Molell, Musiba wamchambua Zitto na genge lake

Kupeleka hoja binafsi Bungeni kuwa Zitto adui wa Taifa Mbunge wa Jimbo la Siha kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Godwin Molell anatarajia kupeleka hoja binafsi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwanini Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe asichukuliwe kama Adui wa Taifa hili. Molell alisema amefikia azma  hiyo dhidi ya Zitto ni […]

Kupeleka hoja binafsi Bungeni kuwa Zitto adui wa Taifa

Mbunge wa Jimbo la Siha kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Godwin Molell anatarajia kupeleka hoja binafsi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwanini Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe asichukuliwe kama Adui wa Taifa hili.

Molell alisema amefikia azma  hiyo dhidi ya Zitto ni kutokana na kitendo  cha Mbunge huyo wa Kigoma  kuandika Barua Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Human Rights Watch  Zama Neff ya kutaka Tanzania isipewe mkopo kwa madai kuwa pesa hiyo itatumiwa kisiasa na Serikali ya CCM.

Wakati Molell akiongea hayo,Mwanaharakati huru nchini Cyprian Musiba amesema, anatarajia kuandika barua Benki ya Dunia, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, utakaoelezea mambo mazuri yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John  Magufuli, na kuwataka  wapuuze maneno ya uongo yanayoenezwa watu wasiokuwa wema na nchgi yao.

Mbunge huyo wa Siha alisema, kupitia barua hiyo Zitto amezuia Shule za Bweni zaidi ya 1000 za kisasa ambazo ndio zilikuwa zijengwe kutokana na mkopo huo, ambazo zingeweza kusaidia watoto wa kike ambao wamekuwa na changamoto ya kupata mimba za utotoni.

‘’Hivi huyo Zitto ana akili kweli, yaani mtu anaandika barua Benki ya Dunia kupinga Tanzania isipewe mkopo kwa ajili ya ujenzi wa Shule za kike kwaajili ya ,maslahi yake binafsi, hakika huyu ni muhujumu uchumi’’, alisema Molell.

Mbunge huyo alisema sababu kubwa ya watoto wa kike kupata mimba za utotoni kunachangiwa na umaskini na umbali wa kutoka Shule hadi nyumbani, lakini Serikali ya Magufuli kwa upendo ikaomba mkopo kwa ajili ya kujenga mabweni ya watoto wa kike ili waweze kuepuka changamoto hiyo inayowakabili.

‘’Baada ya  Zitto na huyo mshirika wake kuandika barua ya kuzuia mkopo huo, eti mzungu mmoja  kutoka huko Benki ya Dunia ameleta barua Bungeni, ikihoji eti kwanini Tanzania ipewe pesa?, wakati hizo shule 1000 zitakazojengwa zitaokoa watoto wa kike 200,000 watakao lala katika mabweni hayo’’, alisema Mbunge huyo.

Molell ambaye pia ni mwanaharakati alisema, kwa mujibu wa barua hiyo Zitto anajifanya kama anatetea watoto wa kike,lakini ukweli anawahujumu na hana nia njema na watoto wa kike katika maendeleo yao.

‘’Kuna usemi usemao ukimuelimisha mtoto wa kike, umeelimisha jamii nzima, sasa Rais wetu kwa kulijua hilo alitaka pesa ya mkopo huo, ajenge Shule za Bweni 1000, ambazo zingesaidia watoto hao, lakini Zitto yuko kinyume na harakati njema za Mh. Rais, nafikiri huyu siyo mwenzetu’’, alisema Molell.

Aidha Mbunge huyo wa Siha alisema, anatarajia kuwasiliana na Spika wa Bunge Job Ndung’ai na wabunge wote wanaitakia mema nchi yao kuwapiga vita wanaohujumu Taifa hili kwa kuangalia maslahi yao binafsi.

‘’Kwa mfano huyu Zitto kama Mbunge aliapa kuilinda nchi na kulinda sheria na katiba ya nchi, sasa iweje huyo huyo alisema atailinda nchi, anaenda kubomoa nchi huko Ulaya?, alihoji Molell na kutaka Spika pamoja na wabunge wamchukulie Zitto ka Muhujumu Uchumi’’, alisema Mbunge huyo.

Wakati huo huo  Molell ameshangaa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na genge lake, wanatambea nchi za Ulaya wakiwa na maelezo ya vivutio vya Tanzania yakiwemo Madini, na kuwahadaa mabepari hao kuwa wakiwapa pesa na kufanikiwa kuingai Ikulu, eti wasaidia kuwapati Madini yaliyopo nchini.

‘’ Yaani Mbowe na genge lake ni wezi, amekiibia Chama chake, pesa za Ruzuku karibu Billioni 15, hazieleweki zimefanya kazi gani, kwani hawa wapinzani wapo kwaajili ya kupiga tu’’, alisema Molell.

Mbunge huyo aliziatak Asasi za kiraia kama wao wanatetea haki za binadamu, kwanini haziendi kuulizia wizi unaofaanywa na Mbowe CHADEMA na badala yake wanaisumbua Serikali ya Magufuli inayofanya mambo mazuri.

Mwanaharakati huyo alisema kuwa, katika barua hiyo atakayoandika  mazuri ya Serikali ya  Magufuli, kivuli cha barua hiyo itapelekwa kwa Watanzania waishio nje ya nchi maarufu kwa jina la Diaspora na nyingine atapeleka kwa Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Paramagamba Kabudi.

Aidha kufuatia mambo yanayofanywa na Mbunge huyo wa Kigoma, Musiba alisema wao kama wanaharakati  hawawezi kukubali kuona Serikali na Rais Magufuli inachafuliwa wakati wao wapo.

‘’Yaani Zitto anaandika barua kwa Mataifa ya nje kwa kutumia Nembo ya Bunge, kuichafua nchi na Rais wake, sasa naomba Serikali isijibu hiyo barua, na badala yake watuachie sisi wanaharakati tupo kuitetea nchi yetu, hii ndio kazi yetu’, alisema Musiba.

 

Aidha Mwanaharakati huyo alaisema kufuatia barua hiyo ya akina Zitto kupinga ujenzi wa mabweni hayo, inaashiria kuwa Mbunge huyo wa Kigoma anachochea mimba za utotoni kwa watoto wa kike na hana nia nzuri.

‘’Hivi huyu Zitto hana watoto kweli? yeye kama mzazi anawezaje kuandika barua ya kupinga isiletwe pesa hapa nchini kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya watoto wa Kike, hiyo inaoonesha anachochea uzinzi kwa watoto wetu’, alisema Musiba.

 

 

Aidha Musiba ameitaka Benki ya Dunia impuuze Zitto na genge lake, kwani benki hiyo na Tanzania wamekuwa na uhusiano mzuri tangu enzi za Mwalimu Nyerere na Taifa hili halina uhusiano mbaya na Matifa ya nje.

Vilevile Musiba alisema, Zitto ameungana na Tundu Lisu, na Nassoro Mazrui wanafanya ziara Mataifa ya Ulaya, kuomba pesa kwa ajili ya kuharibu Uchaguzi  Mkuu ujao kwa kuunda makundi ya vijana kuleta vurugu katika Uchaguzi Mkuu wa Urais, Wabunge na Madiwani mwishoni mwa mwaka huu.

‘’Wanachokifanya Zitto na genge lake wanaichonganisha Serikali na Mataifa rafiki, ili yasiwe na ushirikiano mzuri na Tanzania, hivyo Serikali isiwaonee huruma watu hawa’’, alisema Mwanaharakati huyo.

Aidha Musiba  alisema kuwa, Maalim Seif  akiwa mshauri Mkuu wa genge hilo, wamelenga kufanya vurugu hizo Zanzibar, ili ipatikane Serikali ya Kitaifa ambayo wanalenga kuwemo katika uongozi wa Serikali hiyo,

‘’Zitto na genge lake wanataka kuunda vikundi vya vijana Visiwani Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu, na itokee vurugu kama iliyotokea miaka ya 90 ikapatikana Serikali ya Kitaifa, Maalim akiwemo.

Mwanaharakati huyo ameeleza kuwa, Zitto anajua hawezi kurudi Bungeni hivyo anataka kutumia njia hiyo ili yeye na wenziwe waweze kupata madaraka ya Kitaifa huko Zanzibar, hivyo amewataka Watanzania kuwa makini na makundi hayo yatakayokuwa yakiratibiwa na Chama cha Siasa cha ACT Wazalendo.

You may also like

0 comments

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh