Ubarozi

Kwa miaka mitano Rais Magufuli kapunguza kiwango cha umaskini kutoka asilima 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia

(SOMA ZAIDI)

Serikali imeuomba Umoja wa Ulaya (EU) kuwekeza katika maeneo ya maendeleo
ambayo tayari Serikali imeanza kuyatekeleza ikiwemo uboreshaji wa miundombinu
katika mkataba mpya wa ushirikiano kati ya Tanzania na EU kwa mwaka 2021 hadi
2027.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,
alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini
Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi.
Dkt. Mpango alisema kuwa, katika mkataba mpya wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya
Tanzania na EU unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2021 ni vema ukaendelea
kuimarisha maeneo ya maendeleo ambayo tayari yameanza kutekelezwa na Serikali
hususani katika Sekta ya Elimu, Afya, miundombinu na mingine ili kufikia malengo
endelevu.

 

Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango
Kwa upande wake Balozi wa EU nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, aliipongeza
Serikali kwa kuwa na Sera nzuri za maendeleo lakini pia akasema kuwa ili kuboresha
mazingira ya kibiashara, miongoni mwa mambo yanayohitajika ni pamoja na
Miundombinu, mafunzo, kuwa na uchumi wa kidigitali na siasa bora, mambo ambayo
Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuyatekeleza.

Mhe. Manfredo Fanti, Balozi wa EU nchini Tanzania
Katika tukio jingine, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango namekutana na
mkufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikianao wa Biashara wa Finland, Mhe. Ville
Skinnari, ambapo walijadili mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya ushirikiano na
maendeleo ya kiuchumi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani, Umoja wa Ulaya (EU), Angola na Kuwait nchini, na kuwahakikishia kuwa Tanzania ipo salama, na pia katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu utakuwa wa huru na haki.

Akizungumza na mabalozi hao waliofika kwa wakati tofauti ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo, Simbachawene amesema vyombo vyake vinaendelea kufanya kazi kwa weledi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao nchini.

“Tunatarajia kufanya uchaguzi mwaka huu, na swali lako hali ya usalama nchini, tunawahakikishia nchi ipo salama, ulinzi utaimarishwa na uchaguzi utakua wa huru na haki,” alisema Simbachawene.

Pia Waziri Simbachawene aliwahakikishia shirikiano zaidi kati ya Wizara yake na mabalozi hao katika masuala mbalimbali ya utendaji kazi.

“Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yangu imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio hapa nchini,” alisema Simbachawene

Simbachawene aliwashuru mabalozi hao kwa kumtembelea, na aliwataka wawe huru muda wowote wanapohitaji kumuona wanakaribishwa ofisini kwake.

“Najisikia furaha kwa ujio wenu na karibuni sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Simbachawene.

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh