Africa

Msanii wa nyimbo za injili Rwanda ajinyonga 

Jeshi la Polisi nchini Rwanda limetangaza kifo cha mwimbaji wa injili Kizito Mihigo ambaye alikutwa amefariki gerezani baada ya kujinyonga.

Mwaka mmoja na nusu baada ya kuachiliwa huru kwa msamaha wa Rais, Mihigo alikamatwa tena Februari 13, 2020.

Alikuwa anashtakiwa kwa makosa yanayaohusu kutaka kuvuka mpaka wa Burundi kinyume cha sheria ili ajiunge na makundi yenye silaha.

Katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter jana, Jeshi hilo lilibaini kwamba mwimbaji huyo alikutwa amefariki akiwa kwenye chumba chake alipokuwa anazuiliwa majira ya saa 11:00 alfajiri.

Mamlaka ilisema kuwa mwimbaji huyo alijiua, bila kutoa maelezo zaidi, na kuongeza kwamba imeanzisha uchunguzi.

Mwimbaji huyo wa Injili alikuwa kizuizini katika kituo cha polisi cha Remera katika mji mkuu Kigali kwa siku tatu. Alikamatwa Februari 13 katika Wilaya ya Nyaruguru, Kusini Mashariki mwa Rwanda.

Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda (RIB) ilikuwa inamshutumu kwa makosa yanayohusiana na kutaka kuvuka mpaka wa Burundi kinyume cha sheria ili ajiunge na makundi yenye silaha, na kwa kujaribu kutoa hongo kwa wanakijiji ambao walimuona.

Tangu kukamatwa kwake, ndugu zake walielezea mshangao wao kusikia habari hizo za kutaka kuvuka mpaka kuingia nchini Burundi, na kuhakikisha kwamba hakuwa amewaambia kuhusu mpango wa kuondoka nchini humo.

Kizito Mihigo hapo awali alionekana kama mtetezi wa maridhiano na mmoja wa waimbaji mashuhuri nchini Rwanda.

Mihigo alikamatwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2014. Wakati huo alitoweka kwa siku kadhaa kabla ya mamlaka kuthibitisha kukamatwa kwake.

Mwimbaji huyo alikuwa mmoja wa manusura wa mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994, alifungwa jela kwa kipindi cha miaka minne, akishutumiwa na makosa ya kula njama dhidi ya kuhatarisha usalama dhidi ya Rwanda.

Mwishowe aliachiliwa huru Septemba 2018 kwa uamuzi wa Rais Paul Kagame, pamoja na mpinzani Victoire Ingabire.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Nasser Bourita  amelalamikia kitendo cha kutoalikwa nchi yake kushiriki mkutano wa amani ya Libya mjini Berlin, Ujerumani na kusema kuwa vigezo vinavyotumiwa kuchagua nchi kushiriki katika mkutano huo vinaibua maswali mengi.

Bourita alisema katika mazungumzo na televisheni ya al Jazeera kuwa Morocco ikiwa nchi jirani na Libya imeshangazwa na kutoalikwa kwenye mkutano huo.

Waziri Mkuu huyo wa Morocco aliongeza kuwa moja ya matatizo ya mkutano wa Berlin ni washiriki wa mkutano huo.

Tunisia pia ilikataa mwaliko huo ikilalamimika kwamba imepewa mwaliko huo kwa kuchelewa kwa ajili ya kushiriki katika mkutano huo wa Berlin.

Kutoalikwa Morocco na kutoshiriki Tunisia ambazo ni nchi jirani na Libya katika eneo la kaskazini mwa Libya katika mkutano wa Berlin na wakati huo huo kualikwa nchi kama Imarati na Uingereza, kunatilia shaka vigezo vilivyotumiwa kuchagua nchi za washiriki katika mkutano huo.

Pande zinazopigana nchini Libya Januari 13 mwaka huu zilikutana Moscow nchini Urusi kwa ajili ya kusaini mapatano rasmi ya usitishaji vita.

Hata hivyo Jenerali Khalifa Haftar kamanda wa wanamgambo wanaojiita jeshi la kitaifa la Libya, mwishoni mwa mazungumzo hayo alikataa kusaini mapatano hayo.

Mkutano huo wa Berlin ulimalizika juzi kwa pande zote zilizoshiriki kukubaliana juu ya suala la kutouunga mkono au kuusaidia upande wowote kati ya makundi yanayozozana nchini Libya.

Vilevile uliszisitiza udharura wa kudumishwa vikwazo vya silaha dhidi ya Libya.

Balozi-wa-Tanzania-nchini-Ujerumani-Dr.Abbdallah-Possi-akiwa-pamoja-na-Bi.Upendo-Fölsen-Mwenyekiti-Umoja-wa-Tanzania-Ujerumani

Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani (UTU ) Mwalimu Bi.Venessa Upendo Fölsen siku ya jumamosi aliongoza kamati ya uongozi wa umoja huo katika kikao cha kukutana na balozi wa Tanzania nchini ujerumani Mheshimiwa Dkt.Abdallah Possi katika ubalozi wa Tanzania mjini Berlin,ambako ubalozi uliwakaribisha kwa mikono miwili na kufanya mazungumzo nao ambayo Kiongozi wa umoja wa Tanzania Ujerumani amelezea kuwa Umoja huo utaitangaza Tanzania nchini ujerumani kwa nguvu zote kwa maslahi ya Tanzania na watanzania,ususani katika sekta ya

Mwalimu-Bi.Venessa-Upendo-Fölsen-Mwenyekiti-wa-Umoja-wa-Tanzania-Ujerumani

Utalii,uwekezaji,afya na elimu ni mojawapo ya mambo yakatayopewa kipau mbele,Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani ndio mwamvuli pekee unawakusanya watanzania waishio nchini ujerumani na moja ya niya yake ni kuleta mshikamano wenye kuleta maslahi kwa watanzania ujerumani na nyumbani Tanzania.Pia kwa upande wake Mheshimiwa Balozi Dkt. Abdallah Possi amewataka watanzania kuungana pamoja kwa maslahi yao na ya Tanzania,pia kujivunia utanzania wao kwa kuitangaza vema Tanzania katika nyanza zote na vivutio vyake katika tufe la dunia ili kufanikisha Tanzania ya Viwanda itakayokuza uchumi.

BOSTON, MAREKANI

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) na Makamu wa Tatu wa Rais wa
Shirikia la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt.
Agnes Kijazi, amewataka watendaji wa Shirika la
Hali ya Hewa Duniani (WMO) kuandaa mpango wa
pamoja wa kuboresha zaidi uaandaaji na
uwasilishwaji  wa taarifa za hali ya hewa kwa jamii
zinazoishi katika mazingira hatarishi.
Dkt. Kijazi aliyasema hayo wakati akichangia mada
katika mkutano ulioandaliwa na WMO kwa
kushirikiana na Taasisi ya Hali ya hewa ya
Marekani “National Oceanic and Atmospheric
Administration (NOAA)- National Weather
Service,” uliofanyika Januari 11, 2020 Boston,
nchini Marekani.
Lengo la mkutano huo  lilikuwa kujadili uboreshaji
wa uandaaji na uwasilishwaji wa taarifa za hali ya
hewa  kwa jamii zinazoishi katika mazingira
hatarishi, hususan visiwa vilivyopo katika ukanda
wa tropic na arctic (Improving Communication and
Preparedness in Vulnerable Regions and

Underserved Communities of the tropical and
Arctic region islands), ambavyo viko katika
mazingira hatarishi ya kukumbwa na vimbunga na
mawimbi ya tsunami.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi
wa WMO, ikiwa ni pamoja na Rais wa WMO Prof.
Gerhard Adrian, Makamu wa kwanza wa Rais wa
WMO Prof. Celeste Saulo, Makamu wa Pili wa Rais
wa WMO Ndugu Albert Martis na Makamu wa
Tatu wa Rais wa WMO Dkt. Agnes Kijazi.
Wengine ni Katibu Mkuu wa WMO, Prof. Petteri
Taalas, Wakuu wa Taasisi za hali ya hewa kutoka
baadhi ya nchi wanachama wa WMO na wadau wa
huduma za hali ya hewa, miongoni mwao ikiwa ni
sekta binafisi na watafiti kutoka Vyuo Vikuu.
Majadiliano ya mkutano huo yalijielekeza zaidi
katika matokeo ya tafiti zilizofanyika katika nchi
za Guyana, Finland, Indonesia, Marekani (Jimbo la
Alaska), visiwa vya Caribbean na Bahamas, pamoja
na eneo la Pacific zilizowasilishwa.

Tafiti hizo ziliainisha changamoto katika uandaaji
na uwasilishwaji wa taarifa za hali ya hewa kwa
jamii zinazoishi katika mazingira hatalishi ya
kukumbwa na majanga yanayotokana na hali mbaya
ya hewa, ambayo hutokea katika maeneo hayo.
Vile vile, tafiti hizo ziliainisha njia za asili
zinazotumiwa na jamii hizo katika kuchukua
tahadhari  na kutoa mapendekezo ya kuboresha ili
kupunguza maafa yanayotokana na majanga hayo.
Akichangia mada, Dkt. Kijazi alifafanua kwamba
kwa kuwa changamoto zilizowasilishwa zinaweza
kuwepo katika maeneo mengi, yakiwemo maeneo
yanayofanana na hayo yaliyopo katika bara la
Afrika, ni vyema kuandaa mpango wa pamoja
utakaoratibiwa na WMO wa kushughulikia
changamoto hizo.

Hivyo, akawataka watendaji wa WMO kuangalia
uwezekano wa kuandaa mpango huo ili kuboresha
zaidi uaandaaji na uwasilishwaji  wa taarifa za hali
ya hewa kwa jamii husika.

Ili kuharakisha utatuzi wa
changamoto  zilizowasilishwa, viongozi waandamizi
wa WMO (Rais, Makamu wa Rais wote watatu na
Katibu Mkuu) wameazimia kufanya vikao kwa njia
ya mtandao (teleconference) kila mwisho wa
mwezi, kuanzia mwezi Januari 2020.

Mkutano huu ni sehemu ya mkutano mkuu wa 100
wa wadau wa huduma za hali ya hewa wa
Marekani  unaofanyika Boston, Marekani kuanzia
tarehe 10 hadi 16 Januari, 2020 kujadili
utekelezaji wa maazimio ya mkutano mkuu wa
WMO uliofanyika Juni 2019. Dkt. Kijazi anashiriki
katika mkutano huo kama Makamu wa Tatu wa Rais
wa WMO.
CAPTION
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) na Makamu wa Tatu wa Rais wa
Shirikia la Hali ya Hewa Duniani (WMO)
akifafanua jambo walipokutana na Mkurugenzi wa
Taasisi ya Hali ya Hewa ya Canada (ambaye pia ni

msaidizi wa Naibu Waziri mwenye dhamana ya
masuala ya hali ya hewa), Diane Campbell kwa
maongezi mafupi wakati wa mapumziko nje ya
ukumbi wa mkutano Boston nchini Marekani.

*Awataka kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya Tanzania *Atoa wiki mbili wawe wameripoti kwenye vituo vyao vya kazi

RAIS Dkt. John Magufuli amewaagiza mabolizi aliowaapisha kuhakikisha wanakwenda kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya Tanzania.

Mabalozi hao ni Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini na Dkt. Modestus Francis Kipilimba anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Namibia.

Wengine ni Profesa Emmanuel David Mwaluko Mbennah anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe na Dkt. Benson Alfred Bana kuwa Balozi Tanzania nchini Nigeria.

Rais Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya Mbalozi hao kula kiapo hicho ambapo aliwaeleza kuwa wote wanakwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mataifa muhimu ambayo kama yakitumiwa vizuri yatainufaisha Tanzania kiuchumi.

“Niwapongeze wote kwa kuteuliwa kuwa mabalozi, mkafanye majukumu yenu kwa manufaa ya Taifa letu,” alisema Rais Dkt. Magufuli.

Rais Dkt. Magufuli aliwaagiza mabalozi wote wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye nchi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuhakikisha wanatekeleza mikakati iliyopitishwa na jumuiya hiyo.

Alitumia fursa hiyo kuhakikisha ndani ya wiki mbili wanaripoti kwenye vituo vyao vya kazi na kuwataka wakatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi akitoa salaamu katika hafla hiyo, aliwataka mabalozi wanaiwakilisha Tanzania katika nchi za SADC kuhakikisha wanasimamia mambo ambayo Marais wa nchi hizo walikubalana na Rais Dkt. Magufuli alipozitembelea.

Akitoa maagizo kwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi alimtaka kuhakikisha fursa ambayo Tanzania iliipata kuhusu ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili nchini humo anaifuatilia na kujua hatua iliyofikia.

Profesa Kabudi alibainisha kuwa kama sio juhudi za Rais Dkt. Magufuli fursa hiyo Tanzania ilishaikosa.

Hivyo alimtaka akiripoti tu nchini humo jambo la kwanza liwe ni kukutana na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo, kwamba kabla ya mwezi wa pili atoe ripoti ya kinachoendelea juu ya suala hilo.

Kadhalika alimuagiza kufuatilia na kujua suala la ushirikiano baina ya Shule ya Chifu Albert Lithui iliyopo Mazimbu mkoani Morogoro na shule yoyote nchini Afrika Kusini limefikia wapi.

Ikumbukwe kuwa Agosti mwaka jana Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alipotembelea nchini alifika katika shule hiyo na kuahidi kuanzisha ushirikano baina ya shule hiyo na shule yoyote ya nchini kwake kutokana na historia muhimu ya nchi hiyo na mahali hapo.

Profesa Kabudi akizungumzia Balozi wa Tanzania nchini Namibia Dkt. Modestus Francis Kipilimba, alieleza kuwa ubalozi huo ni mpya kuanzishwa nchini humo kufuatia makubaliano baina ya Rais Dkt. John Magufuli na Rais Hage Geingob.

Hivyo alimweleza kuwa anakwenda kuanzisha kituo muhimu, kwamba Serikali imeshamhakikishia nyumba na ofisi atakayokwenda kuanzia kazi ambapo alimuagiza kufuatilia kwenye ushirikiano katika uvuvi wa bahari kuu na masuala ya nyama.

Kwa upande wa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Profesa Emmanuel David Mwaluko Mbennah alikumbushwa kuwa ziara ya Rais Dkt. Magufuli nchini humo ilikuwa na matumaini makubwa kwa wananchi wa nchi hiyo.

Hususan pale ambapo Rais Dkt. Magufuli alipotoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuiondolea vikwazo vya kiuchumi, hivyo alimuagiza kuendeleza mahusiano hayo. Kadhalika alimpa mwezi mmoja kuhakikisha analeta ripoti kuhusiana na fursa zinazopatikana nchini humo.

Profesa Kabudi akitoa maagizo kwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dkt. Benson Alfred Bana, alimuagiza kuhakikisha anainufaisha Tanzania kujifunza kuhusu masuala ya kilimo.

Hivyo alimtaka kutumia fursa hiyo kuimarisha ushirikiano zaidi na nchi ya Ivory Coast ambayo ni mahili katika masuala ya kilimo cha Korosho na Kahawa.

RAIS Dkt. John Magufuli amewasili Visiwani Zanzi- bar kwa ziara ya kikazi.

Akiwasili jana visiwani humo majira ya saa nane mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume alipokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Baada ya mapokezi hayo Rais Dkt. Magufuli alishuhudia vikundi mbal- imbali vya ngoma ambavyo vilikuwa vimeandaliwa kwa ajili yake.

Rais Dkt. Magufuli ana- fanya ziara hiyo baada ya kutoka mikoa ya Kanda ya ziwa ambapo aliwasili jijini Dar es Salaam juzi kisha jana kuanza ziara hiyo.

Katika ziara hiyo Rais Dkt. Magufuli atazindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kushiriki sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Mkuru- genzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa ilisema kuwa Januari 10, 2020 Rais Dkt. Magufuli anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku tano visiwani humo.

“Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli aliyekuwa ma- pumzikoni nyumbani kwake, Chato mkoani Gei- ta amewasili leo (juzi) Al- hamisiJanuari9,2020jijini Dar es Salaam.

“Mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini DaresSalaam akiwa na mkewe, Janeth, Rais Dkt. Magufuli amesalimia na baadhi ya wafanyakazi katika uwanja huo,” alisema.

Alisema miongoni mwa masuala yatakayofanyiwa kazi wakati akiwa Zanzibar ni kuweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar.

Leo Januari 11, 2020 Rais Dk. Magufuli ataweka jiwe la msingi la shule ya sekondari ya Mwanakw- erekwe iliyopo Mjini Ma- gharibi na atafungua hoteli yenye hadhi ya nyota tano iitwayo Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa ili- yopo Mtoni.

Rais Dkt. John Magufuli akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Baloz Seif Ali Idi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aman Abeid Karume.

 

Rais Dkt. Magufuli atashiriki Sherehe za Maa- dhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitakazofanyika Jumapili Januari 12, 2020 katika uwanja wa Amaan, Mjini Magharibi.

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh