Wizara

Kwa miaka mitano Rais Magufuli kapunguza kiwango cha umaskini kutoka asilima 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia

(SOMA ZAIDI)

BAKITA NA BAKIZA zapewa kongole katika kukuza Kiswahili.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zimepongeza Baraza la Kiswahili Tanzania pamoja na Baraza la Kiswahili Zanzibar kwa kazi kubwa waliyofanya katika kuandaa waraka wa ushawishi wa kuingiza kiswahili kama moja ya lugha rasmi ya mawasiliano katika nchi za SADC.

Pongezi  hizo zimetolewa katika kikao cha ushirikiano baina ya  Wizara zenye dhamana ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kati ya Serikali ya Jamahuri ya Muungano wa Tanzania  na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ngazi ya Makatibu Wakuu kilichofanyika Zanzibar Machi 03,2020.

Akizungumza katika kikao hicho ngazi ya Makatibu Wakuu Mwenyekiti ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  Bw.Saleh Yusuf Mnemo amesema kuwa BAKITA na BAKIZA zimefanya juhudi kubwa katika kukuza lugha ya Kiswahili ambayo ni nguzo muhimu katika kudumisha muungano wetu.

“Mabaraza haya mawili yanafanya kazi kubwa sana katika kukuza lugha yetu ya Kiswahili ni lazima tuyapongeze lakini ni vizuri yakaendelea kushirikiana katika kuelimisha watanzania matumizi mazuri na sahihi ya lugha hiyo ili iendelee kuwa miongoni mwa lugha bora duniani”alisema Bw.Saleh Yusuf.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally  Possi ameyataka mabaraza hayo kuendelea kutafuta nama bora zaidi ya kukuza lugha hiyo nje ya nchi kwa kutumia fursa za uhitaji wa watalaam wa lugha hiyo zinazojitokeza kwakua tayari ina kanzidata ya watalaamu hao.

“Sekta hizi zina umuhimu mkubwa katika Muungano wetu ni vizuri wakuu wa idara na taasisi kuwa na utaratibu wa kukutana angalau mara moja kwa mwaka ili kujadili utekelazji wa maazimio ya maeneo ya ushirikiano pamoja na kutatua changamoto ambazo zinajitokeza kabla mamlaka za juu hazijafanya hivyo”alisema Dkt.Possi.

Hata hivyo sekta hizo zimeendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali ambapo zimefanikiwa kuandaa na kushiriki tamasha la JAMAFEST 2019 lililofanyika jijini Dar es Salaam na matamasha mengine kama ZIFF,SIFF pamoja na Sauti za Busara ambayo yanaendelea kuimarisha muungano.

Kikao hicho cha ngazi ya Makatibu wa Wakuu ni maandailizi ya kikao cha Mawaziri wanaosimamia sekta hizo kitakachokuwa na lengo la kupitia utekelezaji wa  maazimio ya maeneo ya ushirikiano waliyotiana saini mwezi julai 2019 Jijini Dodoma.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua mradi wa Maji wa Bokwa wilayani Kilindi, Machi 4, 2020. Kulia ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na kushoto ni Mbunge wa Kilindi, Omar Kigua. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijaza maji katika ndoo wakati alipozindua mradi wa Maji wa Bokwa wilayani Kilindi, Machi  4, 2020. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na kulia ni mmoja wa wanufaika wa mradi huo, Mariam Mgaza Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba ndoo ya maji, Mariam Mgaza Hassan wakati alipozindua mradi wa maji wa Bokwa wilayani Kilindi, Machi 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Makao Makuu ya Wizara na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika Kikao cha kupitia Utekelezaji wa Bajeti na Miradi ya Maendeleo, kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Makao Makuu ya Wizara na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika Kikao cha kupitia Utekelezaji wa Bajeti na Miradi ya Maendeleo, kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kushoto meza kuu ni Waziri wa Wizara hiyo, George Simbachawene.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (wapili kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Wanja Mtawazo (wapili kushoto), alipokuwa anasoma taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti na Miradi ya Makao Makuu ya Wizara katika Kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo wa wa Wizara hiyo na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) cha kupitia Utekelezaji wa Bajeti na Miradi ya Maendeleo, kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dkt. Arnold Kihaule.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akisalimiana na Watumishi wa Wizara ya Ulinzi na JKT alipowasili kwa ajili ya kuripoti katika kituo chake kipya cha kazi Mtumba Jijini Dodoma nyuma yake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Florens Turuka aliyestaafu utumishi wake.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe  amekabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Dkt. Florens Turuka na kuanza kazi mara moja huku akiahidi kushirikiana vema na watumishi.

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Ulinzi na JKT zililopo katika Mji mpya wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma Dkt. Mnyepe alilakiwa na Watumishi wa Wizara hiyo wakiongozwa na Dkt. Florens Turuka ambaye amestaafu utumishi kwa umri.

Baadaye tukio la makabidhiano lilifanyika katika ukumbi wa Wizara na kuhudhuriwa na Makamishna, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Ulinzi na JKT.

Akizungumza baada ya kumkabidhi nyaraka mbalimbali za Wizara Katibu Mkuu anayemaliza muda wake wa Utumishi Dkt. Florens Turuka aliwashukuru Makamishna, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na watumishi kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu Wizarani hapo.

Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akisaini kitabu cha wageni muda mfupi kabla ya kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake aliyesimama pembeni Dkt. Florens Turuka ambaye amestaafu utumishi kwa umri.

Dkt. Turuka alisema “daima nitaukumbuka mchango mkubwa nilioupata kwa Makamishna, Wakuu wa Idara, Vitengo na watumishi wote wa Wizara hii, kwani hakuna kazi iliyoshindikana chini yao”

“Namshukuru mwenyezi Mungu kuwa niliingia Wizara ya Ulinzi mwaka 2016 na mpaka nastaafu utumishi wangu nimejifunza mambo mengi saana yanayohusu Ulinzi wa nchi yetu” Alisema Dkt. Turuka

Naye Katibu Mkuu mpya Dkt. Faraji Mnyepe akiongea na Makamishna, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alianza kwa kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kisha akamshukuru Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kumuamini na kumteua kuongoza Wizara nyingine nyeti.

“Nimetoka kuongoza Wizara nyeti ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki sasa nipo Wizara ya Ulinzi na JKT ambayo kuna mambo mengi ya msingi yanahusiana kabisa” Alisema Dkt. Mnyepe

Dkt. Mnyepe alisema katika kufanya kazi kwake siku zote yeye amekuwa akiamini ‘Timu Work’ ambapo pamoja na mambo mengine mfumo huu ndiyo wenye mafanikio na ufanisi mkubwa katika kazi.”

Dkt. Florens Turuka Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi anayemaliza muda wake wa Utumishi akimkarisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe katika ofisi yake mpya Mtumba Jijini Dodoma.

Akitoa neon la shukrani kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo Kaimu Kamishna wa Rasilimali watu Wizara ya Ulinzi na JKT Marco Baruti alimshukuru saana Katibu Mkuu anayeondoka na kusema siku zote walimuona kama Mwalimu kwao kwa mambo mbalimbali aliyokuwa akiwafundisha pindi wanapokosea

Pia akamkaribisha Katibu Mkuu mpya na kumuahidi ushirikiano mkubwa katika kufanikisha shughuli za Serikali na kuifanya Wizara ya Ulinzi iendelee kuwa katika hali yake.

Februari 06 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimteua Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kufuatia Dkt. Florens Turuka kustaafu wadhifa huo kwa umri.

HALMASHAURI YA KINONDONI

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bi Faudhia Nombo amefungua na kufunga  mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa watendaji wa kata ambao wanafahamika kama maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata.

Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Vikroria Wihenga, Afisa Utumishi Bi. Faudhia Nombo, wakismikiliza Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles wakati alipotembelea kukagua mafunzo kwa watendaji yaliyokuwa yakitolewa na tume hiyo.
Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bi. Vikroria Wihenga,akizungumza wakati wa kumkaribisha Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles wakatikati mwenye suti wakati alipotembelea kukagua mafunzo kwa watendaji yaliyokuwa yakitolewa na tume hiyo. Kulia ni Afisa Utumishi Bi. Faudhia Nombo.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bi. Faudhia Nombo akizungumza na watendaji waliokuwa wakipewa mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles, akishuhudia watendaji waliokuwa wakifanya mazoezi ya kujifunza namna ya kutumia ( BVR KIT-Biometric Voters Registration Kit) wakati alipotembelea kukagua mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yaliyosimamia na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, yalianza kutolewa Februali 10 na kumalizika Februari  11 katika ukumbi wa Polisi Ofis Mes ambapo jumla ya Kata 20 zilizopo katika Halmashauri hiyo zilishiriki.

Akizungumza wakati wa kufungua na kufunga mafunzo hayo, Bi Faudhia alisema kuwa mafunzo hayo ni chachu kwa maafisa hao na kwamba wanapaswa kutumia nafasi hiyo vizuri ili kuisaidia Serikali kupata idadi kamili na sahihi ya wananchi watakaopiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Alifafanua kuwa  waandikishaji hao wasaidizi kwa ngazi ya kata wanapaswa kuhakikisha kuwa wanafuatilia na kusikiliza mafunzo hayo kwa umakini mkubwa kwani kazi hiyo ya uboreshaji wa dafatri ni nyeti na ni kwa maslahi ya maendeleo ya nchi.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yaliyotolewa kwa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata ambapo yanahusisha mfumo mzima wa namna ya mchakato wa uandikishaji ambapo mfumo huo umegawanyika katika maeneo matatu.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni uandikishaji wa mwananchi mpya kabisa,  uboreshaji wa taarifa za mpiga kura kwenye daftari (hii ni iwapo mwananchi alihama eneo la makazi au iwapo taarifa zilikosewa) pamoja na kumuondoa mpiga kura kwenye daftari kutokana na sababu mbalimbali kama vile kifo.

Alisema mafunzo hayo pia yalitolewa kwa watendaji ambao watahusika na uingizaji wa taarifa za wapiga kura katika mfumo wa kuandikisha wapiga kura (BVR Kit operator) pamoja na waandikishaji wasaidizi.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo pia yalihusisha kuapishwa kwa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata, namna ya ujazaji wa fomu mbalimbali pamoja na namna ya kutumia sanduku litakalotumika kubeba vifaa mbalimbali vilivyounganishwa na kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kuingiza taarifa binafsi za mpiga kura ( BVR KIT-Biometric Voters Registration Kit).

“ Naomba niwaeleze jambo moja, kazi hii mliyopewa ni muhimu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ifikapo Oktoba mwaka huu, tunaboresha daftari la wapigakura kwasababu, kuna wengine wametimiza miaka 18 hivi karibuni, wengine wamehama makazi yao, kwa hiyo huu mchakato ni muhimu sana ni waombe mkafanye kwa uangalifu mkubwa” kama mlivyo elekezwa na watoa mada” alisema Bi Faudhia.

Aliongeza kuwa” mnatakiwa kutumia lugha nzuri unapomuhoji mwananchi aliyefika kujiandikisha au kuboresha taarifa zake,tumeambiwa hapa na Maafisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, uandikishaji huu hauhusiani na kitambulisho cha Taifa, kwa hiyo hata kama mtu atakuja kujiandikisha bila kitambolisho cha NIDA muandikisheni.

Zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  litaanza rasmi Tarehe Februari 14 mwaka huu ambapo  litadumu kwa muda wa siku saba (7 ) na hivyo kumalizika Februari 21 mwaka huu.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akipokea nyaraka mbalimbali zinahusu Ofisi ya Katibu Mkuu kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ally Possi (kulia) ikiwa ni sehemu ya makabidhiano ya Ofisi mara baada ya kikao na viongozi wa Menejimenti ya Wizara alipowasili Februari 04, 2020 Jijini Dodoma.

Katika hali ya kawaida mtu anapofanya vizuri hupongezwa kwa kazi nzuri aliyoifanya ndio maana waswahili husema “Chanda chema huvikwa pete”, maana yake mtu anayefanya mema hulipwa mema.

Maneno hayo yanasadifu usemi aliousema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa anawaapisha viongozi mbalimbali February 3, 2020 Ikulu Jijini Dar es Salaam akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi Said.

Rais Dkt. Magufuli alitanabaisha utendaji wa Dkt. Abbasi kwa kusema ni mchapakazi anayefanya kazi nzuri ya kuisemea vizuri Serikali bila kuchoka kwa kufuata miongozo mizuri ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na viongozi wengine kwenye Wizara hiyo.

“Ningependa aendelee kuwa Msemaji wa Serikali, lakini mahali mtu anapotakiwa kupata promosheni usimnyime kwa sababu ni “Motivating Agent” ndio maana tumemteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, na kwa sasa hivi ataendelea kuwa Msemaji wa Serikali mpaka tutakapopata mwingine, na sasa atakuwa anasema akiwa mkubwa zaidi” alisema Rais Magufuli.

Mara baada ya Kuapishwa Dkt. Hassan Abbasi amesema kipaumbele chake ni kufanya mageuzi katika Wizara hiyo kwa kuwa anazifahamu vizuri sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Februari 03, 2020 Ikulu Jijini Dar es salaam.

“Nimeaminiwa tena na Mhe. Rais namshukuru sana ninamuahidi yeye binafsi, Watanzania wote, wadau wa hizi sekta pamoja na wafanyakazi wenzangu pale Wizarani, kwamba tunaenda kuendeleza mageuzi, sio kuanzisha, kwa sababu watangulizi wangu niwashukuru wameanza kazi kubwa, mimi kazi yangu pale itakuwa ni mageuzi katika Wizara ya Habari watu wasubiri mageuzi makubwa.” alisema Dkt. Abassi.

Mara baada ya kwasili wizarani hapo, Dkt. Abbasi alianza kazi kwa kukabidhiwa ofisi na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Ally Possi ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Suzan Mlawi kustaafu.

“Nimekuta watumishi wazuri sana Wizara hii, nimepata ushirikiano mzuri katika utendajikazi wangu, ni timu nzuri lazima tuiboreshe. Hakika kazi yako ya kuisemea Serikali umeifanya kwa weledi na mapinduzi makubwa sana katika Idara ya Habari ambayo unaendelea kuwa Msemaji wa Serikali, umeipeleka Idara pazuri sana” alisema Dkt. Possi.

Februari 7, 2020 Dkt Abassi alikutana na watumishi wote wa Wizara hiyo waliopo Jijini Dodoma na kubainisha mtarajio yake kwa watumishi hao na kuwahamasisha waendelee kuchapakazi kwa weledi kwa kuzingatia taaluma zao badala ya kuendekeza uvivu, utoro, uchelewaji, majungu, uzandiki na ubazazi.

“Natarajia mtakuwa waadilifu na wazalendo, muipende wizara yenu na nchi yenu na msiruhusu hujuma ya aina yeyote” Alisema.

Katibu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akisalimiana kwa furaha na wafanyakazi wa wizara alipowasili (Februari 04, 2020) katika Ofisi ya Wizara hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma,mara baada ya kuapishwa kwake Februari 03, 2020 na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli.

Natarajia mtakuwa wabunifu katika kazi zenu, mtindo wa kufanyakazi kwa mazoea bila ubunifu hauna nafasi ni vema mtumie taaluma zenu ipasavyo ziwe na tija kwa wadau wetu na nchi yetu” alisisitiza Dkt. Abassi

Katika kuyafikia malengo ya Wizara na ya Serikali, Katibu Mkuu huyo aliainisha siri sita za kusukuma mbele gurudumu la wizara hiyo kwa kuongozwa falsafa yake ya “Timu Tunatekeleza” inayosimamia kuweka malengo katika kazi na kuyasimamia. Malengo ni dira, bila kuweka malengo huwezi kujua hata unataka kwenda wapi wala utafika lini na kwa njia ipi.

Siri nyingine ni kuweka malengo makubwa, kutekeleza malengo hayo na sio maneno matupu, kuwa na mawasiliano madhubuti ndani na nje ya wizara ili kuyafikia malengo hayo, kuwa na ushirikiano baina ya menejimenti, watumishi na wadau wa taasisi pamoja na kuamini nguvu ya Mungu katika kufikia malengo tunayojiwekea kwa kuwa yapo mambo ambayo yanazidi uwezo wa mwanadamu na hapo nafasi ya Muumba ni ya muhimu.

Awali akimkaribisha Katibu Mkuu Dkt. Abbasi kuongea na watumishi hao Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Macelline Patrick alisema lengo la kikao hicho ni kutambulishana pamoja na kutoa ahadi ya uadilifu kwa viongozi na watumishi kwa Kiongozi na Mtendaji Mkuu wa Wizara.

Pia aliongeza kuwa Wizara hiyo ina idadi ya watumishi 224 ambao miongoni mwao wapo Makao Makuu jijini Dodoma na wengine wapo jijini Dar es salaam pamoja na Chuo cha Maendeleo ya Michezo cha Mallya kilichopo mkoani Mwanza.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Abdul Njaidi amesema kuwa wamefurahishwa na uteuzi wa Dkt. Abbasi kushika wadhifa Katibu Mkuu kwa kuwa ataendelea kuwa nao katika tasnia ya Habari.

“Ataifanya TAGCO iende hatua za juu zaidi kwa sababu anaijua, siku zote amekuwa akisimamia taaluma na kutaka watu wafanye kazi kwa matakwa ya taaluma zao ili kufikia malengo ya Serikali ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025” alisema Njaidi.

Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakila kiapo cha Uadilifu katika utumishi wa Umma mele ya Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi baada ya kupata Semina elekezi kutoka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyofanyika Februari 07, 2020 jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kikao kazi cha watumishi wa Wizara hiyo.

Aidha, Baada ya kuteuliwa na Rais Ijumaa Januari 31, 2020, baadhi ya wadau wa sekta ya habari wakiwemo Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini pamoja na Wizara na Taasisi mblimbali walitoa pongezi na maoni yao kupitia jukwaa la “WhatsApp” kuhusiana na uteuzi huo.

Baadhi waliandika pongezi zao kwa Katibu Mkuu Dkt. Abassi ambapo Theodos Komba anasema “Hongera Dkt., Mungu aendelee kukubariki katika utekelezaji wako wa majukumu mapya. Tunafuraha kuwa tunaendelea kuwa pamoja”; Nteghejwa Hosea anasema “Hongera Dkt., Mungu ataendelea kukuongoza hata hapo unapoenda sasa;”

Wengine waliotoa maoni yao ni Mtamike Omary anasema “Hongera Dkt., Mwenyezi Mungu azidi kukujaalia hekima na busara nyingi zaidi wakati wote wa uongozi wako, hakika umekuwa nahodha bora sana kwetu;” Peres Muhagaze anasema “Hongera sana Dkt. Hassan Abbas!! Umeitumikia Serikali na Umma kwa ueledi wa hali ya juu ukiwa Mkuruggenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na  Msemaji Mkuu wa Serikali, umeacha alama, tunakuombea ufanye zaidi katika ofisi yako mpya ya Katibu Mkuu wa Wizara na kuendelea ili  kutimiza adhma yako ya ndani ya kuwatumikia Watanzania katika masuala mbalimbali. Mwenyezi Mungu akutangulie katika maukumu mapya”

Aidha, pongezi hizo kwa Katibu Mkuu Dkt. Abassi pia zimetolewa na Wizara na Taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara yake anayoiongoza, Wizara ya Maji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kampuni ya Magazeti ya serikali Tanzania (TSN) na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Akiwashukuru wadau hao kupitia jukwaa hilo kwa kumpongezi zao, Katibu Mkuu Dkt. Abassi anasema “Team, Kimsingi sina la kusema kwa imani hii kubwa ambayo Mhe. Rais ameendelea kuniamini. Namhuskuru sana sana na zaidi nawashukuru wote kwa salaam.

Ni faraja kwamba bado tuko wote katika sekta ya Habari. Tuanzie hapo tulipoishia. Hii ni Wizara iliyobeba soft power zote za nchi. Nawatakia kasi na utekelezaji mwema wa pale tulipoishia. Nitabaki kuwa mlezi wenu mujarabu. Hakika mmenilea, mmenishauri, mmenisikiliza, mmenivumilia na tumepiga kazi, basi na kazi iendelee. Nyie ni TeamTunatekeleza Tuendelee na kazi Mungu Awabariki.”

Dkt. Abbasi anakuwa Katibu Mkuu wa 26 kuingoza Wizara hiyo akitanguliwa na Makatibu Wakuu 25 tangu nchi yetu kupata Uhuru mwaka 1961 ambapo mnamo mwaka 1964 Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwl. Julius Nyerere aliunda Wizara ya Habari na Utalii ilidumu hadi 1971 ilipoundwa Wizara ya Habari na Utangazaji. Mwaka 1980 Serikali iliunganisha majukumu ya sekta ya Habari na Utamaduni na kuunda Wizara ya Habari na Utamaduni.

Aidha, mwaka 1984 majukumu ya sekta ya Habari na Utamaduni yalihamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais na na mwaka 1995 hadi 2005 majukumu ya Sekta ya Habari yapohamishiwa tena Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Sekta ya Habari, Utamaduni na Michezo ziliunganishwa pamoja na kuunda Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Serikali iliunda Wizara Mpya ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Mwaka 2016 Serikali ya Awamu ya Tano iliunda Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michzo ambayo inafanya kazi hadi sasa.

Makatibu Wakuu waliohudumu katika Wizara hii ni pamoja na Bw. A. K. Tibandebage, Bw. B. J. Mkate, Bw. Bernard Mulokozi, Bibi Zahra Nuru, Dkt. Ben Moses, Bw. Daniel Mloka, Mhandisi Paul Mkanga, Bw. Paul Sozigwa, Bw. Wilfred Mwabulambo, Bw. Silvano Adel, Bw. Elly Mtango, Bibi Rose Lugembe, Bw. Raphael Mollel, Bw. Silvanus Odunga, Bw. Abubakari Rajabu, Bw. Kenya Hassan, Bw.  D. Sepeku, Bw.  Raphael Mhagama, Bibi Kijakazi Mtengwa, Dkt. Florens Turuka, Bw.  Sethi Kamuhanda, Bibi Sihaba Nkinga, Prof. Elisante Ole Gabriel na Bibi Suzan Mlawi.

Dkt Hassan Abbasi Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, ameshika wadhifa wa Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali tangu Agosti 5, 2016 hadi kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo Januari 31, 2020 na kuapishwa Februari 03, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam.

Alizaliwa wilayani Korogwe, Tanga mwaka 1978 na kupata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Hale kati ya mwaka 1988 na 1994. Alimaliza akiwa mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri mkoani humo na kujiunga na Sekondari ya wanafunzi wenye vipaji maalum ya Tabora Wavulana (Tabora School) mwaka 1995 kwa masomo ya sekondari.

Kati ya mwaka 1997 na 1998 alihamia katika Sekondari ya Azania, Dar es Salaam ambapo alimaliza kidato cha nne na kati ya mwaka 1999-2001 alijiunga na Shule ya Sekondari Lindi kwa masomo ya kidato cha tano na sita.

Kati ya mwaka 2002 na 2006 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alichukua shahada ya kwanza ya sheria (LL.B). Akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu pia aliajiriwa kama mwandashi wa habari wa kujitegemea katika kampuni ya Business Times na baadaye kushika nafasi mbalimbali kuanzia mwandishi mwandamizi, mhariri msaidizi hadi mhariri Mkuu katika magazeti ya Majira na Kulikoni.

Mwaka 2005 akiwa bado mwanafunzi, alichaguliwa kuwa Mhariri Mkuu wa Jarida liitwalo “Nyerere Law Journal” linalochapishwa na Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kati ya mwaka 2007 na 2008 alihudhuria masomo ya uandishi wa habari ndani na nje ya nchi ikiwemo makao makuu ya Reuters, London, Uingereza na Chuo Kikuu cha Maine nchini Marekani.

Mwaka 2010 aliajiriwa Serikalini akiwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) tawi la Tanzania, programu iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Nje, ambapo kabla ya mwaka 2014 alikuwa Meneja Mawasiliano katika Ofisi ya Rais, Kitengo cha Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Aidha, ana taaluma ya Sheria ambapo ana hadhi ya Wakili wa Mahakama Kuu tangu mwaka 2011, Dkt. Abbasi pia ana diploma ya uzamili katika usimamizi wa mahusiano ya kimataifa (PGD-MFR) kutoka Chuo cha Diplomasia cha Msumbiji na Tanzania, Kurasini, shahada ya uzamili katika mawasiliano kwa umma (MA Mass. Comm., SAUT) na shahada ya uzamivu katika mawasiliano kwa umma (Ph.D Mass. Comm., SAUT).

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh