Uchumi

Kwa miaka mitano Rais Magufuli kapunguza kiwango cha umaskini kutoka asilima 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia

(SOMA ZAIDI)

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kushoto), akisaini Mikataba mitano yenye thamani ya Dola za Marekani 495.59 na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru (kulia) katika hafla iliyofanyika Benki Kuu Jijini Dar es Salaam.

Serikali ya Tanzania na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), zimesaini mikataba mitano ya mkopo wa masharti nafuu ya Dola za Marekani milioni 495.59 ambayo ni sawa na TZS trilioni 1.14 zitakazowezesha kutekeleza ujenzi wa miradi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato Jijini Dodoma, Dola za Marekani  milioni 271.63, ujenzi wa barabara ya Bagamoyo-Holoholo-Lungalunga–Malindi km.120.8 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 168.76 na Dola 55.2 kwa ajili ya Programu ya utawala bora na kuendeleza Sekta Binafsi.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kushoto), akibadilishana nakala ya Mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru (kulia) katika hafla iliyofanyika Benki Kuu Jijini Dar es Salaam, Tanzania na AfDB zimesaini mikataba mitano yenye thamani ya Dola za Marekani 495.59.

Katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James alisema kuwa Serikali ya Tanzania na Benki ya Maendeleo Afrika zimekuwa na mahusiano mazuri ambayo yamewezesha kutolewa kwa mkopo huo wenye masharti nafuu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano (Ujenzi), Mhandisi Elius Mwakalinga akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege wa Kimaifa wa Msalato Jijini Dodoma, Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Pangani-Tanga uliofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam.

“Kama tunavyojua sekta ya miundombinu ndiyo sekta muhimu ambayo inaweza kuinua biashara na kukuza uchumi kwa hiyo katika kulitambua hilo Benki ya Maendeleo Afrika imekubali kutupatia mkopo huu, ambao utatumika katika utekelezaji wa kuboresha miundombinu kwa ujenzi wa Uwanja mkubwa wa Ndege Msalato Jijini Dodoma utawezesha kumudu ndege kubwa za kimataifa kutua”, alisema Doto James.

Afisa Mtendaji Mkuu Tanroad, Patrick Mfugale akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege wa Kimaifa wa Msalato Jijini Dodoma, Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Pangani-Tanga uliofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa kupitia mikataba hiyo AfDB itaipatia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mikopo ya masharti nafuu  ya dola za Marekani milioni 198.63 kupitia dirisha la African Davelopment Bank ( ADB Window), dola Marekani milioni 246.96 kupitia African Development Fund (ADF Window) na dola milioni 50 kupitia mfuko wa Serikali ya China unaosimamiwa na AfDB.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, akizungumza katika Hafla ya hafla ya utiaji saini wa mikataba ya Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege wa Kimaifa wa Msalato Jijini Dodoma, Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Pangani-Tanga uliofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege Msalato na ujenzi wa barabara ya Bagamoyo-Pangani kwa kiwango cha lami itaisaidia Serikali kuziba pengo la miundombinu na kuchochea kasi ya maendeleo ya Uchumi kwa jamii ya watanzania.

Aidha kupitia AfDB miundombinu ya barabara mbalimbali imeshatekelezwa na zinaendelea kutekelezwa zikiwemo za Tabora-Koga-Mpanda Km 342.9, Mbinga-Mbamba bay Km. 66, mradi wa awamu ya pili ya mabasi yaendayo kasi Km. 20.3, Kabingo-Kasulu-Manyovu Km. 260, barabara ya kuzunguka Jiji la Dodoma Km.110.2 huku upande wa Zanzibar AfDB inafadhili barabara za Bububu-Mahonda-Mkokotoni Km.31 na barabara za kuunganisha vijiji vya Zanzibari Km.21, kwa hiyo benki hii ni wadau wakubwa wa maendeleo Tanzania

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano (Ujenzi), Mhandisi Elius Mwakalinga (wa pili kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika(AfDB), Alex Mubiru( wa pili kulia), Afisa Mtendaji Mkuu Tanroad, Patrick Mfugale na watendaji wa Mamlaka Viwanja vya Ndege na Tanroad mara baada ya utiaji saini wa mikataba ya Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege wa Kimaifa wa Msalato Jijini Dodoma, Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Pangani-Tanga uliofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam.

Pia Alibainisha kuwa kuna barabara nyingi za ufadhili kutoka Benki ya Maendeleo Afrika zimekamilika na kutumiwa na wananchi kufanya biashara na kukuza uchumi wao zikiwemo za Arusha-Namanga km. 105, Singida-Babati-Minjiru km. 223.5, Iringa Dodoma km.260, Tunduru-Mangaka-Mtambaswala km.202.5, Namtumbo-Tunduru km.193 Dodoma-Babati km.188.1 na Arusha bypass km.42.4 pamoja na upanuzi wa barabara ya Sakina-Tengeru km 14.1 kwa njia nne kwa hiyo ushirikiano huu umewezesha kuimarisha ujenzi wa miundombinu hiyo ili kumarisha sekta ya usafirishaji.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika AfDB nchini Tanzania, Bw. Alex Mubiru, alisema kuwa mikataba hiyo inayotoa dola za Marekani 495.6 zitafikisha dola za Marekani bilioni 2.38 ambapo kati ya hiyo dola za Marekani bilioni 1.47 zimewekezwa kwenye miradi ya miundombinu.

“Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Msalato utachukua takribani miaka minne ambapo inakadiliwa kuwa na uwezo wa kubaba ndege 50, 000 kwa mwaka, abiria 1.5 na utakuwa uwanja mkubwa wa kimataifa Jijini Dodoma utakatumiwa na zaidi ya watu milioni 200 duniani kote wafanyabiashara na watalii”, Alisema Alex Mubiri.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanroad, Mhandisi Patrick Mfugale alisema kuwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato Jijini Dodoma utakuwa na uwezo wa Kutosha kubeba ndege kubwa kwani utakuwa na urefu wa kilomita 3.6 na upana wa mita 60.

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika(AfDB), Alex Mubiru, akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege wa Kimaifa wa Msalato Jijini Dodoma, Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Pangani-Tanga uliofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Jijini Dar es Salaam.

“Uwanja huu wa Msalato Jijini Dodoma utakuwa mkubwa wa kuhudumia ndege kubwa aina ya Dreamliner 17, na kama ni aina ya Airbus ni ndege 380, magari  ya kawaida 472, na mabasi ya abiria 72, na ukimalizika utahudumia abiria mililioni 1.5 kwa mwaka”, alisema Mhandisi Mfugale.

Lakini pia ujenzi wa daraja la mto pangani utasaidia wananchi wa Tanga kufanya biashara zao bila usumbufu ambapo daraja hilo litakuwa na nguzo nane, huku barabara ikiwa na km 105 barabra kuu na km. 25 barabara unganishi.

Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa mfumuko wa bei wa taifa umezidi kuimarika kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2020 baada ya kubaki palepale kwenye asilimia 3.7 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioshia Januari 2020.

Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa(NBS), Bi.Ruth Minja, akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali ya Mfumuko wa Bei kwa Mwaka ulioishia Februari 2020, Mkutano ulifanyika Ofisi za Takwimu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Bi.Ruth Minja alisema kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioushia mwezi Februari, 2020 imebaki kuwa sawa na kasi ya iliyokuwepo mwezi Januari, 2020.

“Hali hii ya mfumuko wa bei kubaki kuwa sawa kama ilivyokuwa mwezi Januari imechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Februari 2020”, alisema  Bi. Ruth Minja.

Aidha ameongeza  kuwa kuna baadhi ya bidhaa za vyakula kama nyama ambayo iliongezeka kwa asilimia 1.6, samaki 6.1, mafuta ya kupikia 2.8, maharage 9.3 na viazi vitamu 4.2. Ongezeko la bei ambalo limekuwepo kwa Februari 2020 ni sawa na ongezeko hilo Februari 2019

Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilipungua bei kwa mwezi Februari, 2020 zikilinganishwa na bei za mwezi Februari, 2019 kama vile jiko la gesi ya  kupikia lilipungua kwa asilimia 1.6, viatu vya watoto asilimia 1.0, mafuta ya nywele za  wanawake asilimia 2.5 na  gharama za huduma za starehe asilimia 1.0.

Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa(NBS), Bi.Ruth Minja, akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu hali ya Mfumuko wa Bei kwa Mwaka ulioishia Februari 2020, Mkutano ulifanyika Ofisi za Takwimu Jijini Dar es Salaam.

Minja alibainisha kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioisha mwezi Februari, 2020 umeongezeka hadi asilimia 5.9 kutoka asilimia 5.7 kwa mwaka ulioishia Januari 2020.

Aliitaja Tanzania katika Nchi za  Afrika Mashariki kuwa imeendelea kuwa vizuri kwenye mfumuko wa bei kwa asilimia 3.7 ikilinganishwa na Kenya asilimia 6.37 kutoka asilimia 5.78, wakati Uganda mfumuko wa bei umebakia pale pale 3.4 kwa mwaka ulioishia Januari 2020.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga (katikati), akielekeza jambo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mtwara, Mhandisi, Dotto Chacha (Wa Kwanza Kulia), alipofika kukagua hatua za ujenzi zilizofikiwa katika mradi wa upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mtwara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga,
amesema kuwa ameridhishwa na mradi wa upanuzi wa ujenzi wa Kiwanja
cha Ndege cha Mtwara ambao unajengwa na mkandarasi M/S Beijing
Construction Engineering Group Company Ltd na kugharimu shilingi Bilioni
50.3

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mtwara, Mhandisi, Dotto Chacha, akimuonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga (kulia), hatua ya ujenzi iliyofikiwa ya upanuzi wa Kiwanja cha ndege cha Mtwara.

Akizungungumza wakati akikagua kiwanja hicho ambacho utekelezaji wake
umefika asilimia 31, Mwakalinga, amesema kuwa kukamilika kwake
kutafungua fursa nyingi za uwekezaji katika mkoa huo na kutasaidia
kurahisisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Mwakalinga amebainisha kuwa mkandarasi anaendelea kutekeleza kazi
zake vizuri kwani kazi nyingi za awali ambazo zinahusisha upanuzi wa
uwanja huo zimefanyika kwa asilimia kubwa.
“Hadi sasa kazi inaendelea vizuri, ukiangalia kazi nyingi za awali
zimeshafanyika, kinachotakiwa kwa sasa ni kwa mkandarasi kuendelea na
hatua zinazofuata ili kukamilisha kazi hiyo kwa mujibu wa mkataba”,
amesema Mwakalinga.
Ametaja kazi hizo kuwa ni kuchimba eneo kwa ajili ya kuacha nafasi ya
kuweka tabaka mbalimbali za barabara ya kurukia na kutua ndege pamoja
na kuweka lami nyepesi juu ya tabaka lililochanganywa na saruji katika
barabara hiyo ambayo imefika asilimia 46.
Aidha, ameongeza kuwa kiwanja hicho ambacho kilijengwa kwa mara ya
kwanza na kuanza kutoa huduma katika miaka ya 1952/53 hakikidhi
mahitaji ya ukuaji wa uchumi, hivyo Serikali imeamua kupandisha daraja
kiwanja hicho ili kuweza kuhudumia ndege kubwa za ndani na nje ya Nchi.
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS), mkoa wa Mtwara, Mhandisi, Dotto Chacha, amesema kuwa
upanuzi wa kiwanja hicho unahusisha ujenzi wa barabara ya magari ya
kuingia na kutoka kiwanjani pamoja na maegesho ya magari.

Muonekano wa upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Mtwara ukiwa katika hatua za awali. Mradi huo umefika asilimia 31 na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2020.

“Tunatarajia ujenzi huu utakidhi viwango vya kimataifa kwa kuongeza
daraja kutoka code 3C ya sasa kwenda code 4E na itahusisha ujengaji wa
uzio wa usalama kuzunguka kiwanja, uwekaji wa mfumo wa umeme wa
akiba, vifaa vya zimamoto pamoja na taa na alama za kuongozea ndege”,
amefafanua Chacha.
Katika hatua nyingine, Mwakalinga, amekagua barabara ya Mtwara-
Nanyamba- Tandahimba-Newala-Masasi sehemu ya Mtwara- Mnivata (Km
50) ambapo utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 75.67
Mwakalinga amebainisha kuwa asilimia hiyo inahusisha ujenzi wa
makalvati madogo 41 kati ya 43 pamoja na ujenzi wa makalvati makubwa
manne kati ya sita yamekamilika kwa asilimia mia.

Muonekano wa barabara ya Mtwara- Nanyamba- Tandahimba-Newala-Masasi sehemu ya Mtwara- Mnivata (Km 50), katika kijiji cha Mnivata, ambapo ujenzi wake mahali hapo upo katika tabaka la awali.

Awali wakati akielekea mkoani Mtwara, Mwakalinga alikagua mizani wa sisi
kwa sisi uliopo mkoani Ruvuma na kuwataka watumishi wa mizani hiyo
kuwa mfano wa kuigwa na watumishi wengine kwa kuepuka vitendo vya
rushwa na kufanya kazi kwa uadilifu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,

Uchukuzi na Mawasiliano.

 

BENKI ya NMB, imetangazwa kuwa Mdhamini Mkuu wa Mbio za Bima Marathon 2020, zinazotarajiwa kufanyika Machi 28 jijini Dar es Salaam, chini ya uratibu wa Kampuni ya African Digital Banking Summit.

Kwa udhamini huo, mbio hizo zinazoenda kufanyika kwa mara ya pili mfululizo, zitatambulika kwa jina la NMB Bima Marathon 2020, ambazo zitahusisha mbio za kilomita 21, kilomita 10 na kilomita tano.

NMB imedhamini mbio hizo kwa kitita cha Sh. Milioni 35, ambako hafla ya NMB kutangaza udhamini wake huo katika mashindano hayo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi ya udhamini, Meneja Mwandamizi wa Bima wa NMB, Martin Massawe, alisema wamevutiwa kudhamini Bima Marathon kutokana na mlengo wake.

“Mashindano haya yanatumika kama jukwaa la kutoa elimu ya Bima kwa Watanzania, lakini pia kuimarisha afya. Nasi tumeona ni fursa tunayoweza kuitumia kutangaza huduma mpya ya Bancassuarance.

“Lakini hii sio mara ya kwanza kwetu NMB kudhamini michezo, tumefanya hivyo katika soka ambako tumeidhamini Taifa Stars na timu za Azam FC na Singida United. Tumefanya hivyo pia katika mpira wa magongo, gofu na kriketi na kadhalika,” alisema Massawe.

Alitumia fursa hiyo kuwatakia Watanzania kujenga utamaduni chanya wa kutumia bima kadri ya matahitaji yao, kwa kutembelea matawi yote 224 kote nchini na kukata bima mbalimbali, zikiwamo za maisha, magari, afya, nyumba, kilimo na dhamana kutoka kwa wabia wake.

Huduma za bima zitakazopatikana katika matawi ya NMB ni pamoja na zile za Kampuni za Sanlam Life, UAP, Shirika la Bima la Taifa (NIC), Jubilee Insurance, Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) na Reliance Insurance.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya African Digital Banking Summit inayoratibu mbio hizo, Baraka Mtavangu, aliipongeza NMB kwa udhamini, anaoamini unaenda kubadili taswira ya mashindano hayo.

Alibainisha kuwa, mbio hizo zitanatarajia kushirikisha wakimbiaji watu wazima wapatao 3,500 na watoto 500, na kwamba usajili unafanyika katika vituo mbalimbali, ikiwemo Mlimani city na baadhi ya matawi ya NMB kwa Sh. 20,000 kwa watu wazima na Sh. 15,000 kwa watoto.

“Kutakuwa na Washindi wa kwanza hadi wa tano katika mbio za kilomita 21 na kilomita 10, ambako mshindi wa km 21 atatwaa Sh. Mil. 1, huku mshindi wa km 10 atajishindia Sh. 700,000. Zawadi zingine zitatangazwa baadaye,” alisema Mtavangu.

Mratibu huyo alilishukuru Shirikisho la Riadhaa Tanzania (RT) kwa sapoti, ushirikiano na kibali cha uendeshaji wa mbio hizo, ambazo alisema zitashirikisha Watanzania na wageni wanaoishi nchini, huku wakimbiaji wa nje wakitakiwa kujiandikisha kupitia chama cha riadha nchini .

Picha ni Mhandisi wa mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Kadaya Baluhye akiongea na mafundi wa vifaa vya kieletroniki kwenye mkutano wao na mamlaka hiyo jijini Arusha picha na zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA Kanda ya kaskazini imewataka mafundi wa vifaa vya kieletroniki ikiwemo simu za mkononi kuwa kwenye mfumo wa umoja kwa kuanzisha vikundi vyao kwa Kanda au mkoa.
Kwa muktadha huo kuanzia mwezi julai mwaka huu hakuna fundu ambaye atafanyakazi kama hajasomo wala kusajiliwa hivyo ni muhimu kwenu kujiunga kwenye kikundi ili kupatiwa elimu.
Meza kuu ni Kaimu meneja wa Kanda ya kaskazini wa TCRA Jan Kaaya akiwa na viongozi wa umoja wa mafundi simu Kanda ya kaskazini kwenye mkutano wa mafundi wa vifaa vya kieletroniki uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha
Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria wa mamlaka hiyo Kant Mosha wakati wa mkutano wa mafundi wa vifaa vya kieletroniki uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo aliwataka kuacha kutokuwa na usajili wa kikundi ndio suluhisho.
Alisema kuwa mafundi simu ni kada ambayo ilikuwa imesahauliwa hapo awali lakini kupitia serikali ya awamu ya tano chini ya Rais dkt.John Magufuli imeamua kuwatambua hivyo kuungana ni sehemu ya kufanikiwa kwa malengo yenu.
.Sehemu ya mafundi simu kutoka mikoa ya Manyara na Arusha wakifuatilia kwa kina mkutano huo wa mamlaka ya mawasiliano TCRA Kwenye mkutano wa mafundi simu kutoka Kanda ya kaskazini picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mafundi simu Kanda ya ziwa Maguwa Manyanda amewataka kutambua kwamba mafundi simu ni wathamani kwani jamii inwategemea na wanachangia mapato ya serikali hivyo busara ni kuona umoja ndio suluhisho la changamoto zao.
Alisema kuwa mafunzo hayo yataondoa changamoto na kuwafanya kuwa huru katika shughuli zao za kila siku hivyo umoja ni nguzo ya kuwafikisha kuweza kushirikiana na serikali katika masuala mbalimbali ikiwemo vyombo vya Dola.
Wadau wa sekta ya mawasiliano wakifuatilia mkutano wao na mamlaka ya mawasiliano TCRA wakati walipowataka kuunda umoja wao kwa lengo la kukabiliana na kero mbali mbali picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Alieleza kuwa kufanikiwa ili kila moja aweze kutenda kazi zake ni muhimu Sana wakajiunga na umoja ili kuondoa changamoto zao ambazo zimekuwa zikiwafanya kujikuta wakikumbana na jeshi la polisi.
Nae Mwenyekiti wa umoja wa mafundi simu Kanda ya kaskazini Nasri Mshana Mtengeti alisema kuwa wamefirahi Sana kupata elimu hiyo ya umoja ambayo itawasaidia kuondokana na changamoto hivyo tuhamasishane kujiunga na umoja huu.

Awali akitoa mafunzo kwenye mkutano huo mratibu wa vikundi hivyo kutoka mamlaka ya mawasiliano mhandisi Kadaya Buluhye aliwataka mafundi hao kufanyakazi kwenye umoja kwa lengo la kupata elimu na usajili.
Alisema kuwa jeshi la polisi linafanyakazi ya kulinda usalama na Mali za raia Ila umoja wenu utasaidia kufanya kazi kwa karibu na jeshi hilo na kuondoa changamoto zenu ambazo mmekuwa mkikumbana nazo kama mafundi.
Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh