Msanii wa nyimbo za injili Rwanda ajinyonga

Msanii wa nyimbo za injili Rwanda ajinyonga  Jeshi la Polisi nchini Rwanda limetangaza kifo cha mwimbaji wa injili Kizito Mihigo ambaye alikutwa amefariki gerezani baada ya kujinyonga. Mwaka mmoja na nusu baada ya kuachiliwa huru kwa msamaha wa Rais, Mihigo alikamatwa tena Februari 13, 2020. Alikuwa anashtakiwa kwa makosa yanayaohusu kutaka kuvuka mpaka wa Burundi […]

Msanii wa nyimbo za injili Rwanda ajinyonga 

Jeshi la Polisi nchini Rwanda limetangaza kifo cha mwimbaji wa injili Kizito Mihigo ambaye alikutwa amefariki gerezani baada ya kujinyonga.

Mwaka mmoja na nusu baada ya kuachiliwa huru kwa msamaha wa Rais, Mihigo alikamatwa tena Februari 13, 2020.

Alikuwa anashtakiwa kwa makosa yanayaohusu kutaka kuvuka mpaka wa Burundi kinyume cha sheria ili ajiunge na makundi yenye silaha.

Katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter jana, Jeshi hilo lilibaini kwamba mwimbaji huyo alikutwa amefariki akiwa kwenye chumba chake alipokuwa anazuiliwa majira ya saa 11:00 alfajiri.

Mamlaka ilisema kuwa mwimbaji huyo alijiua, bila kutoa maelezo zaidi, na kuongeza kwamba imeanzisha uchunguzi.

Mwimbaji huyo wa Injili alikuwa kizuizini katika kituo cha polisi cha Remera katika mji mkuu Kigali kwa siku tatu. Alikamatwa Februari 13 katika Wilaya ya Nyaruguru, Kusini Mashariki mwa Rwanda.

Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda (RIB) ilikuwa inamshutumu kwa makosa yanayohusiana na kutaka kuvuka mpaka wa Burundi kinyume cha sheria ili ajiunge na makundi yenye silaha, na kwa kujaribu kutoa hongo kwa wanakijiji ambao walimuona.

Tangu kukamatwa kwake, ndugu zake walielezea mshangao wao kusikia habari hizo za kutaka kuvuka mpaka kuingia nchini Burundi, na kuhakikisha kwamba hakuwa amewaambia kuhusu mpango wa kuondoka nchini humo.

Kizito Mihigo hapo awali alionekana kama mtetezi wa maridhiano na mmoja wa waimbaji mashuhuri nchini Rwanda.

Mihigo alikamatwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2014. Wakati huo alitoweka kwa siku kadhaa kabla ya mamlaka kuthibitisha kukamatwa kwake.

Mwimbaji huyo alikuwa mmoja wa manusura wa mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994, alifungwa jela kwa kipindi cha miaka minne, akishutumiwa na makosa ya kula njama dhidi ya kuhatarisha usalama dhidi ya Rwanda.

Mwishowe aliachiliwa huru Septemba 2018 kwa uamuzi wa Rais Paul Kagame, pamoja na mpinzani Victoire Ingabire.

You may also like

0 comments

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh