Hija

MHASHAMU  Baba Askofu wa Jimbo la Singida,Edward Mapunda amezindua kituo kipya cha Hija katika Kijiji cha Sukamahela,wilayani Manyoni,Mkoani Singida pamoja na kuadhimisha siku ya amani duniani.

Akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kikatoliki kwenye maadhimisho ya sherehe za uzinduzi wa Kituo cha Hija kilichopo Parokia ya Chibumagwra,Askofu huyo alisisitiza kwamba mwaka huu wa 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa kuwachaugua Rais,wabunge pamoja na madiwani

“Mwaka huu taifa letu litakuwa na uchaguzi,taifa letu litakuwa na uchaguzi,uchaguzi wa kumchagua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Raisi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar,wabunge na madiwani kwa hiyo ndugu zangu nawaalika tuiweke nchi yetu katika sala”alisisitiza Askofu Mapunda

Aidha askofu huyo wa jimbo katoliki la singida aliweka wazi kwamba kutokana na uwepo wa uchaguzi huo ni wakati muafaka sasa kuiweka nchi katika sala na kikubwa zaidi ni kuikabidhi nchi yetu kwa bikira Maria mama wa mungu.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo mkuu wa katoliki ni jukumu la bikira maria kuuweka uchaguzi mkuu ujao kwenye moyo wake mtakatifu,na kwamba iwapo atauweka uchaguzi huo kwenye roho mtakatifu utakwenda vizuri kwa sababu yeye ni malikia wa amani

“Tumuombee Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye niwaambie tu pia ametuchangia ujenzi wetu,naomba tushangilie alileta mchango wake kupitia Mkuu wa Mkoa wetu wakati anaelekea Chato kwenye mapumziko,kwa hiyo tunamshukuru sana Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt,John Pombe Joseph Magufuli kwa sala na michango yake mbali mbali.:”alifafanua

Hata hivyo Askofu Mapunda aliweka bayana kwamba kituo cha hija kilichozinduliwa katika Kijiji cha Sukamahela ni cha pili  baada ya kile cha Kijiji cha Kimbwi kinachotumiwa na waumini wa madhehebu ya dini ya kikristo kwenda kuhija kwa kipindi cha kila mwaka.

Kwa mujibu wa baba askofu huyo baada ya kituo hicho kuzinduliwa kutakuwa kukifanyika sherehe za kuiombea nchi amani na kumshukuru Mungu kila dis,09,ya kila mwaka.

Akitoa maelezo ya awali juu ya wazo la kuanzishwa kwa kituo hicho cha hija,Makamu Askofu wa Jimbo la Singida,Francis Limu alibainisha kuwa  pamoja na wengine wote aliomba kuwataja wawili ambao ndiyo walikuwa waanzilishi wa wazo hilo ambao ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt.Rehema Nchimbi na Mhashamu Edward Mapunda.

‘Waliwaza hapa Sukamahela iliyo katikati ya Tanzania kiwepo kitu fulani cha kiroho,ndiyo wazo la kwanza kiwepo kitu fulani cha kiroho ambacho kinaonesha upekee mahali hapa kijiografia”alisisitiza.

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh