Kimataifa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Nasser Bourita  amelalamikia kitendo cha kutoalikwa nchi yake kushiriki mkutano wa amani ya Libya mjini Berlin, Ujerumani na kusema kuwa vigezo vinavyotumiwa kuchagua nchi kushiriki katika mkutano huo vinaibua maswali mengi.

Bourita alisema katika mazungumzo na televisheni ya al Jazeera kuwa Morocco ikiwa nchi jirani na Libya imeshangazwa na kutoalikwa kwenye mkutano huo.

Waziri Mkuu huyo wa Morocco aliongeza kuwa moja ya matatizo ya mkutano wa Berlin ni washiriki wa mkutano huo.

Tunisia pia ilikataa mwaliko huo ikilalamimika kwamba imepewa mwaliko huo kwa kuchelewa kwa ajili ya kushiriki katika mkutano huo wa Berlin.

Kutoalikwa Morocco na kutoshiriki Tunisia ambazo ni nchi jirani na Libya katika eneo la kaskazini mwa Libya katika mkutano wa Berlin na wakati huo huo kualikwa nchi kama Imarati na Uingereza, kunatilia shaka vigezo vilivyotumiwa kuchagua nchi za washiriki katika mkutano huo.

Pande zinazopigana nchini Libya Januari 13 mwaka huu zilikutana Moscow nchini Urusi kwa ajili ya kusaini mapatano rasmi ya usitishaji vita.

Hata hivyo Jenerali Khalifa Haftar kamanda wa wanamgambo wanaojiita jeshi la kitaifa la Libya, mwishoni mwa mazungumzo hayo alikataa kusaini mapatano hayo.

Mkutano huo wa Berlin ulimalizika juzi kwa pande zote zilizoshiriki kukubaliana juu ya suala la kutouunga mkono au kuusaidia upande wowote kati ya makundi yanayozozana nchini Libya.

Vilevile uliszisitiza udharura wa kudumishwa vikwazo vya silaha dhidi ya Libya.

Balozi-wa-Tanzania-nchini-Ujerumani-Dr.Abbdallah-Possi-akiwa-pamoja-na-Bi.Upendo-Fölsen-Mwenyekiti-Umoja-wa-Tanzania-Ujerumani

Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani (UTU ) Mwalimu Bi.Venessa Upendo Fölsen siku ya jumamosi aliongoza kamati ya uongozi wa umoja huo katika kikao cha kukutana na balozi wa Tanzania nchini ujerumani Mheshimiwa Dkt.Abdallah Possi katika ubalozi wa Tanzania mjini Berlin,ambako ubalozi uliwakaribisha kwa mikono miwili na kufanya mazungumzo nao ambayo Kiongozi wa umoja wa Tanzania Ujerumani amelezea kuwa Umoja huo utaitangaza Tanzania nchini ujerumani kwa nguvu zote kwa maslahi ya Tanzania na watanzania,ususani katika sekta ya

Mwalimu-Bi.Venessa-Upendo-Fölsen-Mwenyekiti-wa-Umoja-wa-Tanzania-Ujerumani

Utalii,uwekezaji,afya na elimu ni mojawapo ya mambo yakatayopewa kipau mbele,Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani ndio mwamvuli pekee unawakusanya watanzania waishio nchini ujerumani na moja ya niya yake ni kuleta mshikamano wenye kuleta maslahi kwa watanzania ujerumani na nyumbani Tanzania.Pia kwa upande wake Mheshimiwa Balozi Dkt. Abdallah Possi amewataka watanzania kuungana pamoja kwa maslahi yao na ya Tanzania,pia kujivunia utanzania wao kwa kuitangaza vema Tanzania katika nyanza zote na vivutio vyake katika tufe la dunia ili kufanikisha Tanzania ya Viwanda itakayokuza uchumi.

*Awataka kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya Tanzania *Atoa wiki mbili wawe wameripoti kwenye vituo vyao vya kazi

RAIS Dkt. John Magufuli amewaagiza mabolizi aliowaapisha kuhakikisha wanakwenda kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya Tanzania.

Mabalozi hao ni Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini na Dkt. Modestus Francis Kipilimba anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Namibia.

Wengine ni Profesa Emmanuel David Mwaluko Mbennah anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe na Dkt. Benson Alfred Bana kuwa Balozi Tanzania nchini Nigeria.

Rais Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya Mbalozi hao kula kiapo hicho ambapo aliwaeleza kuwa wote wanakwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mataifa muhimu ambayo kama yakitumiwa vizuri yatainufaisha Tanzania kiuchumi.

“Niwapongeze wote kwa kuteuliwa kuwa mabalozi, mkafanye majukumu yenu kwa manufaa ya Taifa letu,” alisema Rais Dkt. Magufuli.

Rais Dkt. Magufuli aliwaagiza mabalozi wote wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye nchi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuhakikisha wanatekeleza mikakati iliyopitishwa na jumuiya hiyo.

Alitumia fursa hiyo kuhakikisha ndani ya wiki mbili wanaripoti kwenye vituo vyao vya kazi na kuwataka wakatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi akitoa salaamu katika hafla hiyo, aliwataka mabalozi wanaiwakilisha Tanzania katika nchi za SADC kuhakikisha wanasimamia mambo ambayo Marais wa nchi hizo walikubalana na Rais Dkt. Magufuli alipozitembelea.

Akitoa maagizo kwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi alimtaka kuhakikisha fursa ambayo Tanzania iliipata kuhusu ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili nchini humo anaifuatilia na kujua hatua iliyofikia.

Profesa Kabudi alibainisha kuwa kama sio juhudi za Rais Dkt. Magufuli fursa hiyo Tanzania ilishaikosa.

Hivyo alimtaka akiripoti tu nchini humo jambo la kwanza liwe ni kukutana na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo, kwamba kabla ya mwezi wa pili atoe ripoti ya kinachoendelea juu ya suala hilo.

Kadhalika alimuagiza kufuatilia na kujua suala la ushirikiano baina ya Shule ya Chifu Albert Lithui iliyopo Mazimbu mkoani Morogoro na shule yoyote nchini Afrika Kusini limefikia wapi.

Ikumbukwe kuwa Agosti mwaka jana Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alipotembelea nchini alifika katika shule hiyo na kuahidi kuanzisha ushirikano baina ya shule hiyo na shule yoyote ya nchini kwake kutokana na historia muhimu ya nchi hiyo na mahali hapo.

Profesa Kabudi akizungumzia Balozi wa Tanzania nchini Namibia Dkt. Modestus Francis Kipilimba, alieleza kuwa ubalozi huo ni mpya kuanzishwa nchini humo kufuatia makubaliano baina ya Rais Dkt. John Magufuli na Rais Hage Geingob.

Hivyo alimweleza kuwa anakwenda kuanzisha kituo muhimu, kwamba Serikali imeshamhakikishia nyumba na ofisi atakayokwenda kuanzia kazi ambapo alimuagiza kufuatilia kwenye ushirikiano katika uvuvi wa bahari kuu na masuala ya nyama.

Kwa upande wa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Profesa Emmanuel David Mwaluko Mbennah alikumbushwa kuwa ziara ya Rais Dkt. Magufuli nchini humo ilikuwa na matumaini makubwa kwa wananchi wa nchi hiyo.

Hususan pale ambapo Rais Dkt. Magufuli alipotoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuiondolea vikwazo vya kiuchumi, hivyo alimuagiza kuendeleza mahusiano hayo. Kadhalika alimpa mwezi mmoja kuhakikisha analeta ripoti kuhusiana na fursa zinazopatikana nchini humo.

Profesa Kabudi akitoa maagizo kwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dkt. Benson Alfred Bana, alimuagiza kuhakikisha anainufaisha Tanzania kujifunza kuhusu masuala ya kilimo.

Hivyo alimtaka kutumia fursa hiyo kuimarisha ushirikiano zaidi na nchi ya Ivory Coast ambayo ni mahili katika masuala ya kilimo cha Korosho na Kahawa.

SEOUL‎,KOREA KUSINI
RAIS wa Korea Kusini, Moon Jae-in amesema anasikitishwa na kukosekana kwa maendeleo ya mazungumzo kati ya nchi yake na Korea Kaskazini.
Akizungumza jana, Moon aliapa kwamba ataendelea kujaribu kuzungumza na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un.
Miradi ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili jirani imesimama kutokana na kuongezeka kwa wasiwasi na Korea Kaskazini, ambayo imesitisha mazungumzo ya kuachana na silaha za nyuklia na Marekani.
Aidha, Kim alionya kuwa nchi yake hivi karibuni itazindua silaha mpya za kimkakati hadi hapo Marekani itakaporidhia kuiondolea vikwazo.
Katika hotuba yake ya Mwaka Mpya mjini Seoul, Moon alisema anavunjika moyo na anatamani kuwepo kwa njia za kweli za kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Alitoa wito wa kuwepo mazungumzo mapya kati ya pande hizo mbili na ameapa kuendelea kufanya kazi itakayowezesha kufanyika kwa mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini.

BRUSSELS, UBELGIJI

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg ameitaka Iran kujizuia na ghasia zaidi na uchochezi.

Matamshi hayo aliyatoa katika mkutano wa mabalozi wa NATO mjini Brussels nchini Ubelgiji, uliokuwa unaijadili hali ya Mashariki ya Kati baada ya Marekani kumuua Jenerali wa ngazi ya juu wa Iran, Qassem Soleimani.

Stoltenberg alisema mzozo mpya hautokuwa na maslahi na mtu yeyote, hivyo Iran inapaswa kujizuia na ghasia zaidi.

Alisema ingawa nchi washirika zinaunga mkono operesheni za NATO nchini Iraq, operesheni hizo zitaendelea kusimamishwa kwa muda.

Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zimetoa wito wa kujizuia na vitendo vyovyote vyenye kuleta ghasia katika Mashariki ya Kati, wakati ambapo maafisa wa Iran wanatoa vitisho dhidi ya majeshi ya Marekani na bunge la Iraq kupiga kura kupitisha azimio linalovitaka vikosi vya Marekani viondoke nchini humo.

TEHRAN, IRAN
HARAKATI ya Muqawama ya Hizbullah ya Iraq imemuonya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba iwapo ataiwekea vikwazo nchi hiyo, basi harakati hiyo itazuia usafirishaji mafuta ya kwenda soko la nchi hiyo.
Onyo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Harakati hiyo Ali Askari, na kuongeza kuwa iwapo Rais Trump ataiwekea vikwazo vya kiuchumi serikali ya nchi hiyo, basi harakati hiyo itashirikiana na marafiki zake kuzuia usafirishaji mafuta ghafi ya nchi za Ghuba ya Uajemi kwenda Marekani.
Aidha alizidi kufafanua kuwa ikiwa Wamarekani watakataa kuondoka Iraq, basi kambi zao za jeshi la anga zilizopo ardhi ya nchi hiyo, zitageuzwa mavumbi na kusisitiza kuwa Harakati ya Hizbullah imejiweka tayari kuyasaidia mashirika ya China kuendesha shughuli zao nchini Iraq.
Kufuatia hatua ya kigaidi ya Serikali ya Marekani ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC pamoja na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi ya Hashdu sh-Sha’abi Ijumaa alfajiri katika uwanja wa ndege wa mjini Baghdad, Jumapili iliyopita wawakilishi wa Bunge la nchi hiyo walipitisha mpango wa kuwatimua askari wa Marekani kutoka Iraq.
Baada ya hatua hiyo Rais Trump wa Marekani alitoa radiamali kuhusiana na upitishwaji wa mpango huo wa kuwaondoa askari wa nchi yake kutoka Iraq ambapo alitishia kuiwekea vikwazo vikali serikali ya Baghdad.

WASHINGTON, MAREKANI

MAREKANI imekataa kumpa viza ya usafiri Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Dkt. Mohammad Javad Zarif kwa ajili ya kushiriki mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) unaotazamiwa kufanyika Januari kesho mjini New York.

Vyombo vya habari vya Marekani vimethibitisha habari hiyo ya utawala wa Washington kumnyima kibali hicho muhimu cha kusafiri mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Iran kwenda kushiriki mkutano wa Baraza la Usalama la UN.

Hatua hiyo ya Washington inakiuka ‘Makubaliano ya Makao Mkuu ya 1947’ ambayo yanaishurutisha Marekani kuwaruhusu nchini humo wanadiplomasia wa kigeni wanaokwenda kushiriki mikutano ya Umoja wa Mataifa.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif amesema uhai wa Marekani unaelekea kufikia tamati na mchakato huo umeanzia hapa katika eneo hili la Asia Magharibi.

Dkt. Zarif alisema hayo jana katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa Duru ya 23 ya Mazungumzo ya Tehran na kufafanua kuwa, “Kufikia tamati uwepo wa Marekani kumeanzia hapa eneo la Asia Magharibi, baada ya watawala wa Washington kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani.”

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alieleza bayana kuwa, Marekani kupitia mahesabu yake mabaya na maamuzi hasi ya kistratajia dhidi ya Iran na Asia Magharibi, imeiweka dunia katika hali ya ukosefu wa usalama.

Dkt. Zarif aliongeza kuwa, “Athari ya marais wa Marekani akiwemo Trump, kwa kutanguliza maslahi ya kisiasa ya ndani ya nchi, wamekuwa wakiwasha moto wa migogoro, uharibifu na umwagaji damu katika eneo na kote duniani.”

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh