Siasa

Kwa miaka mitano Rais Magufuli kapunguza kiwango cha umaskini kutoka asilima 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia

(SOMA ZAIDI)

Rais Dkt. John Magufuli amemhamisha Wizara aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na, George Simbachawene, kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuchukua nafasi ya Kangi Lugola, ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Pia Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Mussa Azzan Zungu Mbunge wa Ilala, kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Muungano na Mazingira akichukua nafasi ya Simbachawene aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hayo yalibainishwa jana Ikulu jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Dkt. John Magufuli.
“Siku ya kuapishwa kwa mawaziri walioteuliwa itatangazwa baadaye,” alisema Balozi Kijazi.
Balozi Kijazi alibainisha pia kwmaba Rais Dkt. Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu akiwemo Meja Jenerali Jacob Kingu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kabla ya kuandaka barua ya kujiuzulu hapo juzi.
Wengine ni aliyekuwa Kamishina Jenerali wa Magereza Faustine Kasike na Dkt. John Steven Simbachawene, ambapo Balozi Kijazi alibainisha kuwa vituo vyao vya kazi vitatangazwa baadaye.
Aidha kwa mujibu wa Balozi Kijazi, Rais Dkt. Magufuli ametengua nafasi ya aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto nchini, Thobias Andengenye na nafasi yake itajazwa hapo baadaye.

Rais Dkt. John Magufuli amewatumbua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye kwa kusaini mkataba wa hovyo
Pia Naibi Waziri wa Wizara hiyo Hamad Masauni na Katibu Mkuu Meja Jenerali Jacob Kingu wamemuanikia barua ya kujiuzulu nyazifa zao jambo ambalo Rais alililidhia.
Rais Dkt. Magufuli alichukua hatua hiyo jana wakati akizindua nyumba 12 za makazi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kuchukua uamuzi huo Rais Dkt. Magufuli aliweka wazi sababu za kuchukua hatua hiyo kuwa ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kulikuwa kunatengenezwa mkataba wa hovyo wenye thamani ya Euro milioni 408 sawa na zaidi ya shiling trilioni moja.
Alisema mkataba huo kwa hatua za awali ulikuwa umeshasainiwa baina ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (Memorandum of Understanding (MOU) Andengenye na Kampuni moja ya kutoka Romania kwa ajili ya ununuaji wa vifaa vya jeshi hilo.
Hivyo kutokana na madudu hayo aliwapongeza Naibu Waziri Masauni na Katibu Mkuu Kingu kwa kuandika barua za kujiuzulu huku akisahangazwa na Waziri Lungula pamoja na Kamishna Jenerali Andengenye kuendelea na nyazifa zao.
“Nimpongeze Waziri wa Mambo ya Ndani (Masauni) kujiuzuli kwa kutambua hilo. Hivi karibuni kulikuwa na mkataba mmoja wa ajabu unatengenezwa Wizara ya Mambo ya Ndani wenye thamani ya Euro milioni 408. Mkataba umesainiwa na Kamishna Jenerali wa Zimamoto. Haujapitishwa na Bunge.
“Kangi Lugola pamoja na mwili wake ni Mwanafunzi wangu nimemfundisha Sengerema Secondary, lakini kwa hili hapana, Kamishna Jenerali Thobias Andengenye kwa hili pia Hapana. Kangi Lugola nilitegemea barua yake ya kujiuzulu leo (jana) angetakiwa asiwepo hapa, Watu wamesaini mradi wa hovyo ambao hata Bunge haiujui ni mambo ya hovyo watu walikuwa wanalipwa sitting allowance ya dola 800.” Alisema Rais Dkt. Magufuli.
Aidha Rais Dkt. Magufuli alibainisha kwamba katika madudu hayo walishiriki pia watu kutoka kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
“Kuna Watu wengine kwenye hili wapo ndani ya Mkataba huu wa hovyo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu walisubiria Mwanasheria Mkuu hayupo wakasaini pia wale wasaidizi wa Andengenye nao wapo ndani ya mkataba huu naomba wote washughulikiwe na vyombo husika,” alieleza Rais Dkt. Magufuli.
Kadahalika Rais alisema watu wengine wanaohusika ni Wawizara ya Mambo ya Ndani, ndani ya kitengo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiwemo wasaidizi wa Kamishna Jenerali Andengenye.
Lugola anakuwa ni Waziri wa tatu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kutumbuliwa katika Sarikali hii ya Awamu ya Tano, waliomtangulia ni Charles Kitwanga na Mwigulu Nchemba.
Wakati akichukua uamuzi huo kwa masikitiko na uchungu mkubwa Rais Dkt. Magufuli aliweka wazi kuwa ni moja ya Wizara ambayo tangu aingie madarakani imekuwa ikimtesa sana kutokana na kuongoza katika kuingia mikataba ya hovyo.
Akizungumzia Mradi wa Nyumba za Makazi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, alisema ujenzi wa majengo hayo umegharimu shilingi Bilioni 13 ambapo awali aliagiza Jeshi la Magereza lipewe shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo.
Hivyo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ilipewa zabuni ya ujenzi lakini ilishindwa kumaliza kazi kwa miezi 27 wakiwa wamefikia asilimia 45 tu, ndipo alipoagiza kazi hiyo ikabidhiwe kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambao walipatiwa shilingi Bilioni 3 na kufanikiwa kukamilisha ujenzi huo kwa muda wa miezi 7.
Alilipongeza JWTZ kupitia JKT kwa kazi nzuri waliyoifanya katika ujenzi huo na ujenzi wa miradi mingine ikiwemo ukuta wa eneo la madini ya Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara, kambi ya JWTZ Ngerengere Mkoani Morogoro na ujenzi wa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Hata hivyo alilitaka Jeshi la Magereza kujirekebisha na kujifunza kutoka JKT kwa kuwa linayo nguvu kazi ya wafungwa takribani 13,000 ambao wanaweza kutumika katika uzalishaji mali na kujenga miundombinu ya jeshi hilo yakiwemo makazi ya Maafisa na Askari badala ya kusubiri kujengewa na majeshi mengine ama kutumia wakandarasi.
Rais Dkt. Magufuli alieleza kusikitishwa kwake na kusuasua kwa ujenzi wa jengo la kiwanda cha kutengeneza viatu cha Gereza Kuu Karanga kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro ambacho licha ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF (ambao ni wabia) kutoa shilingi Bilioni 9 tangu Oktoba 2019, hadi sasa Jeshi la Magereza limeshindwa kuharakisha ujenzi huo ambao umefikia asilimia 45 tu, ilihali mitambo inayopaswa kufungwa katika jengo hilo imeshawasili Bandari ya Dar es Salaam.
Alimuagiza Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike kuhakikisha majengo mapya 12 yaliyojengwa katika Gereza la Ukonga yanatunzwa na kuendeleza utaratibu wa kujenga nyumba za Maafisa na Askari wake pamoja na kukarabati zilizopo, kwa kuwa haridhishwi na hali duni ya makazi ya Maafisa na Askari Magereza hapa nchini.
Pia alimtaka CGP Kasike kuhakikisha maji yanaingizwa katika nyumba za makazi ya Maafisa na Askari Magereza katika majengo mapya 12 ya Ukonga, kwa kuwa wakati wa ukaguzi amebaini kuwa makazi hayo hayajaunganishwa na mtandao wa maji ndani ya nyumba.

ambao umejengwa na Jashi la Kujenga Taifa (JKT) chini ya usimamizi wa Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Charles Mbuge, Rais Dkt. Magufuli alisema kuwa amefurahi kuona mradi huo umekamilika.
Hata hivyo alilitaka Jeshi la Magereza kujitathimini kwa nini lishindwe kujenga nyumba zake lenyewe hadi lijengewe na JKT huku wakiwa na nguvukazi ya kutosha wakiwemo wafungwa na mahabusu.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) upande wa Bara, Tundu Lissu ametangaza kuwatelekeza wadhamini wa kesi ya uchochezi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Kinachotafsirika kuwatelekeza wadhamini hao ni kitendo chake cha kusema kwamba anawaonea huruma waliomdhamini katika kesi hiyo ya uchochezi inayomkabili. Hivyo aliiomba mahakama itende haki kwa kuwa wadhamini wake hao hawawezi kumrejesha Tanzania.

Lissu ambaye kwa sasa yupo nchini Ubelgiji anakabiliwa na kesi ya uchochezi katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, juzi Januari 20, 2020 wadhamini wake walitakiwa na mahakama hiyo kuhakikisha anarejea nchini ili kuendelea na kesi yake. Mbunge huyo wa zamani wa Singida Mashariki amesema wadhamini hao, Robert Katula na Ibrahimu Ahmed hawawezi kumrejesha Tanzania kwa kuwa hawakumpeleka. “Mimi nitarejea nitakapohakikishiwa usalama wangu, uhai ni mkubwa kuliko kesi hiyo,”alisema Lissu.

Lissu alieleza hayo juzi ikiwa ni siku moja tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa siku 31 kwa wadhamini wake kuhakikisha wanamfikisha mahakamani hapo. Juzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilisikilizwa kesi ya uchochezi inayomkabili Lissu na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ilielezwa na wadhamini wa Lissu kuwa wamemuandikia barua Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumtaka amrejeshe mshtakiwa huyo nchini. Lissu yupo Ubelgiji tangu Januari 6, 2018 alikokwenda kwa matibabu akitokea Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako nako alifikishwa usiku wa Septemba 7, 2017 baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana akiwa katika makazi yake eneo la Area D, Dodoma.

Hakimu Simba alitaka wadhamini hao kuhakikisha Februari 20 wanampeleka mshitakiwa huyo na si vinginevyo. Kabla ya maagizo hayo Katula alisema juhudi walizofanya kuhakikisha mshtakiwa anafika mahakamani ni pamoja na kumwandikia barua Mbowe

Katika maelezo yake kuhusu wadhamini wake, Lissu alisema, “Ninawahurumia sana wadhamini wangu kwa sababu wamewekwa katika mazingira ambayo ni magumu na mabaya bila sababu ya msingi.” “Mtu anapokuwa mdhamini katika kesi za jinai, anachukua reasonable steps kuhakikisha mtu aliyemdhamini anafika mahakamani wakati anapohitajika kufika mahakamani., “Katika kesi yangu, hakimu anajua na waendesha mashtaka wanajua kuwa niliondoka Tanzania katika mazingira gani, wote wanajua, katika mazingira hayo hata bila kuambiwa au kuombwa alipaswa awaondoe kwa sababu hawana namna yoyote ya kunirudisha.” “Sasa mahakama huyu Hakimu Simba anasema wanipeleke mahakamani, hawawezi kunileta na hawawezi tena na wamesema hivyo,” alisema. Mbali na Lissu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na mchapishaji wa kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh. Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002. Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 12 na 14, 2016 jijini Dar es Salaam ambapo Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’ Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi.

 • Lengo ni kuchochea ushawishi kwa waumini waikatae CCM 2020
 • Pia kupandikiza chuki kati ya madhehebu ya dini na Serikali

  Wapanga kufufua mchakato wakudai madhehebu ya dini na Serikali Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi

  MIKAKATI ya siri ambayo im- evuja kutoka ndani ya Cha- ma Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) inadai kwamba Kamati Kuu ya chama hi- cho hivi karibuni ilikutana katika eneo la siri mkoani Kilimanjaro na kupanga mikakati ya kuanzisha uchochezi wa machafuko nchini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

  Katika kikao hicho ambacho kiliongozwa na Mbowe, wajumbe walikubaliana kuanzisha genge la vijana wa chama hicho am- balo litasambazwa kwenye madhehebu mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kusambaza siasa za Chadema.

  Chanzo cha habari hii kime- dai kwamba kikao hicho cha siri kilikuwa na agenda mbalimbali ambapo agenda kuu ilikuwa ni kuandaa mkakati kabambe wa kupambana na CCM katika Uch- aguzi Mkuu wa mwaka huu.

  Kupitia agenda hiyo ndipo ul- ipitishwa mkakati wa kusambaza siasa za Chadema kwenye madhe- hebu ya dini kwa kutumia vijana ambao watakuwa na hoja mahu- susi za kuwashawishi waumini waunge mkono chama hicho.

  Pia katika kikao hicho walikubaliana kuingiza uchochezi kwa wananchi wa kuwahamasisha wa- nanchi kuanza kudai mchakato wa Katiba Mpya pamoja na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

  Chanzo cha habari hii kiliende- leza kuelezea kwamba pamoja na mkakati huo pia wachumbe wa mkutano huo waliazimia kuunda UKAWA mpya yenye nguvu kubwa.

  Kwamba viongozi wa chama hi- cho waliridhia kuungana na Chama Cha ACT Wazalendo lengo ni ku- unganisha viongozi kutoka Zanzi- bar kupitia ACT.

  Kikao hicho kiliingiza azimio la kuwashughulikia kwa njia yoyote wabunge na watu ambao ni maaduiwa mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.

  Azimio lingine ambalo wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema wali- kubaliana ni kuandaa ziara nchi nzi- ma kwa kuwashirikisha wabunge na wenyeviti wa kanda.

  Katika hatua nyingine chanzo cha habari hii kilidai kwamba Mbowe amekuwa akitumia mbinu hiyo ya kuendesha vikao katika hoteli zake kama njia moja wapo ya kunyonya fedha za chama.

  Tanzanite lilifanya jitihada za kumtafuta Mbowe ili kudhibitisha madai hayo lakini hakupatikana kutokana na simu yake kutopati- kana.

Mwanaharakati Huru ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Cz Informstion & Media Consultant Ltd, Cyprian Musiba akizuingumza na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi mkuu unaotalajiwa kufanyika mwaka huu na kuhitajika kuchaguiliwa tena kwa Rais Kipenzi cha Watanzania Dkt. John Magufuli kuiongoza nchi hii.Mazungumzo hayo yal;ifanyika jijini Dar es Salaam jana. Picha na Deus Mhagale

 

 

BOSTON, MAREKANI

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) na Makamu wa Tatu wa Rais wa
Shirikia la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt.
Agnes Kijazi, amewataka watendaji wa Shirika la
Hali ya Hewa Duniani (WMO) kuandaa mpango wa
pamoja wa kuboresha zaidi uaandaaji na
uwasilishwaji  wa taarifa za hali ya hewa kwa jamii
zinazoishi katika mazingira hatarishi.
Dkt. Kijazi aliyasema hayo wakati akichangia mada
katika mkutano ulioandaliwa na WMO kwa
kushirikiana na Taasisi ya Hali ya hewa ya
Marekani “National Oceanic and Atmospheric
Administration (NOAA)- National Weather
Service,” uliofanyika Januari 11, 2020 Boston,
nchini Marekani.
Lengo la mkutano huo  lilikuwa kujadili uboreshaji
wa uandaaji na uwasilishwaji wa taarifa za hali ya
hewa  kwa jamii zinazoishi katika mazingira
hatarishi, hususan visiwa vilivyopo katika ukanda
wa tropic na arctic (Improving Communication and
Preparedness in Vulnerable Regions and

Underserved Communities of the tropical and
Arctic region islands), ambavyo viko katika
mazingira hatarishi ya kukumbwa na vimbunga na
mawimbi ya tsunami.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi
wa WMO, ikiwa ni pamoja na Rais wa WMO Prof.
Gerhard Adrian, Makamu wa kwanza wa Rais wa
WMO Prof. Celeste Saulo, Makamu wa Pili wa Rais
wa WMO Ndugu Albert Martis na Makamu wa
Tatu wa Rais wa WMO Dkt. Agnes Kijazi.
Wengine ni Katibu Mkuu wa WMO, Prof. Petteri
Taalas, Wakuu wa Taasisi za hali ya hewa kutoka
baadhi ya nchi wanachama wa WMO na wadau wa
huduma za hali ya hewa, miongoni mwao ikiwa ni
sekta binafisi na watafiti kutoka Vyuo Vikuu.
Majadiliano ya mkutano huo yalijielekeza zaidi
katika matokeo ya tafiti zilizofanyika katika nchi
za Guyana, Finland, Indonesia, Marekani (Jimbo la
Alaska), visiwa vya Caribbean na Bahamas, pamoja
na eneo la Pacific zilizowasilishwa.

Tafiti hizo ziliainisha changamoto katika uandaaji
na uwasilishwaji wa taarifa za hali ya hewa kwa
jamii zinazoishi katika mazingira hatalishi ya
kukumbwa na majanga yanayotokana na hali mbaya
ya hewa, ambayo hutokea katika maeneo hayo.
Vile vile, tafiti hizo ziliainisha njia za asili
zinazotumiwa na jamii hizo katika kuchukua
tahadhari  na kutoa mapendekezo ya kuboresha ili
kupunguza maafa yanayotokana na majanga hayo.
Akichangia mada, Dkt. Kijazi alifafanua kwamba
kwa kuwa changamoto zilizowasilishwa zinaweza
kuwepo katika maeneo mengi, yakiwemo maeneo
yanayofanana na hayo yaliyopo katika bara la
Afrika, ni vyema kuandaa mpango wa pamoja
utakaoratibiwa na WMO wa kushughulikia
changamoto hizo.

Hivyo, akawataka watendaji wa WMO kuangalia
uwezekano wa kuandaa mpango huo ili kuboresha
zaidi uaandaaji na uwasilishwaji  wa taarifa za hali
ya hewa kwa jamii husika.

Ili kuharakisha utatuzi wa
changamoto  zilizowasilishwa, viongozi waandamizi
wa WMO (Rais, Makamu wa Rais wote watatu na
Katibu Mkuu) wameazimia kufanya vikao kwa njia
ya mtandao (teleconference) kila mwisho wa
mwezi, kuanzia mwezi Januari 2020.

Mkutano huu ni sehemu ya mkutano mkuu wa 100
wa wadau wa huduma za hali ya hewa wa
Marekani  unaofanyika Boston, Marekani kuanzia
tarehe 10 hadi 16 Januari, 2020 kujadili
utekelezaji wa maazimio ya mkutano mkuu wa
WMO uliofanyika Juni 2019. Dkt. Kijazi anashiriki
katika mkutano huo kama Makamu wa Tatu wa Rais
wa WMO.
CAPTION
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) na Makamu wa Tatu wa Rais wa
Shirikia la Hali ya Hewa Duniani (WMO)
akifafanua jambo walipokutana na Mkurugenzi wa
Taasisi ya Hali ya Hewa ya Canada (ambaye pia ni

msaidizi wa Naibu Waziri mwenye dhamana ya
masuala ya hali ya hewa), Diane Campbell kwa
maongezi mafupi wakati wa mapumziko nje ya
ukumbi wa mkutano Boston nchini Marekani.

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh