Mahusiano

Spika mstaafu Anne Makinda. Akizungumza katika kongamano la miaka 25 ya Beijing lililofanyika jijini Dar es salaam, wwengine toka kushoto ni Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu( LHRC) , Anna Henga, Mwanaharakati wa haki z a binadamu Deus Kibamba na Dkt Hellen Kijo Bisimba.
Washiriki wa kongamano hilo wakimsikiliza Anne Makinda
Mkurugenzi wa zamani wa kituo cha Haki za Binadamu na Utawala Bora Dkt. Hellen Kijo Bisimba, akizungumza katika kongamano hilo
Spika Mstaafu Anne Makinda, akisalimiana na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano Mkuu wa wanawake Ulimwenguni uliofanyika Beijing nchini China Getrude Mongella, baada ya kuwasili katika kongamano la miaka 25 ya mkutano huo. Lilifanyika jijini Dar es salaam jana. Picha na Dues Mhagale
Spika mstaafu Anne Makinda. Akizungumza katika kongamano la miaka 25 ya Beijing lililofanyika jijini Dar es salaam, wwengine toka kushoto ni Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu , Anna Henga( LHRC), Mwanaharakati wa haki za binadamu Deus Kibamba na Dkt Hellen Kijo Bisimba na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Wanawake Ulimwenguni uliofasnyika Beijing nchini China Getrude Mongella.
Wazungumzaji katika kongamano hilo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika.
Spika Mstaafu Anne Makinda (kulia), akiagana na Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu( LHRC) Anna Henga baada ya kumalizika kongamano hilo . Katikati ni Mwanaharakati Deus Kibamba
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu( LHRC) Anna Henga (kushoto), akizungumza na viongozi wastaafu Spika Mstaafu Anne Makinda, Dkt, Hellen Kijo Bisimba, na Geterude Mongella, baada ya kumalizika kongamano lililokuwa likizungumzia miaka 25 tangu kufanyika mkutano wa Beijing nchini China. Lililofanyika jijini Dare s salaam jana.

 

Kupeleka hoja binafsi Bungeni kuwa Zitto adui wa Taifa

Mbunge wa Jimbo la Siha kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Godwin Molell anatarajia kupeleka hoja binafsi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwanini Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe asichukuliwe kama Adui wa Taifa hili.

Molell alisema amefikia azma  hiyo dhidi ya Zitto ni kutokana na kitendo  cha Mbunge huyo wa Kigoma  kuandika Barua Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Human Rights Watch  Zama Neff ya kutaka Tanzania isipewe mkopo kwa madai kuwa pesa hiyo itatumiwa kisiasa na Serikali ya CCM.

Wakati Molell akiongea hayo,Mwanaharakati huru nchini Cyprian Musiba amesema, anatarajia kuandika barua Benki ya Dunia, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, utakaoelezea mambo mazuri yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John  Magufuli, na kuwataka  wapuuze maneno ya uongo yanayoenezwa watu wasiokuwa wema na nchgi yao.

Mbunge huyo wa Siha alisema, kupitia barua hiyo Zitto amezuia Shule za Bweni zaidi ya 1000 za kisasa ambazo ndio zilikuwa zijengwe kutokana na mkopo huo, ambazo zingeweza kusaidia watoto wa kike ambao wamekuwa na changamoto ya kupata mimba za utotoni.

‘’Hivi huyo Zitto ana akili kweli, yaani mtu anaandika barua Benki ya Dunia kupinga Tanzania isipewe mkopo kwa ajili ya ujenzi wa Shule za kike kwaajili ya ,maslahi yake binafsi, hakika huyu ni muhujumu uchumi’’, alisema Molell.

Mbunge huyo alisema sababu kubwa ya watoto wa kike kupata mimba za utotoni kunachangiwa na umaskini na umbali wa kutoka Shule hadi nyumbani, lakini Serikali ya Magufuli kwa upendo ikaomba mkopo kwa ajili ya kujenga mabweni ya watoto wa kike ili waweze kuepuka changamoto hiyo inayowakabili.

‘’Baada ya  Zitto na huyo mshirika wake kuandika barua ya kuzuia mkopo huo, eti mzungu mmoja  kutoka huko Benki ya Dunia ameleta barua Bungeni, ikihoji eti kwanini Tanzania ipewe pesa?, wakati hizo shule 1000 zitakazojengwa zitaokoa watoto wa kike 200,000 watakao lala katika mabweni hayo’’, alisema Mbunge huyo.

Molell ambaye pia ni mwanaharakati alisema, kwa mujibu wa barua hiyo Zitto anajifanya kama anatetea watoto wa kike,lakini ukweli anawahujumu na hana nia njema na watoto wa kike katika maendeleo yao.

‘’Kuna usemi usemao ukimuelimisha mtoto wa kike, umeelimisha jamii nzima, sasa Rais wetu kwa kulijua hilo alitaka pesa ya mkopo huo, ajenge Shule za Bweni 1000, ambazo zingesaidia watoto hao, lakini Zitto yuko kinyume na harakati njema za Mh. Rais, nafikiri huyu siyo mwenzetu’’, alisema Molell.

Aidha Mbunge huyo wa Siha alisema, anatarajia kuwasiliana na Spika wa Bunge Job Ndung’ai na wabunge wote wanaitakia mema nchi yao kuwapiga vita wanaohujumu Taifa hili kwa kuangalia maslahi yao binafsi.

‘’Kwa mfano huyu Zitto kama Mbunge aliapa kuilinda nchi na kulinda sheria na katiba ya nchi, sasa iweje huyo huyo alisema atailinda nchi, anaenda kubomoa nchi huko Ulaya?, alihoji Molell na kutaka Spika pamoja na wabunge wamchukulie Zitto ka Muhujumu Uchumi’’, alisema Mbunge huyo.

Wakati huo huo  Molell ameshangaa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na genge lake, wanatambea nchi za Ulaya wakiwa na maelezo ya vivutio vya Tanzania yakiwemo Madini, na kuwahadaa mabepari hao kuwa wakiwapa pesa na kufanikiwa kuingai Ikulu, eti wasaidia kuwapati Madini yaliyopo nchini.

‘’ Yaani Mbowe na genge lake ni wezi, amekiibia Chama chake, pesa za Ruzuku karibu Billioni 15, hazieleweki zimefanya kazi gani, kwani hawa wapinzani wapo kwaajili ya kupiga tu’’, alisema Molell.

Mbunge huyo aliziatak Asasi za kiraia kama wao wanatetea haki za binadamu, kwanini haziendi kuulizia wizi unaofaanywa na Mbowe CHADEMA na badala yake wanaisumbua Serikali ya Magufuli inayofanya mambo mazuri.

Mwanaharakati huyo alisema kuwa, katika barua hiyo atakayoandika  mazuri ya Serikali ya  Magufuli, kivuli cha barua hiyo itapelekwa kwa Watanzania waishio nje ya nchi maarufu kwa jina la Diaspora na nyingine atapeleka kwa Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Paramagamba Kabudi.

Aidha kufuatia mambo yanayofanywa na Mbunge huyo wa Kigoma, Musiba alisema wao kama wanaharakati  hawawezi kukubali kuona Serikali na Rais Magufuli inachafuliwa wakati wao wapo.

‘’Yaani Zitto anaandika barua kwa Mataifa ya nje kwa kutumia Nembo ya Bunge, kuichafua nchi na Rais wake, sasa naomba Serikali isijibu hiyo barua, na badala yake watuachie sisi wanaharakati tupo kuitetea nchi yetu, hii ndio kazi yetu’, alisema Musiba.

 

Aidha Mwanaharakati huyo alaisema kufuatia barua hiyo ya akina Zitto kupinga ujenzi wa mabweni hayo, inaashiria kuwa Mbunge huyo wa Kigoma anachochea mimba za utotoni kwa watoto wa kike na hana nia nzuri.

‘’Hivi huyu Zitto hana watoto kweli? yeye kama mzazi anawezaje kuandika barua ya kupinga isiletwe pesa hapa nchini kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya watoto wa Kike, hiyo inaoonesha anachochea uzinzi kwa watoto wetu’, alisema Musiba.

 

 

Aidha Musiba ameitaka Benki ya Dunia impuuze Zitto na genge lake, kwani benki hiyo na Tanzania wamekuwa na uhusiano mzuri tangu enzi za Mwalimu Nyerere na Taifa hili halina uhusiano mbaya na Matifa ya nje.

Vilevile Musiba alisema, Zitto ameungana na Tundu Lisu, na Nassoro Mazrui wanafanya ziara Mataifa ya Ulaya, kuomba pesa kwa ajili ya kuharibu Uchaguzi  Mkuu ujao kwa kuunda makundi ya vijana kuleta vurugu katika Uchaguzi Mkuu wa Urais, Wabunge na Madiwani mwishoni mwa mwaka huu.

‘’Wanachokifanya Zitto na genge lake wanaichonganisha Serikali na Mataifa rafiki, ili yasiwe na ushirikiano mzuri na Tanzania, hivyo Serikali isiwaonee huruma watu hawa’’, alisema Mwanaharakati huyo.

Aidha Musiba  alisema kuwa, Maalim Seif  akiwa mshauri Mkuu wa genge hilo, wamelenga kufanya vurugu hizo Zanzibar, ili ipatikane Serikali ya Kitaifa ambayo wanalenga kuwemo katika uongozi wa Serikali hiyo,

‘’Zitto na genge lake wanataka kuunda vikundi vya vijana Visiwani Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu, na itokee vurugu kama iliyotokea miaka ya 90 ikapatikana Serikali ya Kitaifa, Maalim akiwemo.

Mwanaharakati huyo ameeleza kuwa, Zitto anajua hawezi kurudi Bungeni hivyo anataka kutumia njia hiyo ili yeye na wenziwe waweze kupata madaraka ya Kitaifa huko Zanzibar, hivyo amewataka Watanzania kuwa makini na makundi hayo yatakayokuwa yakiratibiwa na Chama cha Siasa cha ACT Wazalendo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Nasser Bourita  amelalamikia kitendo cha kutoalikwa nchi yake kushiriki mkutano wa amani ya Libya mjini Berlin, Ujerumani na kusema kuwa vigezo vinavyotumiwa kuchagua nchi kushiriki katika mkutano huo vinaibua maswali mengi.

Bourita alisema katika mazungumzo na televisheni ya al Jazeera kuwa Morocco ikiwa nchi jirani na Libya imeshangazwa na kutoalikwa kwenye mkutano huo.

Waziri Mkuu huyo wa Morocco aliongeza kuwa moja ya matatizo ya mkutano wa Berlin ni washiriki wa mkutano huo.

Tunisia pia ilikataa mwaliko huo ikilalamimika kwamba imepewa mwaliko huo kwa kuchelewa kwa ajili ya kushiriki katika mkutano huo wa Berlin.

Kutoalikwa Morocco na kutoshiriki Tunisia ambazo ni nchi jirani na Libya katika eneo la kaskazini mwa Libya katika mkutano wa Berlin na wakati huo huo kualikwa nchi kama Imarati na Uingereza, kunatilia shaka vigezo vilivyotumiwa kuchagua nchi za washiriki katika mkutano huo.

Pande zinazopigana nchini Libya Januari 13 mwaka huu zilikutana Moscow nchini Urusi kwa ajili ya kusaini mapatano rasmi ya usitishaji vita.

Hata hivyo Jenerali Khalifa Haftar kamanda wa wanamgambo wanaojiita jeshi la kitaifa la Libya, mwishoni mwa mazungumzo hayo alikataa kusaini mapatano hayo.

Mkutano huo wa Berlin ulimalizika juzi kwa pande zote zilizoshiriki kukubaliana juu ya suala la kutouunga mkono au kuusaidia upande wowote kati ya makundi yanayozozana nchini Libya.

Vilevile uliszisitiza udharura wa kudumishwa vikwazo vya silaha dhidi ya Libya.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula ameijia juu halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma kwa kushindwa kuihudumia idara ya ardhi na kusababisha watumishi wa idara hiyo kugharamia baadhi ya vifaa ili kutekeleza majukumu yao.

Hali hiyo ilibainika jana wakati Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika Mkoa wa kigoma.

Akiwa katika Masijala ya Ardhi ya halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Dkt. Mabula alibaini utunzaji majalada ya ardhi usiofuata taratibu huku baadhi ya hati zikiwa hazijakamilishwa kwa ajili ya kuwapatia wamiliki wa ardhi katika halmashauri hiyo tangu mwaka 2018.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwajia juu watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo kwa kushindwa kutekeleza majukumu ipasavyo jambo alilolieleza kuwa linachangia uwepo migogoro ya ardhi sambamba na kuwanyima wananchi fursa ya kupata hati.

Dkt. Mabula aliagiza hati zote ambazo taratibu zake zishakamilishwa ikiwemo wamiliki wake kusaini hati hizo kupelekwa Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Magharibi ndani ya wiki moja  kwa ajili ya kukamilishwa na kupatiwa waombaji.

Hata hivyo, baada ya kuwajia juu watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya Uvinza ndipo Afisa Ardhi wa halmashauri hiyo Manyama Makongo alipomueleza kuwa idara hiyo inashindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na kukosa vifaa jambo lililosababisha kuamua kuchukua  ‘Printer’ yake binafsi na kuipeleka kwenye ofisi hiyo kwa ajili ya kusaidia kazi za idara.

Hali hiyo siyo tu ilimshutua na kumshangaza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi bali ilimsononesha kwa kuona watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo wanatumia fedha zao za mifukoni kuendesha ofisi jambo alilolieleza kuwa halikubaliki.

‘’Hapa jitihada za ziada zinahitajika, halmashauri ipo inashindwa kuihudumia idara ya ardhi, halafu watumishi wanatumia fedha zao za mfukoni hili halikubaliki lazima niwasiliane na Waziri Jafo kuhusiana na suala hili’’ alisema Dkt Mabula.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri Mabula, idara za ardhi katika halmashauri nyingi nchini zimekuwa kama watoto wa kambo kutokana na wakurugenzi wa halmashauri kutozitengea bajeti ya kutosha jambo linalofanya idara kufanya kazi katika mazingira magumu.

Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Lilian Matinga na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Enelia Lutungulu wamewaokoa Maafisa Ardhi wa halmashauri hiyo wasitumbuliwe kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwemo kutokamilisha utoaji wa hati za ardhi kwa muda mrefu.

Walionusurika ni Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Spear Mwalukasa ambaye ilielezwa yuko katika mafunzo  na  Afisa Ardhi Ezekiel Bichuro. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema kutokana na Maafisa hao kuzembea kukamilisha hati kwa muda mrefu basi hawafai kuendelea na nafasi zao kwa kuwa wanakwamisha utoaji hati ambao sasa unaweza kufanyika ndani ya mwezi mmoja pale taratibu zote zinapokuwa zimekamilika.

Hata hivyo, Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matinga na Kaimu Mkurugenzi Enelia Lutungulu waliwatetea kwa kueleza kuwa maafisa hao hawana muda mrefu katika idara hiyo na makosa yanaweza kuwa yalifanywa maafisa waliopita.

Naibu Waziri Mabula alielekeza maafisa hao kupewa barua za onyo kwa kuwa muda wa miezi mitatu waliopo katika idara hiyo wangeweza kuonesha jitihada za kukamilisha hati na kuagiza hati zilizopo zikamilishwe katika kipindi cha mwezi mmoja.

‘’Ikifika tarehe 30 Januari 2020 hati ziwe zimeenda kwa wenyewe, haiwezekani mtu amesaini tangu 2015 halafu mpaka sasa hajapatiwa hati yake, wapo wazembe wachache  wanaochafua Wizara lazima wapewe warning. Alisema Naibu Waziri Mabula.

Naibu Waziri Mabula pia alitembelea wilaya ya Tanganyika ambapo alionesha kutoridhika na kasi ya ukusanyaji mapato yatokanayo na kodi ya pango la ardhi na kuagiza halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kuongeza kasi katika makusanyo sambamba na kupanga, kupima na kumilikisha viwanja kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Afisa Ardhi wa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Penina Simon kiasi cha shilingi milioni 18,069,179.40 kilikusanywa hadi kufikia nusu ya mwaka wa fedha 2019/2020.

CAPTION

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akimsikiliza Afisa Ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Uvinza mkoa wa Kigoma Manyama Makongo kuhusiana na changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi katika halmashauri hiyo jana wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Kigoma.

Balozi-wa-Tanzania-nchini-Ujerumani-Dr.Abbdallah-Possi-akiwa-pamoja-na-Bi.Upendo-Fölsen-Mwenyekiti-Umoja-wa-Tanzania-Ujerumani

Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani (UTU ) Mwalimu Bi.Venessa Upendo Fölsen siku ya jumamosi aliongoza kamati ya uongozi wa umoja huo katika kikao cha kukutana na balozi wa Tanzania nchini ujerumani Mheshimiwa Dkt.Abdallah Possi katika ubalozi wa Tanzania mjini Berlin,ambako ubalozi uliwakaribisha kwa mikono miwili na kufanya mazungumzo nao ambayo Kiongozi wa umoja wa Tanzania Ujerumani amelezea kuwa Umoja huo utaitangaza Tanzania nchini ujerumani kwa nguvu zote kwa maslahi ya Tanzania na watanzania,ususani katika sekta ya

Mwalimu-Bi.Venessa-Upendo-Fölsen-Mwenyekiti-wa-Umoja-wa-Tanzania-Ujerumani

Utalii,uwekezaji,afya na elimu ni mojawapo ya mambo yakatayopewa kipau mbele,Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani ndio mwamvuli pekee unawakusanya watanzania waishio nchini ujerumani na moja ya niya yake ni kuleta mshikamano wenye kuleta maslahi kwa watanzania ujerumani na nyumbani Tanzania.Pia kwa upande wake Mheshimiwa Balozi Dkt. Abdallah Possi amewataka watanzania kuungana pamoja kwa maslahi yao na ya Tanzania,pia kujivunia utanzania wao kwa kuitangaza vema Tanzania katika nyanza zote na vivutio vyake katika tufe la dunia ili kufanikisha Tanzania ya Viwanda itakayokuza uchumi.

NA ELEUTERI MANGI, ARUSHA
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema
Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) ni chombo
muhimu kwa wananchi kuweza kupata taarifa na
kujua matukio mbalimbali yanayotokea nchini kwa
mustakabali wa taifa ili wananchi waweze kujiletea
maendeleo.
Waziri Dkt. Mwakyebe aliyasema hayo alipokuwa
akihitimisha ziara yake ya Kanda ya Kaskazini

ambapo alitembelea mikoa ya Tanga, Kilimanjaro
na Arusha kwa lengo la kuangalia hali ya usikivu wa
Redio ya Taifa TBC inayowarahisishia wananchi
katika mikoa hiyo kupokea taarifa za maendeleo
ya nchi yao.
“Suala la wananchi kupata taarifa sahihi na kwa
wakati sio la hiyari, ni suala la Kikatiba,
tunatekeleza hitaji la Katiba Ibara ya 18 (d) ‘Kila
mwananchi anahaki ya kupata taarifa ya masuala
mbalimbali yanayomhusu yanayohusu maendeleo ya
taifa na ni wajibu wa Serikali ya awamu ya tano
kufanya hivyo’” alisema Dkt. Mwakyembe.
Aliendelea kusema “Namshukuru sana Rais Dkt.
John Pombe Magufuli kwamba aliliona hili mapema
ameingia tu madarakani wakati usikivu wa TBC
Taifa ambayo ni redio yetu ulikuwa ni 54 tu nchi
nzima, sasa hivi tunaongea ni asilimia 73 na
tunatarajia ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020
usikivu utafikia zaidi ya asilimia 90 nchi nzima”
Dkt. Mwakyembe.

Akiwa mkoani Tanga alitembelea kituo cha
mitambo ya kurushia matangazo kiliyopo Mnyusi
Hale wilayani Korogwe ambapo TBC Taifa
inarusha  matangazo katika masafa ya FM 87.7
Mhz na TBC FM inarusha matangazo katika
masafa ya FM 89.7 Mhz wakati wilayani Lushoto
mitambo ya TBC Taifa  ipo katika eneo la
Kwemashai wilaya ya Lushoto inarusha matangazo
yake katika masafa ya FM 87.9 Mhz na TBC FM
inarusha matangazo katika masafa ya FM 89.9
Mhz.
Katika Mkoa wa Kilimanjaro Waziri Dkt.
Mwakyembe alitembelea kituo cha TBC Taifa cha
Mabungo kilichopo Wilaya ya Moshi kinarusha
matangazo katika masafa ya FM  87.9 Mhz na TBC
FM katika masafa ya FM 90.0Mhz wakati Kituo
cha Tarakea kilichopo wilayani Rombo, TBC Taifa
inarusha matangazo yake katika masafa ya 87.9
Mhz na TBC FM inarusha katika 90.0Mhz.
Aidha, Dkt. Mwakembe katika Mkoa wa Arusha
alitembelea mitambo ya TBC Taifa iliyopo eneo la

Themi katika Jiji la Arusha ambapo matangazo
yake yanapatikana katika masafa ya FM 87.7 Mhz
na TBC FM inayorusha matangazo katika masafa
ya FM 89.9 Mhz na kuhitimisha ziara yake kwa
kutembelea kituo cha TBC cha Namanga kilichopo
katika wilaya ya Longido.
Katika ziara hiyo, Waziri Dkt. Mwakyembe alipata
taarifa katika mikoa hiyo ambapo zipo changamoto
mbalimbali ilipo mitambo ya TBC ikiwa ni pamoja
na ubovu wa barabara ambao unapelekea ugumu wa
kufikika kwa urahisi maeneo hayo.
Maeneo ambayo barabara ni mbovu na zinahitaji
kujengwa kwa kiwango cha lami ama kujengwa kwa
zege ni pamoja na Mnyusi kilichopo Hale wilaya ya
Korogwe na Kwemashai wilaya ya Lushoto mkoani
Tanga; Mabungo kilichopo wilaya ya Moshi mkoani
Kilimanjaro pamoja na kituo cha Namanga
kilichopo katika wilaya ya Longido mkoani Arusha.
Aidha, maeneo hayo pia yanahitaji kuwepo kwa
miundombinu ya umeme wa uhakika ili kuhakikisha

radio inakuwa hewani wakati wote na wananchi
waendelee kupata haki yao ya Kikatiba ya kupata
taarifa sahihi na kwa wakati za shughuli
mbalimbali za Serikali kwa manufaa yao na taifa
kwa ujumla.
Nao kwa upande wao Wakuu wa mikoa hiyo
Martine Shigela (Tanga), Anna Mghwira
(Kilimanjaro) pamoja na Mrisho Gambo (Arusha)
walimhakikishia Waziri Dkt. Mwakyembe suala la
miundombinu ya barabara pamoja na umeme katika
maeneo ilipo mitambo ya TBC, kwao ni kipaumbele
ili redio ya Taifa iweze kusikika katika maeneo yao
na wananchi wapate taarifa zitakazowasaidia
katika shughuli za kila siku ikiwemo kilimo, ufugaji,
uvuvi pamoja na taarifa za utalii ikizingatiwa
Kanda ya Kaskazini uchumi wake unachangiwa na
sekta ya utalii .
Kwa mujibu wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.
Hamis Kigwangalla katika Hotuba yake ya Bajeti
Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
alisema kuwa idadi ya watalii walioingia nchini

imeongezeka kutoka 1,327,143 mwaka 2017 hadi
kufikia watalii 1,505,702 mwaka 2018.
Ongezeko hilo limechangia kuongezeka kwa
mapato yatokanayo na utalii kutoka Dola za
Marekani bilioni 2.2 mwaka 2017 hadi kufika Dola
za Marekani bilioni 2.4 mwaka 2018.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ufundi wa
Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mhandisi
Upendo Mbelle aliyeambatana na Waziri Dkt.
Mwakyembe kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa
shirika hilo Dkt. Ayub Rioba alisema kuwa ziara
hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwa shirika
hilo na kuahidi vitu vyote vilivyo ndani ya uwezo wa
TBC wamevichukua na watavifanyia kazi.
Mhandisi Upendo aliongeza kwa vitu ambavyo vipo
kisera alimuoba Waziri, Serikali ivipatie ufumbuzi
hatua itakayosaidia shsirika kufikia malengo yake
ikiwemo miundombinu ya umeme na barabara ili
kuhakikisha usambazaji wa matangazo ya Redio ya
Taifa yanawafikia wananchi wote katika maeneo

yao ili kuwa na tija kwa shirika na taifa kwa ujumla
wakiamini kwao mradi namba moja ni usikivu wa
redio hiyo kwa wananchi.
TBC ni shirika la utangazaji la umma lililoanzishwa
kwa mujibu wa Sharia ya Mashariki ya Umma ya
mwaka 1992 kutoa huduma ya utangazaji kwa
umma kwa njia ya redio na televisheni na kupewa
mamlaka ya kutangaza vipindi mbalimbali
vinavyoakisi misingi ya maadili ya Kitanzania
kupitia vipindi vya elimu na burudani, kutoa habari
za aina mbalimbali, taarifa na uchambuzi kwa
mtazamo wa Kitanzania na kuendeleza maslahi ya
taifa na ya umma.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga amesema kuwa, Mfuko huo utIfikapo 2025 tunataka zaidi asilimia 75 ya watanzania wawe wamejumuishwa katika mfumo wa bima ya afya.

Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na NHIF kupitia vifurushi vipya.

“Tumeleta mfumo wa vifurushi ili kumuwezesha mtanzania mmoja mmoja kujiunga na Bima ya Afya na kuwa na uhakika wa matibabu wakati wowote, ” alisema Bw. Konga.

“Tunaamini mpaka kufika mwaka 2025 tutakuwa unahudumia idadi kubwa ya wananchi kutokana na kuweka utaratibu rafiki wa kila kundi kuwa na fursa ya kujiunga na huduma za bima ya Afya, ” alisema.

Aidha, Bw. Konga alisema kuwa Mfuko umejipanga kuhakikisha unatoa huduma bora za matibabu kwa wanachama wake kwa kuboresha kitita cha mafao na kuwa na mtandao mpana wa vituo vya kutolea huduma.

Akizundua mpango huo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alisema kuwa pamoja na Serikali ya Awamu ya Tano kuboresha Mfumo wa Bima ya Afya pia imeendele kuboresha miundombinu ya maeneo ya kutolea huduma ili mwananchi  anapokuwa na kadi yake ya bima anakuwa na uhakika wa matibabu na yenye kiwango bora.

Alisema kuwa Bima ya Afya ni nyenzo muhimu kwa maisha ya kila watanzania kwa kuwa inampa uhakika na kumuwezesha kufanya kazi kwa kujiamini.

“Watu wanaopinga utaratibu huu wa vifurushi vya bima ya afya hawawatakii mema watanzania, pindi unapopatwa na matatizo hawatakuja kukusaidia, tuwapuuze na tujiunge na mapango huu wa bima ya afya,” alisema.

Aliwaagiza viongozi wa mkoa pamoja na viongozi wa dini kushirikiana kwa pamoja katika kuwahimiza na kuwakumbusha wananchi  umuhimu wa kuwa na bima ya afya.

“Mpango huu wa vifurushi vya bima ya afya unakuwezesha kupata tiba popote pale nchini hivyo ni jambo muhimu sana kwa maendeleo yetu,” alisema.

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh