Usalama

Kwa miaka mitano Rais Magufuli kapunguza kiwango cha umaskini kutoka asilima 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia

(SOMA ZAIDI)

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akikagua mradi wa ujenzi wa kituo cha Polisi kilichopo wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, leo 02/03/2020 wakati akiwa safarini kuelekea mkoani Manyara kwa ajili ya ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.

02/03/2020 BABATI, MANYARA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati), akizungumza na Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Paul Kasabago, wakati akipokelewa na mwenyeji wake kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi mkoani humo leo 02/03/2020. Picha na Jeshi la Polisi.

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akitoka katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, ambapo alisaini kitabu cha wageni na kuzungumza na maofisa wa vyeo mbalimbali na kuwakumbusha wajibu wao katika utendaji kazi, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.

 

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akisalimiana na Watumishi wa Wizara ya Ulinzi na JKT alipowasili kwa ajili ya kuripoti katika kituo chake kipya cha kazi Mtumba Jijini Dodoma nyuma yake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Florens Turuka aliyestaafu utumishi wake.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe  amekabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Dkt. Florens Turuka na kuanza kazi mara moja huku akiahidi kushirikiana vema na watumishi.

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Ulinzi na JKT zililopo katika Mji mpya wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma Dkt. Mnyepe alilakiwa na Watumishi wa Wizara hiyo wakiongozwa na Dkt. Florens Turuka ambaye amestaafu utumishi kwa umri.

Baadaye tukio la makabidhiano lilifanyika katika ukumbi wa Wizara na kuhudhuriwa na Makamishna, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Ulinzi na JKT.

Akizungumza baada ya kumkabidhi nyaraka mbalimbali za Wizara Katibu Mkuu anayemaliza muda wake wa Utumishi Dkt. Florens Turuka aliwashukuru Makamishna, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na watumishi kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu Wizarani hapo.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akisaini kitabu cha wageni muda mfupi kabla ya kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake aliyesimama pembeni Dkt. Florens Turuka ambaye amestaafu utumishi kwa umri.

Dkt. Turuka alisema “daima nitaukumbuka mchango mkubwa nilioupata kwa Makamishna, Wakuu wa Idara, Vitengo na watumishi wote wa Wizara hii, kwani hakuna kazi iliyoshindikana chini yao”

“Namshukuru mwenyezi Mungu kuwa niliingia Wizara ya Ulinzi mwaka 2016 na mpaka nastaafu utumishi wangu nimejifunza mambo mengi saana yanayohusu Ulinzi wa nchi yetu” Alisema Dkt. Turuka

Naye Katibu Mkuu mpya Dkt. Faraji Mnyepe akiongea na Makamishna, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alianza kwa kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kisha akamshukuru Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kumuamini na kumteua kuongoza Wizara nyingine nyeti.

“Nimetoka kuongoza Wizara nyeti ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki sasa nipo Wizara ya Ulinzi na JKT ambayo kuna mambo mengi ya msingi yanahusiana kabisa” Alisema Dkt. Mnyepe

Dkt. Mnyepe alisema katika kufanya kazi kwake siku zote yeye amekuwa akiamini ‘Timu Work’ ambapo pamoja na mambo mengine mfumo huu ndiyo wenye mafanikio na ufanisi mkubwa katika kazi.”

Dkt. Florens Turuka Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi anayemaliza muda wake wa Utumishi akimkarisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe katika ofisi yake mpya Mtumba Jijini Dodoma.

Akitoa neon la shukrani kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo Kaimu Kamishna wa Rasilimali watu Wizara ya Ulinzi na JKT Marco Baruti alimshukuru saana Katibu Mkuu anayeondoka na kusema siku zote walimuona kama Mwalimu kwao kwa mambo mbalimbali aliyokuwa akiwafundisha pindi wanapokosea

Pia akamkaribisha Katibu Mkuu mpya na kumuahidi ushirikiano mkubwa katika kufanikisha shughuli za Serikali na kuifanya Wizara ya Ulinzi iendelee kuwa katika hali yake.

Februari 06 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimteua Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kufuatia Dkt. Florens Turuka kustaafu wadhifa huo kwa umri.

HALMASHAURI YA KINONDONI

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bi Faudhia Nombo amefungua na kufunga  mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa watendaji wa kata ambao wanafahamika kama maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata.

Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Vikroria Wihenga, Afisa Utumishi Bi. Faudhia Nombo, wakismikiliza Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles wakati alipotembelea kukagua mafunzo kwa watendaji yaliyokuwa yakitolewa na tume hiyo.
Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bi. Vikroria Wihenga,akizungumza wakati wa kumkaribisha Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles wakatikati mwenye suti wakati alipotembelea kukagua mafunzo kwa watendaji yaliyokuwa yakitolewa na tume hiyo. Kulia ni Afisa Utumishi Bi. Faudhia Nombo.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bi. Faudhia Nombo akizungumza na watendaji waliokuwa wakipewa mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles, akishuhudia watendaji waliokuwa wakifanya mazoezi ya kujifunza namna ya kutumia ( BVR KIT-Biometric Voters Registration Kit) wakati alipotembelea kukagua mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yaliyosimamia na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, yalianza kutolewa Februali 10 na kumalizika Februari  11 katika ukumbi wa Polisi Ofis Mes ambapo jumla ya Kata 20 zilizopo katika Halmashauri hiyo zilishiriki.

Akizungumza wakati wa kufungua na kufunga mafunzo hayo, Bi Faudhia alisema kuwa mafunzo hayo ni chachu kwa maafisa hao na kwamba wanapaswa kutumia nafasi hiyo vizuri ili kuisaidia Serikali kupata idadi kamili na sahihi ya wananchi watakaopiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Alifafanua kuwa  waandikishaji hao wasaidizi kwa ngazi ya kata wanapaswa kuhakikisha kuwa wanafuatilia na kusikiliza mafunzo hayo kwa umakini mkubwa kwani kazi hiyo ya uboreshaji wa dafatri ni nyeti na ni kwa maslahi ya maendeleo ya nchi.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yaliyotolewa kwa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata ambapo yanahusisha mfumo mzima wa namna ya mchakato wa uandikishaji ambapo mfumo huo umegawanyika katika maeneo matatu.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni uandikishaji wa mwananchi mpya kabisa,  uboreshaji wa taarifa za mpiga kura kwenye daftari (hii ni iwapo mwananchi alihama eneo la makazi au iwapo taarifa zilikosewa) pamoja na kumuondoa mpiga kura kwenye daftari kutokana na sababu mbalimbali kama vile kifo.

Alisema mafunzo hayo pia yalitolewa kwa watendaji ambao watahusika na uingizaji wa taarifa za wapiga kura katika mfumo wa kuandikisha wapiga kura (BVR Kit operator) pamoja na waandikishaji wasaidizi.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo pia yalihusisha kuapishwa kwa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata, namna ya ujazaji wa fomu mbalimbali pamoja na namna ya kutumia sanduku litakalotumika kubeba vifaa mbalimbali vilivyounganishwa na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kuingiza taarifa binafsi za mpiga kura ( BVR KIT-Biometric Voters Registration Kit).

“ Naomba niwaeleze jambo moja, kazi hii mliyopewa ni muhimu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ifikapo Oktoba mwaka huu, tunaboresha daftari la wapigakura kwasababu, kuna wengine wametimiza miaka 18 hivi karibuni, wengine wamehama makazi yao, kwa hiyo huu mchakato ni muhimu sana ni waombe mkafanye kwa uangalifu mkubwa” kama mlivyo elekezwa na watoa mada” alisema Bi Faudhia.

Aliongeza kuwa” mnatakiwa kutumia lugha nzuri unapomuhoji mwananchi aliyefika kujiandikisha au kuboresha taarifa zake,tumeambiwa hapa na Maafisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, uandikishaji huu hauhusiani na kitambulisho cha Taifa, kwa hiyo hata kama mtu atakuja kujiandikisha bila kitambolisho cha NIDA muandikisheni.

Zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  litaanza rasmi Tarehe Februari 14 mwaka huu ambapo  litadumu kwa muda wa siku saba (7 ) na hivyo kumalizika Februari 21 mwaka huu.

Kupeleka hoja binafsi Bungeni kuwa Zitto adui wa Taifa

Mbunge wa Jimbo la Siha kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Godwin Molell anatarajia kupeleka hoja binafsi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwanini Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe asichukuliwe kama Adui wa Taifa hili.

Molell alisema amefikia azma  hiyo dhidi ya Zitto ni kutokana na kitendo  cha Mbunge huyo wa Kigoma  kuandika Barua Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Human Rights Watch  Zama Neff ya kutaka Tanzania isipewe mkopo kwa madai kuwa pesa hiyo itatumiwa kisiasa na Serikali ya CCM.

Wakati Molell akiongea hayo,Mwanaharakati huru nchini Cyprian Musiba amesema, anatarajia kuandika barua Benki ya Dunia, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, utakaoelezea mambo mazuri yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John  Magufuli, na kuwataka  wapuuze maneno ya uongo yanayoenezwa watu wasiokuwa wema na nchgi yao.

Mbunge huyo wa Siha alisema, kupitia barua hiyo Zitto amezuia Shule za Bweni zaidi ya 1000 za kisasa ambazo ndio zilikuwa zijengwe kutokana na mkopo huo, ambazo zingeweza kusaidia watoto wa kike ambao wamekuwa na changamoto ya kupata mimba za utotoni.

‘’Hivi huyo Zitto ana akili kweli, yaani mtu anaandika barua Benki ya Dunia kupinga Tanzania isipewe mkopo kwa ajili ya ujenzi wa Shule za kike kwaajili ya ,maslahi yake binafsi, hakika huyu ni muhujumu uchumi’’, alisema Molell.

Mbunge huyo alisema sababu kubwa ya watoto wa kike kupata mimba za utotoni kunachangiwa na umaskini na umbali wa kutoka Shule hadi nyumbani, lakini Serikali ya Magufuli kwa upendo ikaomba mkopo kwa ajili ya kujenga mabweni ya watoto wa kike ili waweze kuepuka changamoto hiyo inayowakabili.

‘’Baada ya  Zitto na huyo mshirika wake kuandika barua ya kuzuia mkopo huo, eti mzungu mmoja  kutoka huko Benki ya Dunia ameleta barua Bungeni, ikihoji eti kwanini Tanzania ipewe pesa?, wakati hizo shule 1000 zitakazojengwa zitaokoa watoto wa kike 200,000 watakao lala katika mabweni hayo’’, alisema Mbunge huyo.

Molell ambaye pia ni mwanaharakati alisema, kwa mujibu wa barua hiyo Zitto anajifanya kama anatetea watoto wa kike,lakini ukweli anawahujumu na hana nia njema na watoto wa kike katika maendeleo yao.

‘’Kuna usemi usemao ukimuelimisha mtoto wa kike, umeelimisha jamii nzima, sasa Rais wetu kwa kulijua hilo alitaka pesa ya mkopo huo, ajenge Shule za Bweni 1000, ambazo zingesaidia watoto hao, lakini Zitto yuko kinyume na harakati njema za Mh. Rais, nafikiri huyu siyo mwenzetu’’, alisema Molell.

Aidha Mbunge huyo wa Siha alisema, anatarajia kuwasiliana na Spika wa Bunge Job Ndung’ai na wabunge wote wanaitakia mema nchi yao kuwapiga vita wanaohujumu Taifa hili kwa kuangalia maslahi yao binafsi.

‘’Kwa mfano huyu Zitto kama Mbunge aliapa kuilinda nchi na kulinda sheria na katiba ya nchi, sasa iweje huyo huyo alisema atailinda nchi, anaenda kubomoa nchi huko Ulaya?, alihoji Molell na kutaka Spika pamoja na wabunge wamchukulie Zitto ka Muhujumu Uchumi’’, alisema Mbunge huyo.

Wakati huo huo  Molell ameshangaa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na genge lake, wanatambea nchi za Ulaya wakiwa na maelezo ya vivutio vya Tanzania yakiwemo Madini, na kuwahadaa mabepari hao kuwa wakiwapa pesa na kufanikiwa kuingai Ikulu, eti wasaidia kuwapati Madini yaliyopo nchini.

‘’ Yaani Mbowe na genge lake ni wezi, amekiibia Chama chake, pesa za Ruzuku karibu Billioni 15, hazieleweki zimefanya kazi gani, kwani hawa wapinzani wapo kwaajili ya kupiga tu’’, alisema Molell.

Mbunge huyo aliziatak Asasi za kiraia kama wao wanatetea haki za binadamu, kwanini haziendi kuulizia wizi unaofaanywa na Mbowe CHADEMA na badala yake wanaisumbua Serikali ya Magufuli inayofanya mambo mazuri.

Mwanaharakati huyo alisema kuwa, katika barua hiyo atakayoandika  mazuri ya Serikali ya  Magufuli, kivuli cha barua hiyo itapelekwa kwa Watanzania waishio nje ya nchi maarufu kwa jina la Diaspora na nyingine atapeleka kwa Waziri wa Mambo ya Nje Profesa Paramagamba Kabudi.

Aidha kufuatia mambo yanayofanywa na Mbunge huyo wa Kigoma, Musiba alisema wao kama wanaharakati  hawawezi kukubali kuona Serikali na Rais Magufuli inachafuliwa wakati wao wapo.

‘’Yaani Zitto anaandika barua kwa Mataifa ya nje kwa kutumia Nembo ya Bunge, kuichafua nchi na Rais wake, sasa naomba Serikali isijibu hiyo barua, na badala yake watuachie sisi wanaharakati tupo kuitetea nchi yetu, hii ndio kazi yetu’, alisema Musiba.

 

Aidha Mwanaharakati huyo alaisema kufuatia barua hiyo ya akina Zitto kupinga ujenzi wa mabweni hayo, inaashiria kuwa Mbunge huyo wa Kigoma anachochea mimba za utotoni kwa watoto wa kike na hana nia nzuri.

‘’Hivi huyu Zitto hana watoto kweli? yeye kama mzazi anawezaje kuandika barua ya kupinga isiletwe pesa hapa nchini kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya watoto wa Kike, hiyo inaoonesha anachochea uzinzi kwa watoto wetu’, alisema Musiba.

 

 

Aidha Musiba ameitaka Benki ya Dunia impuuze Zitto na genge lake, kwani benki hiyo na Tanzania wamekuwa na uhusiano mzuri tangu enzi za Mwalimu Nyerere na Taifa hili halina uhusiano mbaya na Matifa ya nje.

Vilevile Musiba alisema, Zitto ameungana na Tundu Lisu, na Nassoro Mazrui wanafanya ziara Mataifa ya Ulaya, kuomba pesa kwa ajili ya kuharibu Uchaguzi  Mkuu ujao kwa kuunda makundi ya vijana kuleta vurugu katika Uchaguzi Mkuu wa Urais, Wabunge na Madiwani mwishoni mwa mwaka huu.

‘’Wanachokifanya Zitto na genge lake wanaichonganisha Serikali na Mataifa rafiki, ili yasiwe na ushirikiano mzuri na Tanzania, hivyo Serikali isiwaonee huruma watu hawa’’, alisema Mwanaharakati huyo.

Aidha Musiba  alisema kuwa, Maalim Seif  akiwa mshauri Mkuu wa genge hilo, wamelenga kufanya vurugu hizo Zanzibar, ili ipatikane Serikali ya Kitaifa ambayo wanalenga kuwemo katika uongozi wa Serikali hiyo,

‘’Zitto na genge lake wanataka kuunda vikundi vya vijana Visiwani Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu, na itokee vurugu kama iliyotokea miaka ya 90 ikapatikana Serikali ya Kitaifa, Maalim akiwemo.

Mwanaharakati huyo ameeleza kuwa, Zitto anajua hawezi kurudi Bungeni hivyo anataka kutumia njia hiyo ili yeye na wenziwe waweze kupata madaraka ya Kitaifa huko Zanzibar, hivyo amewataka Watanzania kuwa makini na makundi hayo yatakayokuwa yakiratibiwa na Chama cha Siasa cha ACT Wazalendo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Tambarukwa, kilichopo wilaya ya Nkasi katika ziara yake ya kuelemisha na kuwakataza wananchi kuacha tabia ya kuharibu vyanzo vya maji kwa kufanya shughui za kibinaadamu katika milima ya safu za Lyamba Lyamfipa Mkoani Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaonya wananchi wanaokaa karibu na milima ya Lyamba Lyamfipa kuacha maramoja kufanya shughuli za kibinaadamu katika milima hiyo baada ya shughuli hizo kuharibu mazingira na vyanzo vya maji vilivyomo na matokeo yake kuwasababishia maisha magumu wananchi wanaoishi katika bonde la ziwa Rukwa lililozungukwa na milima hiyo.

Amesema kuwa kuwa na maji ni jambo zuri lakini kuendelea kubaki nayo kwa miongo kadhaa ijayo ni jambo kubwa zaidi na kuongeza kuwa milima hiyo ndio chanzo cha maji cha Ziwa Rukwa, ziwa lililobeba jina la mkoa na hivyo kutokuwepo kwa ziwa hilo ni kuondoa asili ya mkoa jambo ambalo hataruhusu litokee.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aiyevaa rain boot) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Swahila, kilichopo wilaya ya Nkasi katika ziara yake ya kuelemisha na kuwakataza wananchi kuacha tabia ya kuharibu vyanzo vya maji kwa kufanya shughui za kibinaadamu katika milima ya safu za Lyamba Lyamfipa Mkoani Rukwa.

“Milima hii yote ndio chanzo cha maji cha watu wanaoishi bonde la Ziwa Rukwa pamoja na Ziwa Rukwa lenyewe, mkiharibu hiyo milima hiyo ni sawa na kufanya mauaji kwa watu wanaoishi katika bonde la Ziwa Rukwa, kwasababu watakosa maji wale wananchi lakini hata mifugo itakosa maji huko lakini tatu hata ziwa rukwa lenyewe litakauka litajaa tope kwa hivyo vitendo vya kibinaadamu vya kukata miti na maji yaliyopo yatakwisha litafutika,” Alisisitiza

Mh. Wangabo ameyasema hayo alipofanya ziara katika vijiji vilivyo karibu na milima ya Safu za Lyamba Lyamfipa katika Wilaya ya Nkasi na Sumbawanga na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi hao juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na milima hiyo ili kupunguza athari za mvua zinazowatokea watu wanaoishi katika bonde la Ziwa Rukwa.

Amesema kuwa kutotunza vyanzo vya maji na vyanzo vya mvua kutasababisha kilimo chetu kutokuwa na tija na kueleza kuwa milima hiyo ndio tegemezo kwa mkoa wa Rukwa pamoja na mikoa ya jirani na hivyo utunzaji wake ni umuhimu kwa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkwamba, kilichopo wilaya ya Nkasi katika ziara yake ya kuelemisha na kuwakataza wananchi kuacha tabia ya kuharibu vyanzo vya maji kwa kufanya shughui za kibinaadamu katika milima ya safu za Lyamba Lyamfipa Mkoani Rukwa.

Ameongeza kuwa mahala ambapo pamefyekwa na kulimwa si sawa na mahali ambapo hapajalimwa na penye miti kwani mvua ikija itachimba mahali ambapo pameshaharibika na kuacha maeneo ambayo yana miti na nyasi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiwasalimia baadhi ya watoto waliohudhuria kwenye mkutano wake wa hadhara alioufanya katika Kijiji cha Swahila, Wilayani Nkasi kuhamasisha utunzaji wa mazingira.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi hao kuwa watulivu na kutoshawishiwa na wanasiasa wasiopenda utulivu uliopo hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais.

Wananchi wa Jijini la Dar es Salaam, wakiwa wamepanga mstari katika Viwanja vya Mnazi Mmoja wakiendelea na zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Nchi nzima, kufuatia agizo la Rais Dkt. Magufuli kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuongeza siku 20 hadi kufikia mpaka January 20 mwaka huu kuwapatia nafasi wananchi waweze kupata namba ya Utambulisho wa Taifa na kuepusha kufungiwa laini zao za Simu.
Baadhi Wafanyakazi kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakiwahudumia wananchi waliojitokeza eneo la Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kwenye zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Nchi nzima, kufuatia agizo la Rais Dkt. Magufuli kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuongeza siku 20 hadi kufikia mpaka January 20 mwaka huu kuwapatia nafasi wananchi waweze kupata namba ya Utambulisho wa Taifa na kuepusha kufungiwa laini zao za Simu.
Afisa kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akimuhudumia mwananchi aliyejitokeza eneo la Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kwenye zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Nchi nzima, kufuatia agizo la Rais Dkt. Magufuli kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuongeza siku 20 hadi kufikia mpaka January 20 mwaka huu kuwapatia nafasi wananchi waweze kupata namba ya Utambulisho wa Taifa na kuepusha kufungiwa laini zao za Simu.

 

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh