Dkt. Mnyepe ashika Usukani Wizara ya Ulinzi na JKT

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe  amekabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Dkt. Florens Turuka na kuanza kazi mara moja huku akiahidi kushirikiana vema na watumishi. Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Ulinzi na JKT zililopo katika Mji mpya wa Serikali Mtumba Jijini […]

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akisalimiana na Watumishi wa Wizara ya Ulinzi na JKT alipowasili kwa ajili ya kuripoti katika kituo chake kipya cha kazi Mtumba Jijini Dodoma nyuma yake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Florens Turuka aliyestaafu utumishi wake.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe  amekabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Dkt. Florens Turuka na kuanza kazi mara moja huku akiahidi kushirikiana vema na watumishi.

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Ulinzi na JKT zililopo katika Mji mpya wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma Dkt. Mnyepe alilakiwa na Watumishi wa Wizara hiyo wakiongozwa na Dkt. Florens Turuka ambaye amestaafu utumishi kwa umri.

Baadaye tukio la makabidhiano lilifanyika katika ukumbi wa Wizara na kuhudhuriwa na Makamishna, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Ulinzi na JKT.

Akizungumza baada ya kumkabidhi nyaraka mbalimbali za Wizara Katibu Mkuu anayemaliza muda wake wa Utumishi Dkt. Florens Turuka aliwashukuru Makamishna, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na watumishi kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu Wizarani hapo.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akisaini kitabu cha wageni muda mfupi kabla ya kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake aliyesimama pembeni Dkt. Florens Turuka ambaye amestaafu utumishi kwa umri.

Dkt. Turuka alisema “daima nitaukumbuka mchango mkubwa nilioupata kwa Makamishna, Wakuu wa Idara, Vitengo na watumishi wote wa Wizara hii, kwani hakuna kazi iliyoshindikana chini yao”

“Namshukuru mwenyezi Mungu kuwa niliingia Wizara ya Ulinzi mwaka 2016 na mpaka nastaafu utumishi wangu nimejifunza mambo mengi saana yanayohusu Ulinzi wa nchi yetu” Alisema Dkt. Turuka

Naye Katibu Mkuu mpya Dkt. Faraji Mnyepe akiongea na Makamishna, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alianza kwa kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kisha akamshukuru Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kumuamini na kumteua kuongoza Wizara nyingine nyeti.

“Nimetoka kuongoza Wizara nyeti ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki sasa nipo Wizara ya Ulinzi na JKT ambayo kuna mambo mengi ya msingi yanahusiana kabisa” Alisema Dkt. Mnyepe

Dkt. Mnyepe alisema katika kufanya kazi kwake siku zote yeye amekuwa akiamini ‘Timu Work’ ambapo pamoja na mambo mengine mfumo huu ndiyo wenye mafanikio na ufanisi mkubwa katika kazi.”

Dkt. Florens Turuka Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi anayemaliza muda wake wa Utumishi akimkarisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe katika ofisi yake mpya Mtumba Jijini Dodoma.

Akitoa neon la shukrani kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo Kaimu Kamishna wa Rasilimali watu Wizara ya Ulinzi na JKT Marco Baruti alimshukuru saana Katibu Mkuu anayeondoka na kusema siku zote walimuona kama Mwalimu kwao kwa mambo mbalimbali aliyokuwa akiwafundisha pindi wanapokosea

Pia akamkaribisha Katibu Mkuu mpya na kumuahidi ushirikiano mkubwa katika kufanikisha shughuli za Serikali na kuifanya Wizara ya Ulinzi iendelee kuwa katika hali yake.

Februari 06 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimteua Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kufuatia Dkt. Florens Turuka kustaafu wadhifa huo kwa umri.

You may also like

0 comments

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh