Rais

Kwa miaka mitano Rais Magufuli kapunguza kiwango cha umaskini kutoka asilima 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia

(SOMA ZAIDI)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam. Machi 09, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akikagua makabati maalumu kwa ajili ya kuwekea viatu vya waumini
wakati wa swala alipofanya ziara ya kustukiza kukagua maendeleo ya
Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed
wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akishiriki katika dua na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamizi wa Baraza
Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) alipofanya ziara ya kustukiza
kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa
ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es
salaam leo Ijumaa 28, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary
Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la
Waislamu Tanzania (BAKWATA) akitembezwa kukagua maendeleo ya Ujenzi wa
Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita
wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiongea machache na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry
Bin Ally na viongozi wengine waandamiz wa Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) baada ya kufanya ziara ya kustukiza kukagua
maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa
Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo
Ijumaa 28, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akisindikizwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamiz wa Baraza Kuu
la Waislamu Tanzania (BAKWATA) baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa
Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita
wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akisindikizwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamiz wa Baraza Kuu
la Waislamu Tanzania (BAKWATA) baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa
Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita
wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa 28, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akishiriki katika dua na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamizi wa Baraza
Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) alipofanya ziara ya kustukiza
kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa
ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es
salaam leo Ijumaa 28, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akishiriki katika dua na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh
Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamizi wa Baraza
Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) alipofanya ziara ya kustukiza
kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa
ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es
salaam leo Ijumaa 28, 2020

*Awataka kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya Tanzania *Atoa wiki mbili wawe wameripoti kwenye vituo vyao vya kazi

RAIS Dkt. John Magufuli amewaagiza mabolizi aliowaapisha kuhakikisha wanakwenda kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya Tanzania.

Mabalozi hao ni Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini na Dkt. Modestus Francis Kipilimba anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Namibia.

Wengine ni Profesa Emmanuel David Mwaluko Mbennah anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe na Dkt. Benson Alfred Bana kuwa Balozi Tanzania nchini Nigeria.

Rais Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya Mbalozi hao kula kiapo hicho ambapo aliwaeleza kuwa wote wanakwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mataifa muhimu ambayo kama yakitumiwa vizuri yatainufaisha Tanzania kiuchumi.

“Niwapongeze wote kwa kuteuliwa kuwa mabalozi, mkafanye majukumu yenu kwa manufaa ya Taifa letu,” alisema Rais Dkt. Magufuli.

Rais Dkt. Magufuli aliwaagiza mabalozi wote wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye nchi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuhakikisha wanatekeleza mikakati iliyopitishwa na jumuiya hiyo.

Alitumia fursa hiyo kuhakikisha ndani ya wiki mbili wanaripoti kwenye vituo vyao vya kazi na kuwataka wakatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi akitoa salaamu katika hafla hiyo, aliwataka mabalozi wanaiwakilisha Tanzania katika nchi za SADC kuhakikisha wanasimamia mambo ambayo Marais wa nchi hizo walikubalana na Rais Dkt. Magufuli alipozitembelea.

Akitoa maagizo kwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi alimtaka kuhakikisha fursa ambayo Tanzania iliipata kuhusu ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili nchini humo anaifuatilia na kujua hatua iliyofikia.

Profesa Kabudi alibainisha kuwa kama sio juhudi za Rais Dkt. Magufuli fursa hiyo Tanzania ilishaikosa.

Hivyo alimtaka akiripoti tu nchini humo jambo la kwanza liwe ni kukutana na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo, kwamba kabla ya mwezi wa pili atoe ripoti ya kinachoendelea juu ya suala hilo.

Kadhalika alimuagiza kufuatilia na kujua suala la ushirikiano baina ya Shule ya Chifu Albert Lithui iliyopo Mazimbu mkoani Morogoro na shule yoyote nchini Afrika Kusini limefikia wapi.

Ikumbukwe kuwa Agosti mwaka jana Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alipotembelea nchini alifika katika shule hiyo na kuahidi kuanzisha ushirikano baina ya shule hiyo na shule yoyote ya nchini kwake kutokana na historia muhimu ya nchi hiyo na mahali hapo.

Profesa Kabudi akizungumzia Balozi wa Tanzania nchini Namibia Dkt. Modestus Francis Kipilimba, alieleza kuwa ubalozi huo ni mpya kuanzishwa nchini humo kufuatia makubaliano baina ya Rais Dkt. John Magufuli na Rais Hage Geingob.

Hivyo alimweleza kuwa anakwenda kuanzisha kituo muhimu, kwamba Serikali imeshamhakikishia nyumba na ofisi atakayokwenda kuanzia kazi ambapo alimuagiza kufuatilia kwenye ushirikiano katika uvuvi wa bahari kuu na masuala ya nyama.

Kwa upande wa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Profesa Emmanuel David Mwaluko Mbennah alikumbushwa kuwa ziara ya Rais Dkt. Magufuli nchini humo ilikuwa na matumaini makubwa kwa wananchi wa nchi hiyo.

Hususan pale ambapo Rais Dkt. Magufuli alipotoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuiondolea vikwazo vya kiuchumi, hivyo alimuagiza kuendeleza mahusiano hayo. Kadhalika alimpa mwezi mmoja kuhakikisha analeta ripoti kuhusiana na fursa zinazopatikana nchini humo.

Profesa Kabudi akitoa maagizo kwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dkt. Benson Alfred Bana, alimuagiza kuhakikisha anainufaisha Tanzania kujifunza kuhusu masuala ya kilimo.

Hivyo alimtaka kutumia fursa hiyo kuimarisha ushirikiano zaidi na nchi ya Ivory Coast ambayo ni mahili katika masuala ya kilimo cha Korosho na Kahawa.

Umoja wa wawanawake wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) (UWT) Wilaya ya Ukerewe waahidi kumuunga mkona Mwe- nyekiti wa CCM taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muun- gano Dkt John Pombe Magu- fuli kushinda uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo Spelancia Naga- bona wakati wa hafla ya kupokea baiskeli 59 za we- nyeviti na makatibu wa Ju- muiya hiyo wa Kata 25 za Jimbo la Wilaya ya Ukerewe zilizotolewa na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mwanza Kemilembe Lwota na kukabidhiwa mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la UWT Wilaya.
Mwenyekiti Nagabona ali- waeleza wajumbe wa Baraza hilo kuwa baiskeli hizo zi- takabidhiwa kwa kila Mwe- nyekiti na katibu wa Jumuiya hiyo wa Kata zote 25 ili ku- wasaidia usafiri wa kuwafikia wanachama wa ngazi za matawi na kuhamasisha wa- nanchi ili kuwachagua wag- ombea watakaopitishwa na CCM kugombea Ubunge na Udiwani huku wakihakikisha wanampigia debe Rais Dkt Magufuli achaguliwe tena kuliongoza taifa kwa miaka mitano mingine.
Alieleza kuwa Rais Dkt. Magufuli ametekeleza ahadi ya majisafi na kuboresha vi- tuo vya afya na Hosptali ya Wilaya vinatoa huduma bora kwa wananchi sanjari na kui- malisha usafiri ndani ya ziwa Victoria hudusani kisiwa ki- kubwa cha Ukerewe na Uka- ra pia kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata elimu bure ikiwemo sekond- ari, hivyo nijambo la kujivu- nia kumchagua tena Rais na wawakilishi wa wananchi ambao ni Mbunge na Madi- wani wa CCM bila shaka yoyote.
Nagabona alisema wa- nanchi wa Wilaya ya Uk- erewe walifanya ushabiki na wakakosea kuuchagua upin- zani kwa miaka nane ambapo mambo yalikuwa hayaendi kabla ya Mbunge Joseph Mkundi aliyesoma alama za nyakati na kurejea CCM kwa kuwa alijua jeshi kubwa la wanawake wa Wilaya ya Ukerewe limejipanga kureje- sha Jimbo kutoka upinzani hata hivyo wamejipanga kuhakikisha vitongoji, vijiji, Kata, Jimbo na Rais wote wa- natoka CCM kwa ushindi wa kishindo.
“Nikupongeze Mbunge Lwota kwa kutekeleza ahadi yako yakutusaidia usafiri ili kuhakikisha kazi za Jumuiya zinaimalika na kuwafikia wa- nachama ikiwemo kuongeza wanachama wapya wa Ju- muiya yetu na Chama lakini pia kuisemea miradi mbalim-
bali iliyotekelezwa na serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi na ahadi za viongozi ikiwemo wabunge na madiwani,” alisema.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mwanza, Kemilem- be Lwota akikabidhi baiskeli hizo alisema ametekeleza ahadi ya kutoa usafiri kwa viongozi wa Jumuiya hiyo ngazi ya Kata katika Wilaya zote ambazo Jografia za ku- wafikia wanachama zinaka- biliwa na inachangamoto ya usafiri.
“Niliwaahidi kupitia kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya Mkoa leo nimekabidhi bais- keli 59 kwa ajili ya matumizi ya usafiri lakini pia nimetoa mabati 100, mbao 100 na mi- fuko 50 ya saruji ili kukamil- ishwa kwa mradi wa ujenzi wa jengo la kitegauchumi la Jumuiya Wilaya ya Ukerewe ili kujiingizia fedha zitakazo- saidia kuendeleza Jumuiya pia nimetoa mashuka 200 na vitanda Jumuiya Hospitali ya Wilaya iliyopo Mji wa Nansio sanjali na kuipatia Jumuiya mradi wa pikipiki kuwasaidia kuingiza fedha za uendeshaji shughuli za kila siku,” alise- ma Lwota.
Mbuge Lwota amewa- hakikishia wanachama wa CCM, Jumuiya hiyo na wa- nanchi kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt John Magufuli mzalendo utaen- delea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na
kuhakikisha huduma bora zinapatikana kupitia sekta zote hiyo waendelee kuiunga mkono CCM na serikali ku- fika malengo na taifa liweze kufikia uchumi wa kati na upatikanaji huduma bora za kijamii.
“Wanawake ni jeshi kubwa hivyo tujipange sawa sawa kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ili kuendelea kuongoza taifa na kuhakikisha raslimali za taifa zinawanufaisha watanzania wote na kupatikana maen- deleo yatakayoambatana na huduma bora za kijamii chini ya Rais Dkt Magufuli in- awezekana na mumemuona mzalendo amekuwa akip- ambana kutekeleza miradi mikubwa kwa fedha za kodi yetu,” alisema.
Kwa upande wake Mwe- nyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Ally Mambile alimpongeza Mbunge Lwota kwa kujitolea kusaidia baiskeli ambazo watazitumia kwa usafiri len- go ikiwa ni kutafuta kura za wagombea wa CCM mwezi Oktoba lakini pia zitaweze- sha jeshi kubwa la wanawake kufika maeneo mbalimbali kuwafikia wananchi na ku- waomba wawamchague Rais Dkt Magufuli, Wabunge na Madiwani.
“Niwahase viongozi wa UWT Wilaya na Kata kuzitu- mia baiskeli hizi kuhakikisha malengo yanafikiwa ikiwemo
kuongeza wanachama na ku- pata ushindi wa kimbunga zaidi ya uhuu wa serikali za Mitaa ambapo tumefanya vizuri na kauli mbiu yetu Wilaya ya Ukerewe ni CCM 2020 ni Rais Dkt Magufuli, Mbunge na Madiwani Kata zote 25 mali ya CCM,” alise- ma.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Boniphace Magembe aliwahakikishia viongozi na wanachama wa CCM kuwa serikali imejipanga kuhakiki- sha amani na utulivu wakati wa michakato ya kura za maoni na kampeni za Uch- aguzi mkuu kwa wagom- bea kunadi sera zinafanyika bila vurugu na watakaoleta uchochezi na uvunjifu wa am- ani watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na hawata mfumbia macho mtu ama kikundi cha watu wachache watakaoandaliwa kuvuruga amani maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Uke- rewe, Joseph Mkundi (CCM), aliwashukuru viongozi na wanachama kumpokea al- ipoamua kurejea CCM na kuwa bega kwa bega ku- hakikisha maendeleo yana- patikana ikiwemo kutekele- zwa kwa miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta za majisafi, elimu, barabara, umeme, kilimo cha kisasa, ufugaji wa tija, usafiri kulin- gana na jiografia ya visiwa vyetu hivyo tuhakikishe Rais Dkt Magufuli anapeta kwa

MAMBO 10 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli yanayowavutia wapinzani kiasi cha kuamua kumpongeza hadharini haya hapa.

Katika kipindi kifupi, Rais Dkt. Magufuli amekuwa gumzo ndani na nje ya nchi kutokana na uwezo alionao katika kushawishi watu kufikia maendeleo yaliyotarajiwa kwa kuondoa taratibu zisizofaa kama vile uzembe kazini, ubadhirifu wa mali ya umma na kumaliza kama si kupunguza kero mbalimbali kwa wananchi zilizokuwa zikiwakabili ikiwamo ya upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Kiongozi huyu amefanikiwa kuhakikisha Watanzania wanatoka hatua moja kwenda nyingine kimaendeleo badala ya kubaki kama walivyo miaka nenda miaka rudi.

Aina ya uongozi wa Rais Dkt. Magufuli umeonyesha uwezo au karama ya kuondoa taratibu zilizozoeleka katika jamii na kisha kubuni, kuelekeza njia sahihi kwa vitendo ni ushindi wa mafanikio katika uongozi wake.

Itakumbukwa Novemba, 2015 alipokuwa akizindua na kulihutubia Bunge la Kwanza la 11 Novemba, 2015, Rais Magufuli alisema miongoni mwa kero kubwa alizopokea kutoka kwa wananchi alipokuwa akifanya kampeni ya kuomba kura za Urais, ilikuwa ni ya kukatika katika kwa umeme na yeye aliahidi mbele ya Bunge hilo kuwa ataimaliza kero hiyo katika kipindi cha uongozi wake.

Ahadi hiyo tayari ameshaanza kuitekeleza kwa sababu tayari Watanzania wameshaanza kushuhudia miradi mikubwa ya kuzalisha umeme ikijengwa kwa kasi na mradi mkubwa unaotekelezwa hivi sasa ni ujenzi wa bwawa kubwa la Julius Nyerere la kufua umeme wa maji wa MW 2,115 katika eneo la Mto Rufiji ambalo liko ndani ya Pori la Akiba la Selous, mkoani Pwani.

MIUNDOMBINU

Jambo la pili ni ujenzi wa miundombinu mipya ya barabara ambayo inalisaidia taifa letu kumaliza mkwamo wa kiuchumi katika eneo hili.

Katika kushughulikia jambo hili tumeshuhudia juhudi za Rais Magufuli katika kujenga barabara za juu Fly overs kama daraja la Mfugale, Ubungo na upanuzi wa njia nane wa barabara ya Kimara hadi Kibaha jijini Dar es Salaam.

Miundombinu mingine ni pamoja na ujenzi wa daraja la Selander unaoambatana na njia ya mkato kutoka hosipital ya Ocean Road hadi Kenyata Drive kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.

Ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi kwa shilingi Bilioni 699, ujenzi wa barabara za juu Ubungo – Dar es Salaam kwa shilingi Bilioni 247, ujenzi wa daraja la selander shilingi Bilioni 270, ujenzi wa barabara ya njia 8 kutoka Kimara – Kibaha kwa shilingi Bilioni 140.

Miradi mingine ni ujenzi wa barabara na madaraja shilingi Trilioni 5.37, ujenzi wa meli katika maziwa makuu shilingi Bilioni 172.3, ujenzi wa barabara za lami katika Jiji la Dar es Salaam shilingi Bilioni 660, ujenzi wa majengo ya halmashauri shilingi Trilioni 1.35, ujenzi wa lada 4 katika viwanja vya ndege shilingi Bilioni 67.

SEKTA AFYA

Jambo la tatu ni Afya: Kwa upande wa Sekta ya afya, utekelezaji wa agizo la Rais kujenga vituo vya afya kila kata na baadaye kila kijiji umezinduliwa na tayari unaendelea ambapo Serikali imetumia kiasi cha jumla ya ujenzi wa hospitali na vituo vya afya nchini (shilingi Bilioni 361).

UNUNUZI WA VIFAA TIBA

Jambo la nne ni ununuzi vifaa tiba vya hospitali (shilingi Bilioni 64).Aidha serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka Sh bilioni 31 mwaka 2015 hadi Sh bilioni 270 kwa mwaka 2018.

ELIMU

Jambo la tano ni mikopo kwa elimu ya juu shilingi Trilioni 1.612, kutoa elimu bure shilingi Bilioni 348.67, kukarabati shule na vyuo vikongwe shilingi Bilioni 308.1.

Ongezeko la fedha za serikali kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mujibu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi limeleta ahueni kubwa kwa wazazi pamoja na kuwepo kwa changamoto kwa kada ya ualimu, ambapo bajeti ya fedha za mikopo kwa wanafunzi imeboreshwa zaidi.

MIKOPO ELIMU YA JUU

Jambo la sita ni kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaopata mikopo kwa sasa imeongezeka kutoka wanafunzi 98,000 waliokuwa wanapata mkopo kabla Rais Dkt. Magufuli hajaingia madarakani ambapo walikuwa wanapata mkopo wa Sh bilioni 340 tu, lakini katika mwaka 2016/17 wanafunzi 120,000 walifanikiwa kupata mkopo wa Sh. Bilioni 483, ambapo kwa mwaka 2018/19 jumla ya wanafunzi 40,000 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 7000 wanatarajia kupata mkopo wa Sh. Bilioni 437!

BOMBA LA MAFUTA

Jambo la saba ni ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Ziwa Albert (Hoima) nchini Uganda hadi Tanga ambao ujenzi wake unapitia katika wilaya 24 na jumla ya vijiji 184 katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga.

UJENZI BANDARI

Jambo la nane ni ujenzi wa miundombinu ya bandari. Ujenzi wa bandari kuu kwa shilingi Trilioni 1.2.

VIWANJA VYA NDEGE

La tisa ni ujenzi wa viwanja vya ndege 15 kwa shilingi Trilioni 1.868. Ununuzi wa ndege shilingi Trilioni 1.03.

Juhudi za sasa za Serikali ya awamu ya tano zimezalisha dhamira madhubuti sio ya kulihuisha tu Shirika letu la ndege bali kulipa sura mpya, ufanisi mpya wa kiutendaji na kiuongozi.

UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR)

Jambo la kumi ni ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (SGR) utakaogharimu shilingi Trilioni 7.5.

SGR kwa sasa inajengwa kwa awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza ya ujenzi ni kutoka Dar es Salaam-Morogoro (Km 300), awamu ya pili kutoka Morogoro hadi Makutupora –Dodoma (km 400).

Ujenzi wa reli hii ambayo itakuwa na vituo maalum vya kusimama kupakua na kupakia abiria na mizigo katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Kigoma, Tabora na Mwanza inayojengwa kwa urefu wa km 726 na kutoa ajira 30,000 itakapokamilika ina manufaa makubwa kwani uanzishwaji wa miji katika maeneo haya ya vituo ni jambo lisilokwepeka.

Miji hii midogo inaweza kukua na kuwa miji mikubwa kutokana na uwepo wa vituo hivi vya treni ikizingatiwa kuwa mahitaji ya kiuchumi na kibinadamu yatakuwa ni kipaumbele.

Maduka ya jumla na rejareja yatalazimika kujengwa na wafanyabiashara ili kukidhi matakwa na mahitaji ya kibiashara na kihuduma kwenye maeneo ya karibu na mbali kutoka eneo la kituo.

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh