Michezo

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akipokea nyaraka mbalimbali zinahusu Ofisi ya Katibu Mkuu kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ally Possi (kulia) ikiwa ni sehemu ya makabidhiano ya Ofisi mara baada ya kikao na viongozi wa Menejimenti ya Wizara alipowasili Februari 04, 2020 Jijini Dodoma.

Katika hali ya kawaida mtu anapofanya vizuri hupongezwa kwa kazi nzuri aliyoifanya ndio maana waswahili husema “Chanda chema huvikwa pete”, maana yake mtu anayefanya mema hulipwa mema.

Maneno hayo yanasadifu usemi aliousema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa anawaapisha viongozi mbalimbali February 3, 2020 Ikulu Jijini Dar es Salaam akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi Said.

Rais Dkt. Magufuli alitanabaisha utendaji wa Dkt. Abbasi kwa kusema ni mchapakazi anayefanya kazi nzuri ya kuisemea vizuri Serikali bila kuchoka kwa kufuata miongozo mizuri ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na viongozi wengine kwenye Wizara hiyo.

“Ningependa aendelee kuwa Msemaji wa Serikali, lakini mahali mtu anapotakiwa kupata promosheni usimnyime kwa sababu ni “Motivating Agent” ndio maana tumemteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, na kwa sasa hivi ataendelea kuwa Msemaji wa Serikali mpaka tutakapopata mwingine, na sasa atakuwa anasema akiwa mkubwa zaidi” alisema Rais Magufuli.

Mara baada ya Kuapishwa Dkt. Hassan Abbasi amesema kipaumbele chake ni kufanya mageuzi katika Wizara hiyo kwa kuwa anazifahamu vizuri sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Februari 03, 2020 Ikulu Jijini Dar es salaam.

“Nimeaminiwa tena na Mhe. Rais namshukuru sana ninamuahidi yeye binafsi, Watanzania wote, wadau wa hizi sekta pamoja na wafanyakazi wenzangu pale Wizarani, kwamba tunaenda kuendeleza mageuzi, sio kuanzisha, kwa sababu watangulizi wangu niwashukuru wameanza kazi kubwa, mimi kazi yangu pale itakuwa ni mageuzi katika Wizara ya Habari watu wasubiri mageuzi makubwa.” alisema Dkt. Abassi.

Mara baada ya kwasili wizarani hapo, Dkt. Abbasi alianza kazi kwa kukabidhiwa ofisi na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Ally Possi ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Suzan Mlawi kustaafu.

“Nimekuta watumishi wazuri sana Wizara hii, nimepata ushirikiano mzuri katika utendajikazi wangu, ni timu nzuri lazima tuiboreshe. Hakika kazi yako ya kuisemea Serikali umeifanya kwa weledi na mapinduzi makubwa sana katika Idara ya Habari ambayo unaendelea kuwa Msemaji wa Serikali, umeipeleka Idara pazuri sana” alisema Dkt. Possi.

Februari 7, 2020 Dkt Abassi alikutana na watumishi wote wa Wizara hiyo waliopo Jijini Dodoma na kubainisha mtarajio yake kwa watumishi hao na kuwahamasisha waendelee kuchapakazi kwa weledi kwa kuzingatia taaluma zao badala ya kuendekeza uvivu, utoro, uchelewaji, majungu, uzandiki na ubazazi.

“Natarajia mtakuwa waadilifu na wazalendo, muipende wizara yenu na nchi yenu na msiruhusu hujuma ya aina yeyote” Alisema.

Katibu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akisalimiana kwa furaha na wafanyakazi wa wizara alipowasili (Februari 04, 2020) katika Ofisi ya Wizara hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma,mara baada ya kuapishwa kwake Februari 03, 2020 na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli.

Natarajia mtakuwa wabunifu katika kazi zenu, mtindo wa kufanyakazi kwa mazoea bila ubunifu hauna nafasi ni vema mtumie taaluma zenu ipasavyo ziwe na tija kwa wadau wetu na nchi yetu” alisisitiza Dkt. Abassi

Katika kuyafikia malengo ya Wizara na ya Serikali, Katibu Mkuu huyo aliainisha siri sita za kusukuma mbele gurudumu la wizara hiyo kwa kuongozwa falsafa yake ya “Timu Tunatekeleza” inayosimamia kuweka malengo katika kazi na kuyasimamia. Malengo ni dira, bila kuweka malengo huwezi kujua hata unataka kwenda wapi wala utafika lini na kwa njia ipi.

Siri nyingine ni kuweka malengo makubwa, kutekeleza malengo hayo na sio maneno matupu, kuwa na mawasiliano madhubuti ndani na nje ya wizara ili kuyafikia malengo hayo, kuwa na ushirikiano baina ya menejimenti, watumishi na wadau wa taasisi pamoja na kuamini nguvu ya Mungu katika kufikia malengo tunayojiwekea kwa kuwa yapo mambo ambayo yanazidi uwezo wa mwanadamu na hapo nafasi ya Muumba ni ya muhimu.

Awali akimkaribisha Katibu Mkuu Dkt. Abbasi kuongea na watumishi hao Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Macelline Patrick alisema lengo la kikao hicho ni kutambulishana pamoja na kutoa ahadi ya uadilifu kwa viongozi na watumishi kwa Kiongozi na Mtendaji Mkuu wa Wizara.

Pia aliongeza kuwa Wizara hiyo ina idadi ya watumishi 224 ambao miongoni mwao wapo Makao Makuu jijini Dodoma na wengine wapo jijini Dar es salaam pamoja na Chuo cha Maendeleo ya Michezo cha Mallya kilichopo mkoani Mwanza.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Abdul Njaidi amesema kuwa wamefurahishwa na uteuzi wa Dkt. Abbasi kushika wadhifa Katibu Mkuu kwa kuwa ataendelea kuwa nao katika tasnia ya Habari.

“Ataifanya TAGCO iende hatua za juu zaidi kwa sababu anaijua, siku zote amekuwa akisimamia taaluma na kutaka watu wafanye kazi kwa matakwa ya taaluma zao ili kufikia malengo ya Serikali ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025” alisema Njaidi.

Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakila kiapo cha Uadilifu katika utumishi wa Umma mele ya Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi baada ya kupata Semina elekezi kutoka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyofanyika Februari 07, 2020 jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kikao kazi cha watumishi wa Wizara hiyo.

Aidha, Baada ya kuteuliwa na Rais Ijumaa Januari 31, 2020, baadhi ya wadau wa sekta ya habari wakiwemo Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini pamoja na Wizara na Taasisi mblimbali walitoa pongezi na maoni yao kupitia jukwaa la “WhatsApp” kuhusiana na uteuzi huo.

Baadhi waliandika pongezi zao kwa Katibu Mkuu Dkt. Abassi ambapo Theodos Komba anasema “Hongera Dkt., Mungu aendelee kukubariki katika utekelezaji wako wa majukumu mapya. Tunafuraha kuwa tunaendelea kuwa pamoja”; Nteghejwa Hosea anasema “Hongera Dkt., Mungu ataendelea kukuongoza hata hapo unapoenda sasa;”

Wengine waliotoa maoni yao ni Mtamike Omary anasema “Hongera Dkt., Mwenyezi Mungu azidi kukujaalia hekima na busara nyingi zaidi wakati wote wa uongozi wako, hakika umekuwa nahodha bora sana kwetu;” Peres Muhagaze anasema “Hongera sana Dkt. Hassan Abbas!! Umeitumikia Serikali na Umma kwa ueledi wa hali ya juu ukiwa Mkuruggenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na  Msemaji Mkuu wa Serikali, umeacha alama, tunakuombea ufanye zaidi katika ofisi yako mpya ya Katibu Mkuu wa Wizara na kuendelea ili  kutimiza adhma yako ya ndani ya kuwatumikia Watanzania katika masuala mbalimbali. Mwenyezi Mungu akutangulie katika maukumu mapya”

Aidha, pongezi hizo kwa Katibu Mkuu Dkt. Abassi pia zimetolewa na Wizara na Taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara yake anayoiongoza, Wizara ya Maji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kampuni ya Magazeti ya serikali Tanzania (TSN) na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Akiwashukuru wadau hao kupitia jukwaa hilo kwa kumpongezi zao, Katibu Mkuu Dkt. Abassi anasema “Team, Kimsingi sina la kusema kwa imani hii kubwa ambayo Mhe. Rais ameendelea kuniamini. Namhuskuru sana sana na zaidi nawashukuru wote kwa salaam.

Ni faraja kwamba bado tuko wote katika sekta ya Habari. Tuanzie hapo tulipoishia. Hii ni Wizara iliyobeba soft power zote za nchi. Nawatakia kasi na utekelezaji mwema wa pale tulipoishia. Nitabaki kuwa mlezi wenu mujarabu. Hakika mmenilea, mmenishauri, mmenisikiliza, mmenivumilia na tumepiga kazi, basi na kazi iendelee. Nyie ni TeamTunatekeleza Tuendelee na kazi Mungu Awabariki.”

Dkt. Abbasi anakuwa Katibu Mkuu wa 26 kuingoza Wizara hiyo akitanguliwa na Makatibu Wakuu 25 tangu nchi yetu kupata Uhuru mwaka 1961 ambapo mnamo mwaka 1964 Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwl. Julius Nyerere aliunda Wizara ya Habari na Utalii ilidumu hadi 1971 ilipoundwa Wizara ya Habari na Utangazaji. Mwaka 1980 Serikali iliunganisha majukumu ya sekta ya Habari na Utamaduni na kuunda Wizara ya Habari na Utamaduni.

Aidha, mwaka 1984 majukumu ya sekta ya Habari na Utamaduni yalihamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais na na mwaka 1995 hadi 2005 majukumu ya Sekta ya Habari yapohamishiwa tena Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Sekta ya Habari, Utamaduni na Michezo ziliunganishwa pamoja na kuunda Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Serikali iliunda Wizara Mpya ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Mwaka 2016 Serikali ya Awamu ya Tano iliunda Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michzo ambayo inafanya kazi hadi sasa.

Makatibu Wakuu waliohudumu katika Wizara hii ni pamoja na Bw. A. K. Tibandebage, Bw. B. J. Mkate, Bw. Bernard Mulokozi, Bibi Zahra Nuru, Dkt. Ben Moses, Bw. Daniel Mloka, Mhandisi Paul Mkanga, Bw. Paul Sozigwa, Bw. Wilfred Mwabulambo, Bw. Silvano Adel, Bw. Elly Mtango, Bibi Rose Lugembe, Bw. Raphael Mollel, Bw. Silvanus Odunga, Bw. Abubakari Rajabu, Bw. Kenya Hassan, Bw.  D. Sepeku, Bw.  Raphael Mhagama, Bibi Kijakazi Mtengwa, Dkt. Florens Turuka, Bw.  Sethi Kamuhanda, Bibi Sihaba Nkinga, Prof. Elisante Ole Gabriel na Bibi Suzan Mlawi.

Dkt Hassan Abbasi Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, ameshika wadhifa wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali tangu Agosti 5, 2016 hadi kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo Januari 31, 2020 na kuapishwa Februari 03, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Alizaliwa wilayani Korogwe, Tanga mwaka 1978 na kupata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Hale kati ya mwaka 1988 na 1994. Alimaliza akiwa mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri mkoani humo na kujiunga na Sekondari ya wanafunzi wenye vipaji maalum ya Tabora Wavulana (Tabora School) mwaka 1995 kwa masomo ya sekondari.

Kati ya mwaka 1997 na 1998 alihamia katika Sekondari ya Azania, Dar es Salaam ambapo alimaliza kidato cha nne na kati ya mwaka 1999-2001 alijiunga na Shule ya Sekondari Lindi kwa masomo ya kidato cha tano na sita.

Kati ya mwaka 2002 na 2006 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alichukua shahada ya kwanza ya sheria (LL.B). Akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu pia aliajiriwa kama mwandashi wa habari wa kujitegemea katika kampuni ya Business Times na baadaye kushika nafasi mbalimbali kuanzia mwandishi mwandamizi, mhariri msaidizi hadi mhariri Mkuu katika magazeti ya Majira na Kulikoni.

Mwaka 2005 akiwa bado mwanafunzi, alichaguliwa kuwa Mhariri Mkuu wa Jarida liitwalo “Nyerere Law Journal” linalochapishwa na Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kati ya mwaka 2007 na 2008 alihudhuria masomo ya uandishi wa habari ndani na nje ya nchi ikiwemo makao makuu ya Reuters, London, Uingereza na Chuo Kikuu cha Maine nchini Marekani.

Mwaka 2010 aliajiriwa Serikalini akiwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) tawi la Tanzania, programu iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Nje, ambapo kabla ya mwaka 2014 alikuwa Meneja Mawasiliano katika Ofisi ya Rais, Kitengo cha Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Aidha, ana taaluma ya Sheria ambapo ana hadhi ya Wakili wa Mahakama Kuu tangu mwaka 2011, Dkt. Abbasi pia ana diploma ya uzamili katika usimamizi wa mahusiano ya kimataifa (PGD-MFR) kutoka Chuo cha Diplomasia cha Msumbiji na Tanzania, Kurasini, shahada ya uzamili katika mawasiliano kwa umma (MA Mass. Comm., SAUT) na shahada ya uzamivu katika mawasiliano kwa umma (Ph.D Mass. Comm., SAUT).

Na Mwandishi wetu

MABINGWA wa kihistoria Yanga jana wamechezea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mtanange uliopigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika dakika ya 13 mshambuliaji wa Kagera Sugar,
Mhilu alifungua akaunti ya mabao dakika ya 13 kwa kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango Farouk Shikalo.

Yanga ikiwa chini ya nahodha wao Haruna Niyonzima kwenye mchezo wa leo ilimshuhudia kiungo wao Mohamed Issa ‘Mo Banka’ akiwapunguzia kasi dakika ya 44 baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa kucheza faulo kwa wachezaji wa Kagera Sugar.

Kipindi cha kwanza Yanga walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0 walijipanga kurejea kupindua meza kipindi cha pili mambo yakazidi kuwa magumu kwani Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime ilimzidi ujanja Luc Eymael ambaye ni mara yake ya kwanza kukaa kwenye benchi la ufundi akipokea kijiti cha Mwinyi Zahera.

Bao la pili kwa Kagera Sugar lilifungwa dakika ya 66 kupitia kwa Ally Ramadhan aliyemalizia pasi ya Abdallah Siseme na msumari wa mwisho ulipachikwa kwa kichwa dakika ya 89 na kuifanya Yanga kushindwa kutumia dakika nne za nyongeza kupata bao la kufutia machozi.

MABINGWA watetezi Simba jana wameibuka na ushindi wa kuichapa Alliance FC mabao 4-1

katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa CCM Kirum- ba mjini Mwanza.

Simba SC inafikisha pointi 41 baada ya

kucheza mechi 16, ikiwa imebakiza mchezo mmo-ja kuwa sawa na wengi ambao wametanguliwa mbele kwa mchezo mmoja.

Katika Dakika ya 27 Patrick Mwenda aliipatia timu yake ya Alliance bao ,hata hivyo katika dakika ya nyongeza 48 Jonas Mkude anasawazi- sha kwa guu lake la kulia akiwa nje ya 18.

Dakika ya 58 Kagere anafunga bao la pili aki- malizia pasi ya Clatous Chama, Dakika ya 63 Clatous Chama anafunga bao la tatu kwa faulo ak- iwa nje ya 18kwa guu la kulia.

Hata hivyo mpira ul- iokuwa na ushindani kwa timu zote mbili huku Al- liance wakijitahidi ku- kaba katika dakika ya 72 Dilunga anafunga bao la nne kwa kumalizia pasi ya Shiboub,katika daki- ka ya 73 Fraga anain- gia akichukua nafasi ya Shiboub,huku pia dakika ya 81 Ajibu ndani Chama anatoka,Dakika ya 84 Bocco anaingia kuchukua nafasi ya Dilunga.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Haruna Shamte, Gardiel Michael, Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Jonas Mkude/Muzamil Yassin dk65, Ibrahim Ajibu/Clatous Chama dk78, Said Hamisi Ndemla, John Bocco, Sharaf Shiboub na Francis Kahata/Deo Kanda dk56.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Mustafa Suleiman, Adeyoum Ahmed, Lamine Moro, Ally Mtoni ‘Sonso’, Abdullaziz Makame, Deus Kaseke, Feisal Salum/ Mapinduzi Balama dk46, David Molinga/ Tariq Seif dk46, Mrisho Ngassa/Papy Kabamba Tshishimbi dk69 na Patrick Sibomana

TIMU YA RIADHA TABORA YAPOKELEWA KWA SHANGWE.

NA BENNY KINGSON,TABORA.

TIMU ya mchezo wa riadha ya Mkoa wa Tabora imepokelewa na uongozi wa Mkoa hapa kwa furaha na shangwe baada ya kufanikiwa kutwaa jumla ya medali 8 na kuibuka mshindi wa tatu kitaifa katika mashindano ya taifa ya mchezo huo yaliyomalizika hivi karibuni jijini Mwanza.

Akiongea kwa niaba ya Afisa Elimu wa Mkoa huu Suzan Nusu baada ya mapokezi hayo, Afisa Michezo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Josephat Ngazime alisema kuwa ushindi huo umeuletea heshima kubwa mkoa huo.

Ngazime alisema uongozi wa mkoa huo unajivunia kuwa na vijana wenye vipaji vya michezo mbalimbali na kuwataka walimu, wazazi na walezi kuwapa fursa zaidi watoto hao ya kushiriki michezo mbalimbali ili kuendeleza vipaji hivyo.

Alimpongeza Katibu wa chama cha riadha Mkoa Salumu Tarradady (kocha) na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa chama hicho Allan Kitwe kwa jitihada zao kubwa zilizowezesha timu hiyo kufanya vizuri sana katika mashindano hayo.

Alibainisha kuwa uongozi wa mkoa huo unathamini sana michezo na utaendelea kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha watoto wenye vipaji wanaendelezwa ikiwemo kuhamishiwa katika shule zinazolea wanamichezo.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha  riadha Salumu Tarradady alitaja watoto waliotwaa medali za dhahabu kuwa ni Rose Seif  (2 kuruka chini), Agness Josephat (1mita. 5000), Catherine Amir (1 kurusha
mkuki) na Jilya Shagembe (1kurusha mkuki).

Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Allan Kitwe alisema timu ya Mkoa wa Kusini Unguja iliibuka kidedea baada ya kupata jumla ya medali 26 ikiwemo 12 za dhahabu ikifuatiwa na Mkoa wa Singida uliopata jumla ya medali 14 zikiwemo 7 za dhahabu huku Tabora ikipata medali 8 za dhahabu.

Waliotwaa medali za shaba ni Catherine Amir katika mchezo wa kuruka,Tausi Simon, Rose Seif, Bora Hassan na Catherine Amir katikamchezo wa kupokezana vijiti huku waliotwaa medali za fedha
wakiwa ni Rose Seif, Catherine Amir, Bora Hassan na Magdalena Thadeo katika mchezo huo pia.

Wachezaji Jilya Shagembe na Rose Seif waliomba uongozi wa mkoa na wadau wa michezo kuwasaidia hasa pale wanapohitaji kuwezeshwa ili kushiriki mashindano mbalimbali ili vipaji vyao viweze kutumika
ipasavyo.

PAMBANO hilo la kukata na shoka ambalo ni la kwanza msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, litachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam Jan 4 saa 11 jioni.

Katika pambano hilo simba ambao ni mabingwa watetezi na vinara wa ligi kuu katika ligi wakiwa wamevuna pointi 34 na wamecheza mechi 13 wamefungwa mechi moja na kutoka sare moja.

Simba inaingia uwanjani kishujaa baada ya kushinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Ndanda na kuibuka na 2-0.

Huku Yanga wakiwa na jumla ya pointi 24 na wamecheza mechi 11 na kufungwa moja na kutoka sare mara mbili katika mzunguko wa ligi msimu huu.

“Kikosi hicho, ambacho kipo chini ya Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck,pamoja na Selemani Matola ambao ni mechi yao ya nne ya ligi kuu tangu kuanza kukinoa kikosi hicho.”

Kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa amejipanga kushinda mchezo dhidi ya Yanga kwa kuwa malengo yake ni kutetea ubingwa wa ligi hiyo.

Hata hivyo Mbelgiji huyo mpaka sasa akiwa na Simba amefanikiwa kuiongoza kwenye mechi nne, tatu za Ligi Kuu Bara ambazo amefanikiwa kuchukua pointi tisa na moja ikiwa ni ya Kombe la FA.

Vandenbroeck alisema kuwa lengo lake ni kuhakikisha anashinda kila mchezo uliopo mbele yake ukiwemo wa Yanga ili kujihakikishia ubingwa.

“Kikosi kipo tayari isipokuwa kwa Miraji na Rashid ambao wana majeruhi lakini waliobaki wapo tayari kwa mchezo wa kesho,kiukweli hakuna jambo rahisi kwetu lazima tupambane ili kufikia malengo kutokana na ubora wa timu yetu, hatuwezi kuangalia nani anakuja mbele zaidi ya kujikita kwenye malengo ya kushinda pointi tatu, Yanga ni wazuri lakini kwetu tunachoangalia ni kuchukua pointi tatu kwao ili kufikia malengo,” alisema Vandenbroeck.”

Kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck

“Kwa upande wa nahodha wa kikosi cha Simba John Bocco alisema kuwa anaamini mashabiki ni wachezaji wa 12 hivyo aliwataka wajitokeze kwa wingi.

“Tunaenda kupambana sababu ya timu, tunaenda kutafuta alama tatu ili tuendelee kusalia kileleni, tunaamini kwa juhudi zetu kama Simba na Mungu akitusaidia tutaibuka na ushindi.” bocco

Kwa upande wa kocha mkuu wa Klabu ya Yanga Sc, Boniface Mkwasa amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa mchezo wa dhidi ya Simba.

Aliongeza kuwa katika mchezo huo Yanga itawakosa wachezaji Tariq Seif ambaye alipata maumivu Katika mchezo dhidi ya Biashara na Lamine Moro ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

KLABU ya soka ya Singida United FC ya Mkoani Singida imetangaza majina ya wachezaji sita,akiwemo mchezaji kutoka Nchini Malawi iliowasajili wakati wa kipindi cha dirisha dogo,wanaoona kuwa wataweza kusaidia kuweza kuikwamua kutoka mwisho kwenye nafasi iliyopo kuwa siyo nzuri.

Akitangaza majina ya wachezaji hao wa kutumainiwa, Katibu wa Timu ya Singida United,Abdurahmani Sima alisisitiza kwamba wameanza michakato ya kupata baadhi ya wachezaji wanaoona kuwa wataweze kuwasaidia kuweza kuikwamua timu hiyo kwenye nafasi ya mkiani.

“Ni kweli tumeanza michakato ya baadhi ya wachezaji ambao tunaona wanaweza kutusaidia kuweza kuikwamua timu yetu kutoka kwenye nafasi iliyopo kwani siyo nzuri”alisisitiza Sima.”

Kwa mujibu wa Sima wachezaji waliosajiliwa kwenye dirisha dogo ni pamoja na Haruna Moshi “Bobani” kutoka Yanga, Athumani Idd Chuji,kutoka Coastal Union,Sixtus Ally Mwasekaga kutoka Alliance,Owen Chaima kutoka Nchini Malawi anayecheza timu ya Mbeya City,Ame Ally kutoka Ndanda Fc na Tumba Swedi kutoka Ruvu Shooting.

“Wachezaji hao wote wameshakamilisha mazungumzo nao na endapo taratibu zingine zitakamilika pia watakuwepo kwenye mchezo wa Jan,mosi,mwaka 2020 kati ya Singida United Fc dhidi ya Azamu FC.”alifafanua msemaji huyo wa Singida United”

Hata hivyo Sima aliweka bayana kwamba hadi kufikia jan,15,mwaka ujao siku ambayo ni mwisho wa kusajili wachezaji kwa kipindi cha dirisha dogo watakamilisha mazungumzo na wachezaji wengine,akiwemo streaker kutoka nchini Ghana na mwingine kutoka Burundi.

Kwa upande wao baadhi ya washabiki,wapenzi na wadau wa michezo wa Mkoa wa Singida,Saad Mhando maarufu kwa jina la Mangala dansi akizungumzia usajili uliofanywa,aliweka bayana kuwa anauunga mkono  kutokana na kwamba wengi wao ni wazoefu katika mchezo wa soka.”

Katika hatua nyingie akizungumzia mchezo kati ya Singida United Fc na Azamu Fc,Katibu wa singida united aliwahakikishia wanasingida kwamba uongozi wa timu hiyo wameona kuna umuhimu wa kuibadili timu hiyo kwa kuyafanyia kazi mapungufu yaliyoiweka nafasi ya mkiani.

“Kwa upande wao baadhi ya washabiki,wapenzi na wadau wa michezo wa Mkoa wa Singida,Saad Mhando maarufu kwa jina la Mangala dansi akizungumzia usajili uliofanywa,aliweka bayana kuwa anauunga mkono  kutokana na kwamba wengi wao ni wazoefu katika mchezo wa soka.”

Azamu Fc,Katibu wa singida united aliwahakikishia wanasingida kwamba uongozi wa timu hiyo wameona kuna umuhimu wa kuibadili timu hiyo kwa kuyafanyia kazi mapungufu yaliyoiweka nafasi ya mkiani.
Mwandishi wetu
Senior Writer

KLABU ya soka ya Singida United FC ya Mkoani Singida imetangaza majina ya wachezaji sita waliojiunga katika klabu hiyo kwa kusajiliwa kipindi cha dirisha dogo.

Akitangaza majina ya wachezaji hao jana Katibu wa Timu ya Singida United,Abdurahmani Sima alisisitiza kwamba wameanza michakato ya kupata baadhi ya wachezaji wanaoona kuwa wataweza kuwasaidia kuweza kuikwamua timu hiyo kwenye nafasi ya mkiani.

“Ni kweli tumeanza michakato ya baadhi ya wachezaji ambao tunaona wanaweza kutusaidia kuweza kuikwamua timu yetu kutoka kwenye nafasi iliyopo kwani siyo nzuri”alisisitiza Sima.

Kwa mujibu wa Sima wachezaji waliosajiliwa kwenye dirisha dogo ni pamoja na Haruna Moshi “Bobani” kutoka Yanga, Athumani Idd Chuji,kutoka Coastal Union,Sixtus Ally Mwasekaga kutoka Alliance,Owen Chaima kutoka Nchini Malawi anayecheza timu ya Mbeya City,Ame Ally kutoka Ndanda Fc na Tumba Swedi kutoka Ruvu Shooting.

“Wachezaji hao wote wameshakamilisha mazungumzo nao na endapo taratibu zingine zitakamilika pia watakuwepo kwenye mchezo wa Jan,mosi,mwaka 2020 kati ya Singida United Fc dhidi ya Azamu FC.”alifafanua msemaji huyo wa Singida United . Hata hivyo Sima aliweka bayana kwamba hadi kufikia jan,15,mwaka ujao siku ambayo ni mwisho wa kusajili wachezaji kwa kipindi cha dirisha dogo watakamilisha mazungumzo na wachezaji wengine,akiwemo streaker kutoka nchini Ghana na mwingine kutoka Burundi.

Singida United yaleta majembe 6 timu yao

Kwa upande wao baadhi ya washabiki,wapenzi na wadau wa michezo wa Mkoa wa Singida,Saad Mhando maarufu kwa jina la Mangala dansi akizungumzia usajili uliofanywa,aliweka bayana kuwa anauunga mkono kutokana na kwamba wengi wao ni wazoefu katika mchezo wa soka.

Katika hatua nyingine akizungumzia mchezo kati ya Singida United Fc na Azamu Fc,Katibu wa singida united aliwahakikishia wanasingida kwamba uongozi wa timu hiyo wameona kuna umuhimu wa kuibadili timu hiyo kwa kuyafanyia kazi mapungufu yaliyoiweka nafasi ya mkianiso.”
Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh