Bunge

Spika Mstaafu, Mhe. Anne Makinda (wa pili kulia mbele) katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi ya Bunge nje ya ofisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto mbele ni Katibu wa Bunge, Ndg.Stephen Kagaigai
Spika wa Bunge Mstaafu, Mhe. Anne Makinda akiteta jambo na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai walipokutana leo katika ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, Ndg. Daniel Eliufoo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni jijini Dodoma, Februari 6, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali kutoka kwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni Freeman Mbowe, bungeni jijini Dodoma, Februari 6, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Serikali imeandaa programu mbalimbali za kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti
zaidi ya bilioni moja katika eneo la Mlima Kilimanjaro ili kukabiliana na matatizo ya mabadiliko
ya tabia nchi.
Akijibu swali leo Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano
na Mazingira, Mussa Zungu alisema,“Programu ya kwanza ni kupanda miti zaidi ya bilioni moja
katika eneo la Mlima Kilimanjaro ili kulinda barafu iliyopo katika nchi yetu, pamoja na kuanza
mkakati wa kuomba fedha zilizopo katika Mfuko mpya ulioanzishwa na nchi ya Ufaransa, wa
dola za kimarekani bilioni 100, ulioanzishwa kwa lengo la kuboresha mazingira katika nchi
zenye uhitaji, ikiwemo Tanzania”.
Aidha, Waziri Zungu aliongeza kuwa mkakati huo wa kupanda miti na kuitunza hivi sasa
unaandaliwa katika wilaya zote nchini, na miti itakayopandwa katika kila wilaya itakuwa ya aina
maalumu ili kuendana na mazingira yaliyopo katika wilaya husika.
“Nchi yetu imebarikiwa kuwa na asilimia 39.9 ya misitu, misitu hii inapotea, kuanzia mwaka
1990 hadi mwaka 2010 tumeshapoteza takribani ekari milioni 8 ya misitu, na hii ni hatari
kubwa sana kwa watanzania, tuhakikishe tunaacha kukata miti, tutumie miti kama fursa ya
kibiashara, badala ya kuikata tuweke mazao ya nyuki”, amesisitiza Waziri Zungu.

Kupeleka hoja binafsi Bungeni kuwa Zitto adui wa Taifa

Mbunge wa Jimbo la Siha kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Godwin Molell anatarajia kupeleka hoja binafsi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwanini Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe asichukuliwe kama Adui wa Taifa hili.

Molell alisema amefikia azma  hiyo dhidi ya Zitto ni kutokana na kitendo  cha Mbunge huyo wa Kigoma  kuandika Barua Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Human Rights Watch  Zama Neff ya kutaka Tanzania isipewe mkopo kwa madai kuwa pesa hiyo itatumiwa kisiasa na Serikali ya CCM.

Wakati Molell akiongea hayo,Mwanaharakati huru nchini Cyprian Musiba amesema, anatarajia kuandika barua Benki ya Dunia, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, utakaoelezea mambo mazuri yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John  Magufuli, na kuwataka  wapuuze maneno ya uongo yanayoenezwa watu wasiokuwa wema na nchgi yao.

Mbunge huyo wa Siha alisema, kupitia barua hiyo Zitto amezuia Shule za Bweni zaidi ya 1000 za kisasa ambazo ndio zilikuwa zijengwe kutokana na mkopo huo, ambazo zingeweza kusaidia watoto wa kike ambao wamekuwa na changamoto ya kupata mimba za utotoni.

‘’Hivi huyo Zitto ana akili kweli, yaani mtu anaandika barua Benki ya Dunia kupinga Tanzania isipewe mkopo kwa ajili ya ujenzi wa Shule za kike kwaajili ya ,maslahi yake binafsi, hakika huyu ni muhujumu uchumi’’, alisema Molell.

Mbunge huyo alisema sababu kubwa ya watoto wa kike kupata mimba za utotoni kunachangiwa na umaskini na umbali wa kutoka Shule hadi nyumbani, lakini Serikali ya Magufuli kwa upendo ikaomba mkopo kwa ajili ya kujenga mabweni ya watoto wa kike ili waweze kuepuka changamoto hiyo inayowakabili.

‘’Baada ya  Zitto na huyo mshirika wake kuandika barua ya kuzuia mkopo huo, eti mzungu mmoja  kutoka huko Benki ya Dunia ameleta barua Bungeni, ikihoji eti kwanini Tanzania ipewe pesa?, wakati hizo shule 1000 zitakazojengwa zitaokoa watoto wa kike 200,000 watakao lala katika mabweni hayo’’, alisema Mbunge huyo.

Molell ambaye pia ni mwanaharakati alisema, kwa mujibu wa barua hiyo Zitto anajifanya kama anatetea watoto wa kike,lakini ukweli anawahujumu na hana nia njema na watoto wa kike katika maendeleo yao.

‘’Kuna usemi usemao ukimuelimisha mtoto wa kike, umeelimisha jamii nzima, sasa Rais wetu kwa kulijua hilo alitaka pesa ya mkopo huo, ajenge Shule za Bweni 1000, ambazo zingesaidia watoto hao, lakini Zitto yuko kinyume na harakati njema za Mh. Rais, nafikiri huyu siyo mwenzetu’’, alisema Molell.

Aidha Mbunge huyo wa Siha alisema, anatarajia kuwasiliana na Spika wa Bunge Job Ndung’ai na wabunge wote wanaitakia mema nchi yao kuwapiga vita wanaohujumu Taifa hili kwa kuangalia maslahi yao binafsi.

‘’Kwa mfano huyu Zitto kama Mbunge aliapa kuilinda nchi na kulinda sheria na katiba ya nchi, sasa iweje huyo huyo alisema atailinda nchi, anaenda kubomoa nchi huko Ulaya?, alihoji Molell na kutaka Spika pamoja na wabunge wamchukulie Zitto ka Muhujumu Uchumi’’, alisema Mbunge huyo.

Wakati huo huo  Molell ameshangaa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na genge lake, wanatambea nchi za Ulaya wakiwa na maelezo ya vivutio vya Tanzania yakiwemo Madini, na kuwahadaa mabepari hao kuwa wakiwapa pesa na kufanikiwa kuingai Ikulu, eti wasaidia kuwapati Madini yaliyopo nchini.

‘’ Yaani Mbowe na genge lake ni wezi, amekiibia Chama chake, pesa za Ruzuku karibu Billioni 15, hazieleweki zimefanya kazi gani, kwani hawa wapinzani wapo kwaajili ya kupiga tu’’, alisema Molell.

Mbunge huyo aliziatak Asasi za kiraia kama wao wanatetea haki za binadamu, kwanini haziendi kuulizia wizi unaofaanywa na Mbowe CHADEMA na badala yake wanaisumbua Serikali ya Magufuli inayofanya mambo mazuri.

Mwanaharakati huyo alisema kuwa, katika barua hiyo atakayoandika  mazuri ya Serikali ya  Magufuli, kivuli cha barua hiyo itapelekwa kwa Watanzania waishio nje ya nchi maarufu kwa jina la Diaspora na nyingine atapeleka kwa Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Paramagamba Kabudi.

Aidha kufuatia mambo yanayofanywa na Mbunge huyo wa Kigoma, Musiba alisema wao kama wanaharakati  hawawezi kukubali kuona Serikali na Rais Magufuli inachafuliwa wakati wao wapo.

‘’Yaani Zitto anaandika barua kwa Mataifa ya nje kwa kutumia Nembo ya Bunge, kuichafua nchi na Rais wake, sasa naomba Serikali isijibu hiyo barua, na badala yake watuachie sisi wanaharakati tupo kuitetea nchi yetu, hii ndio kazi yetu’, alisema Musiba.

 

Aidha Mwanaharakati huyo alaisema kufuatia barua hiyo ya akina Zitto kupinga ujenzi wa mabweni hayo, inaashiria kuwa Mbunge huyo wa Kigoma anachochea mimba za utotoni kwa watoto wa kike na hana nia nzuri.

‘’Hivi huyu Zitto hana watoto kweli? yeye kama mzazi anawezaje kuandika barua ya kupinga isiletwe pesa hapa nchini kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya watoto wa Kike, hiyo inaoonesha anachochea uzinzi kwa watoto wetu’, alisema Musiba.

 

 

Aidha Musiba ameitaka Benki ya Dunia impuuze Zitto na genge lake, kwani benki hiyo na Tanzania wamekuwa na uhusiano mzuri tangu enzi za Mwalimu Nyerere na Taifa hili halina uhusiano mbaya na Matifa ya nje.

Vilevile Musiba alisema, Zitto ameungana na Tundu Lisu, na Nassoro Mazrui wanafanya ziara Mataifa ya Ulaya, kuomba pesa kwa ajili ya kuharibu Uchaguzi  Mkuu ujao kwa kuunda makundi ya vijana kuleta vurugu katika Uchaguzi Mkuu wa Urais, Wabunge na Madiwani mwishoni mwa mwaka huu.

‘’Wanachokifanya Zitto na genge lake wanaichonganisha Serikali na Mataifa rafiki, ili yasiwe na ushirikiano mzuri na Tanzania, hivyo Serikali isiwaonee huruma watu hawa’’, alisema Mwanaharakati huyo.

Aidha Musiba  alisema kuwa, Maalim Seif  akiwa mshauri Mkuu wa genge hilo, wamelenga kufanya vurugu hizo Zanzibar, ili ipatikane Serikali ya Kitaifa ambayo wanalenga kuwemo katika uongozi wa Serikali hiyo,

‘’Zitto na genge lake wanataka kuunda vikundi vya vijana Visiwani Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu, na itokee vurugu kama iliyotokea miaka ya 90 ikapatikana Serikali ya Kitaifa, Maalim akiwemo.

Mwanaharakati huyo ameeleza kuwa, Zitto anajua hawezi kurudi Bungeni hivyo anataka kutumia njia hiyo ili yeye na wenziwe waweze kupata madaraka ya Kitaifa huko Zanzibar, hivyo amewataka Watanzania kuwa makini na makundi hayo yatakayokuwa yakiratibiwa na Chama cha Siasa cha ACT Wazalendo.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipandisha bendera kabla ya uzinduzi wa tawi la Simba Bunge ‘Wekundu wa Mjengoni’ nje ya lango kuu la kuingia Bungeni tukio lililofanyika leo Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akikata utepe katika uzinduzi wa tawi la Simba Bunge ‘Wekundu wa Mjengoni ’ nje ya lango kuu la kuingia Bungeni tukio lililofanyika leo Jijini Dodoma. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Simba, Ndg. Senzo Mazingiza na Msemaji wa Klabu ya Simba, Ndg. Haji Manara (kushoto)

Bunge limeazimia kwamba Serikali itumie Taasisi ya Umma ya Wakala Mtandao (E – Government) kusimamia na kuratibu shughuli zinazoendelea za uwekaji mifumo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA).

Ushauri huo ulitolewa bungeni jana na Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC), Naghenjwa Kaboyoka wakati akiwasilisha taarifa ya shughuli za kamati kwa mwaka 2019 ambayo imeanisha changamoto na dosari mbalimbali yaliyojitokeza katika Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Aidha, alisema jambo hilo litasaidia kuweka uwajibikaji na kupunguza gharama ambazo Serikali imekwishaingia hadi sasa.

Alieleza kuwa kamati inamuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kadri atakavyoona inafaa, kufanya ukaguzi wa ufanisi wa shughuli zinazohusu ununuzi na usimikaji wa mifumo katika Taasisi za Umma.

Alisema kuwa ukaguzi huo utakuwa muhimu ili kutoa mwongozo na ushauri kwa Taasisi za Umma katika manunuzi ya mifumo ili kuepuka gharama zisizo za lazima kwa siku zijazo.

Kuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), alisema kwa kuwa taarifa ya CAG imebainisha kutokuwepo kwa makubaliano ya kimaandishi ya mkopo  wa shilingi 82,736,176,217 kati ya NHIF na Chuo Kikuu Dodoma kuhusiana na ujenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, pamoja na kupungua kwa hali ya mtaji wa Mfuko.

Alisema kutokuwepo kwa makubaliano hayo ni dosari ya kiuhasibu katika Hesabu za Mfuko, na pia kupungua kwa hali ya mtaji kunaathiri uwezo wa kifedha wa Mfuko kutekeleza wajibu wake wa Kisheria.

Kutokana na hali hiyo alisema Bunge linaazimia kwamba Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF na Bodi ya Wakurugenzi ya Hospitali ya Benjamini Mkapa wafuatilie kwa karibu Serikalini suala la makubaliano ya kimaandishi ya mkopo wa ujenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa ili kufunga hoja husika.

Kuhusu mtaji wa mfuko, kamati iliitaka NHIF ihakikishe kunakuwepo mwenendo mzuri wa Mfuko, kwa kuongeza udhibiti na ufuatiliaji wa kiwango cha madai ya huduma ili kuepuka madai hewa ambayo yanaathiri shughuli za Mfuko.

Aidha, NHIF iendelee kufanya tafiti mbalimbali za kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuwekeza asilimia fulani ya michango ya wanachama ili uwekezaji huo uje kusaidia malipo ya huduma za afya kwa wanachama pindi watakapostaafu.

Kuhusu Utendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), alisema kwakuwa taarifa ya Ukaguzi katika Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imebainisha dosari kubwa za kiutendaji ikiwa ni pamoja na CAG kutoa “ disclaimer of opinion” katika Hesabu za Shirika.

Alieleza kuwa dosari hizo zimesababisha Serikali kutopata faida stahiki kama gawio na kodi balimbali kutoka kwa STAMICO na Kampuni zake Tanzu.

“Bunge linaazimia kwamba Serikali kupitia Ofisi ya Msajili (TRO) wa Hazina iimarishe usimamizi wa karibu wa STAMICO ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya shughuli za utendaji wa kila siku wa Shirika hilo,”alisema.

Pia, Serikali ifanye mapitio ya Mikataba yote ambayo STAMICO imeingia na Kampuni Tanzu ili kuhakikisha makubaliano katika Mikataba yanatekelezwa ipasavyo na masharti hasi yanaondolewa.

Kaboyoka alisema STAMICO ifanye uthamini wa mali zake ili kutambua thamani halisi ya mali za Kampuni kwa sasa.

Kuhusu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), alisema taarifa ya CAG imebainisha uwepo wa Miradi mingi iliyo chini ya NHC ambayo imeshindwa kukamilika kwa wakati   kutokamilika kwa Miradi hiyo kumeongeza gharama za ujenzi na kuisababishia Serikali hasara kubwa, kutopatikana kwa thamani halisi ya fedha iliyowekezwa na pia kuwepo kwa uwezekano wa NHC kushtakiwa na Wakandarasi.

Alisema bunge linaazimia kwamba Serikali iangalie namna bora ya kuiwezesha NHC kukamilisha Miradi ambayo ilikuwa katika hatua za mwisho za utekelezaji ili kupunguza hasara ambayo tayari imepatikana.

Aidha,  Serikali iendelee na uchunguzi wa kina wa Miradi yote ya NHC ili kubaini dosari zilizopo katika Miradi husika. Baadhi ya Miradi imebainika kuwa ilitekelezwa kwa gharama zisizo halisia na usimamizi wake haukuwa na ufanisi.

kuhusu, kutokamilika kwa wakati kwa Miradi ya Wakala wa Majengo Nchini(TBA) alisema kamati imebainisha hali ya kutokamilika kwa wakati kwa Miradi inayotekelezwa na TBA hapa Nchini.

Alifafanua kuwa kutokamilika kwa Miradi hiyo kunaisababishia Serikali hasara kwa kuongeza gharama za ujenzi na kuwanyima Wateja fursa za kutumia Miradi husika kwa wakati mwafaka.

“Bunge linaazimia kwamba TBA waboreshe na kuimarisha Kitengo cha usimamizi wa utekelezaji wa Miradi ili kuhakikisha miradi yote inaanza na kukamilika kwa kuzingatia muda uliokubalika Kimkataba,”alisema.

Aliitaka TBA wabuni utaratibu wenye ufanisi wa udhibiti wa mifumo ya ndani katika utekelezaji wa Miradi hasa katika eneo la matumizi ya fedha, vifaa vya ujenzi na rasilimali watu ili kuharakisha utekelezaji wa Miradi.

Kuhusu, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Uchambuzi wa Kamati katika Taarifa ya CAG ulibaini kuwa uwekezaji wa NSSF katika hisa za Vodacom haukuzingatia mwongozo wa Uwekezaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii;

Alisema uwekezaji huo unatoa riba ndogo kuliko riba inayotolewa na dhamana za Serikali hivyo kuikosesha NSSF mapato stahiki hivyo Bunge linaazimia kwamba, Serikali ifanye uchunguzi wa kina wa suala hili na kuchukua hatua stahiki kwa kuzingatia matokeo ya uchunguzi.

Kuhusu, usimamizi wa Mikataba ya Ujenzi katika Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia
alisema kamati imebaini mapungufu katika usimamizi wa shughuli za ujenzi na ukarabati wa vyuo vya Ualimu unaotekelezwa katika Fungu – 46 Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Alieleza kuwa mapungufu hayo yamesababisha ongezeko la gharama za ujenzi na hivyo kuisababishia Serikali hasara na pia kutofikiwa kwa malengo ya Wizara hivyo Bunge linaazimia kwamba wizara hiyo iimarishe Kitengo cha usimamizi wa Mikataba ya ujenzi na ukarabati.

Aidha, majengo yote ambayo yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi yakamilike na taarifa zitolewe kwa CAG.

Bunge limeiagiza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia maafa Jenista Mhagama kuhakikisha wanashughulikia suala la mafuriko lililojitokeza katika jimbo la Ruangwa mkoani Lindi kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Maagizo hayo yalitolewa bungeni jana na Spika wa Bunge Job Ndugai wakati wa kipindi cha maswali na majibu yaliyokuwa yakijibiwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kuhusu athari za miundombinu ya barabara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Mara baada ya Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara kujibu swali la Mbunge wa Mtera, Livingston Lusinde(CCM) aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani wa kuifanyia matengenezo na ukarabati miundombinu ya barabara ambayo imeharibikaa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchi nzima huzusani barabara za Mvumi.

Mara baada ya Waziri huyo kumaliza kujibu swali, Spika alisimama  na kueleza kuwa Mvua inanyesha nchi nzima lakini mkoani Lindi kwenye Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa jimboni kwa Waziri Mkuu Majaliwa kuna mafuriko.

”Hivyo tunaomba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu(anayeshughulikia maafa) Mhagama(Jenista) muone hali hiyo,”alisema.

Wakati huohuo, Ofisi ya Rais Tamisemi imewaagiza mameneja wa Wakala wa Barabara Nchini(Tanroad) na mameneja wa Tarula wa mikoa na wilaya kufanya tathmini ya haraka ya uharibifu na adhari za miundombinu ya barabara zilizofababisha na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini ili zifanyiwe utekelezaji wa haraka.

Waitara alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Lusinde aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani wa kuifanyia matengenezo na ukarabati miundombinu ya barabara ambayo imeharibikaa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchi nzima huzusani barabara za Mvumi.

”Barabara ya Mvumi Mission madaraja yote yamevunjika, barabara ya Huzi kwenda Manda katika kituo cha Afya cha Mpyayungu ba barabara zimeoza, wazazi, wagonjwa na wanafunzi wanapata shida kufika katika huduma muhimu, serikali inawaambiaje ili waweze kupata huduma hizo,”alihoji.

Akijibu swali hilo, Waitara alisema tatizo hilo ni la nchi nzima, ndio maana mameneja hao wameagizwa kufanya tathmini na kupeleka bajeti ili changamoto hiyo ipatiwe ufumbuzi.

“Nitumie nafasi hii kuwaelekeza mameneja wa Tanroad na Tarula, kuifanyia kazi changomoto haraka iwezekanavyo,”alisisitiza.

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh