Living

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga amesema kuwa, Mfuko huo utIfikapo 2025 tunataka zaidi asilimia 75 ya watanzania wawe wamejumuishwa katika mfumo wa bima ya afya.

Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na NHIF kupitia vifurushi vipya.

“Tumeleta mfumo wa vifurushi ili kumuwezesha mtanzania mmoja mmoja kujiunga na Bima ya Afya na kuwa na uhakika wa matibabu wakati wowote, ” alisema Bw. Konga.

“Tunaamini mpaka kufika mwaka 2025 tutakuwa unahudumia idadi kubwa ya wananchi kutokana na kuweka utaratibu rafiki wa kila kundi kuwa na fursa ya kujiunga na huduma za bima ya Afya, ” alisema.

Aidha, Bw. Konga alisema kuwa Mfuko umejipanga kuhakikisha unatoa huduma bora za matibabu kwa wanachama wake kwa kuboresha kitita cha mafao na kuwa na mtandao mpana wa vituo vya kutolea huduma.

Akizundua mpango huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alisema kuwa pamoja na Serikali ya Awamu ya Tano kuboresha Mfumo wa Bima ya Afya pia imeendele kuboresha miundombinu ya maeneo ya kutolea huduma ili mwananchi  anapokuwa na kadi yake ya bima anakuwa na uhakika wa matibabu na yenye kiwango bora.

Alisema kuwa Bima ya Afya ni nyenzo muhimu kwa maisha ya kila watanzania kwa kuwa inampa uhakika na kumuwezesha kufanya kazi kwa kujiamini.

“Watu wanaopinga utaratibu huu wa vifurushi vya bima ya afya hawawatakii mema watanzania, pindi unapopatwa na matatizo hawatakuja kukusaidia, tuwapuuze na tujiunge na mapango huu wa bima ya afya,” alisema.

Aliwaagiza viongozi wa mkoa pamoja na viongozi wa dini kushirikiana kwa pamoja katika kuwahimiza na kuwakumbusha wananchi  umuhimu wa kuwa na bima ya afya.

“Mpango huu wa vifurushi vya bima ya afya unakuwezesha kupata tiba popote pale nchini hivyo ni jambo muhimu sana kwa maendeleo yetu,” alisema.

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh