Zungu ateuliwa kuwa Waziri, Simbachawene amrithi Lugola Mambo ya Ndani

Rais Dkt. John Magufuli amemhamisha Wizara aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na, George Simbachawene, kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuchukua nafasi ya Kangi Lugola, ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Pia Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Mussa Azzan Zungu Mbunge wa Ilala, kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya […]

Rais Dkt. John Magufuli amemhamisha Wizara aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na, George Simbachawene, kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuchukua nafasi ya Kangi Lugola, ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Pia Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Mussa Azzan Zungu Mbunge wa Ilala, kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Muungano na Mazingira akichukua nafasi ya Simbachawene aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hayo yalibainishwa jana Ikulu jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Dkt. John Magufuli.
“Siku ya kuapishwa kwa mawaziri walioteuliwa itatangazwa baadaye,” alisema Balozi Kijazi.
Balozi Kijazi alibainisha pia kwmaba Rais Dkt. Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu akiwemo Meja Jenerali Jacob Kingu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kabla ya kuandaka barua ya kujiuzulu hapo juzi.
Wengine ni aliyekuwa Kamishina Jenerali wa Magereza Faustine Kasike na Dkt. John Steven Simbachawene, ambapo Balozi Kijazi alibainisha kuwa vituo vyao vya kazi vitatangazwa baadaye.
Aidha kwa mujibu wa Balozi Kijazi, Rais Dkt. Magufuli ametengua nafasi ya aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto nchini, Thobias Andengenye na nafasi yake itajazwa hapo baadaye.

0 comments

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh