kulikuwa kunatengenezwa mkataba wa hovyo wenye thamani ya Euro milioni 408 sawa na zaidi ya shiling trilioni moja.
Alisema mkataba huo kwa hatua za awali ulikuwa umeshasainiwa baina ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (Memorandum of Understanding (MOU) Andengenye na Kampuni moja ya kutoka Romania kwa ajili ya ununuaji wa vifaa vya jeshi hilo.
Hivyo kutokana na madudu hayo aliwapongeza Naibu Waziri Masauni na Katibu Mkuu Kingu kwa kuandika barua za kujiuzulu huku akisahangazwa na Waziri Lungula pamoja na Kamishna Jenerali Andengenye kuendelea na nyazifa zao.
“Nimpongeze Waziri wa Mambo ya Ndani (Masauni) kujiuzuli kwa kutambua hilo. Hivi karibuni kulikuwa na mkataba mmoja wa ajabu unatengenezwa Wizara ya Mambo ya Ndani wenye thamani ya Euro milioni 408. Mkataba umesainiwa na Kamishna Jenerali wa Zimamoto. Haujapitishwa na Bunge.
“Kangi Lugola pamoja na mwili wake ni Mwanafunzi wangu nimemfundisha Sengerema Secondary, lakini kwa hili hapana, Kamishna Jenerali Thobias Andengenye kwa hili pia Hapana. Kangi Lugola nilitegemea barua yake ya kujiuzulu leo (jana) angetakiwa asiwepo hapa, Watu wamesaini mradi wa hovyo ambao hata Bunge haiujui ni mambo ya hovyo watu walikuwa wanalipwa sitting allowance ya dola 800.” Alisema Rais Dkt. Magufuli.
Aidha Rais Dkt. Magufuli alibainisha kwamba katika madudu hayo walishiriki pia watu kutoka kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
“Kuna Watu wengine kwenye hili wapo ndani ya Mkataba huu wa hovyo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu walisubiria Mwanasheria Mkuu hayupo wakasaini pia wale wasaidizi wa Andengenye nao wapo ndani ya mkataba huu naomba wote washughulikiwe na vyombo husika,” alieleza Rais Dkt. Magufuli.
Kadahalika Rais alisema watu wengine wanaohusika ni Wawizara ya Mambo ya Ndani, ndani ya kitengo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiwemo wasaidizi wa Kamishna Jenerali Andengenye.
Lugola anakuwa ni Waziri wa tatu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kutumbuliwa katika Sarikali hii ya Awamu ya Tano, waliomtangulia ni Charles Kitwanga na Mwigulu Nchemba.
Wakati akichukua uamuzi huo kwa masikitiko na uchungu mkubwa Rais Dkt. Magufuli aliweka wazi kuwa ni moja ya Wizara ambayo tangu aingie madarakani imekuwa ikimtesa sana kutokana na kuongoza katika kuingia mikataba ya hovyo.
Akizungumzia Mradi wa Nyumba za Makazi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, alisema ujenzi wa majengo hayo umegharimu shilingi Bilioni 13 ambapo awali aliagiza Jeshi la Magereza lipewe shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo.
Hivyo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ilipewa zabuni ya ujenzi lakini ilishindwa kumaliza kazi kwa miezi 27 wakiwa wamefikia asilimia 45 tu, ndipo alipoagiza kazi hiyo ikabidhiwe kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambao walipatiwa shilingi Bilioni 3 na kufanikiwa kukamilisha ujenzi huo kwa muda wa miezi 7.
Alilipongeza JWTZ kupitia JKT kwa kazi nzuri waliyoifanya katika ujenzi huo na ujenzi wa miradi mingine ikiwemo ukuta wa eneo la madini ya Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara, kambi ya JWTZ Ngerengere Mkoani Morogoro na ujenzi wa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Hata hivyo alilitaka Jeshi la Magereza kujirekebisha na kujifunza kutoka JKT kwa kuwa linayo nguvu kazi ya wafungwa takribani 13,000 ambao wanaweza kutumika katika uzalishaji mali na kujenga miundombinu ya jeshi hilo yakiwemo makazi ya Maafisa na Askari badala ya kusubiri kujengewa na majeshi mengine ama kutumia wakandarasi.
Rais Dkt. Magufuli alieleza kusikitishwa kwake na kusuasua kwa ujenzi wa jengo la kiwanda cha kutengeneza viatu cha Gereza Kuu Karanga kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro ambacho licha ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF (ambao ni wabia) kutoa shilingi Bilioni 9 tangu Oktoba 2019, hadi sasa Jeshi la Magereza limeshindwa kuharakisha ujenzi huo ambao umefikia asilimia 45 tu, ilihali mitambo inayopaswa kufungwa katika jengo hilo imeshawasili Bandari ya Dar es Salaam.
Alimuagiza Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike kuhakikisha majengo mapya 12 yaliyojengwa katika Gereza la Ukonga yanatunzwa na kuendeleza utaratibu wa kujenga nyumba za Maafisa na Askari wake pamoja na kukarabati zilizopo, kwa kuwa haridhishwi na hali duni ya makazi ya Maafisa na Askari Magereza hapa nchini.
Pia alimtaka CGP Kasike kuhakikisha maji yanaingizwa katika nyumba za makazi ya Maafisa na Askari Magereza katika majengo mapya 12 ya Ukonga, kwa kuwa wakati wa ukaguzi amebaini kuwa makazi hayo hayajaunganishwa na mtandao wa maji ndani ya nyumba.

ambao umejengwa na Jashi la Kujenga Taifa (JKT) chini ya usimamizi wa Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Charles Mbuge, Rais Dkt. Magufuli alisema kuwa amefurahi kuona mradi huo umekamilika.
Hata hivyo alilitaka Jeshi la Magereza kujitathimini kwa nini lishindwe kujenga nyumba zake lenyewe hadi lijengewe na JKT huku wakiwa na nguvukazi ya kutosha wakiwemo wafungwa na mahabusu.

You may also like

0 comments

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh