World

Wananchi wa Jijini la Dar es Salaam, wakiwa wamepanga mstari katika Viwanja vya Mnazi Mmoja wakiendelea na zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Nchi nzima, kufuatia agizo la Rais Dkt. Magufuli kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuongeza siku 20 hadi kufikia mpaka January 20 mwaka huu kuwapatia nafasi wananchi waweze kupata namba ya Utambulisho wa Taifa na kuepusha kufungiwa laini zao za Simu.
Baadhi Wafanyakazi kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakiwahudumia wananchi waliojitokeza eneo la Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kwenye zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Nchi nzima, kufuatia agizo la Rais Dkt. Magufuli kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuongeza siku 20 hadi kufikia mpaka January 20 mwaka huu kuwapatia nafasi wananchi waweze kupata namba ya Utambulisho wa Taifa na kuepusha kufungiwa laini zao za Simu.
Afisa kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akimuhudumia mwananchi aliyejitokeza eneo la Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kwenye zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Nchi nzima, kufuatia agizo la Rais Dkt. Magufuli kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuongeza siku 20 hadi kufikia mpaka January 20 mwaka huu kuwapatia nafasi wananchi waweze kupata namba ya Utambulisho wa Taifa na kuepusha kufungiwa laini zao za Simu.

 

Ukosoaji wa Urusi dhidi ya njama za Marekani za kubadili mlingano wa nguvu Asia Magharibi

MOSCOW, URUSI

HATUA za Marekani katika eneo la Asia Magharibi hususan za kuzidisha uwepo wake kijeshi, mashinikizo dhidi ya Iran na hatimaye kutekeleza hatua za kigaidi hasa za kumuua Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la IRGC.

Naibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Hashdu sh-Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes na shakhsia wengine walioambatana nao, zimekabiliwa na radiamali kali kutoka kwa Urusi kama mmoja wa wacheza karata muhimu katika eneo hili.

Katika uwanja huo Ijumaa iliyopita Maria Zakharova, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova sambamba na kulaani vikali kitendo cha kigaidi cha kumuua Jenerali Soleimani alisema kuwa, Marekani ina lengo la kubadili mlingano wa nguvu katika eneo la Asia Magharibi.

Aliitaja hatua hiyo kuwa itakayoifikisha Marekani kwenye kilele cha kuchukiwa, kudhaniwa na kutazamwa vibaya zaidi duniani.

Serikali ya Urusi inaamini kwamba Marekani inatumia suala la maandamano mbele ya ubalozi wake mjini Baghdad kama kisingizio cha kutekeleza hatua zake zilizo kinyume cha sheria hususan katika kumuua Jenerali Soleimani.

Maria Zakharova amesema: “Katika kulaani mashambulizi dhidi ya ubalozi, serikali tofauti huwasilisha malalamiko yake mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini Marekani haikuwasilisha malalamiko yake mbele ya baraza hilo na hii ina maana kwamba inafuatilia radiamali ya walimwengu na kutaka kubadili mlingano wa nguvu katika eneo.”

Nukta muhimu ni hii kwamba, katika maandamano ya Wairaq ambapo baadhi ya washiriki waliingia hadi ndani ya ubalozi huo, yalifanyika kulalamikia hatua za kijinai za Marekani baada ya askari wa Kimarekani kushambulia ngome za Harakati ya Wananchi ya Hashdu sh-Sha’abi katika mkoa wa Al-Anbar nchini humo.

Ukweli ni kwamba Serikali ya Trump licha ya kwamba inafahamu vyema kuwa Harakti ya Hashdu sh-Sha’abi ni sehemu ya jeshi la Iraq, inatumia visingizio bandia na visivyo na ushahidi wowote kuituhumu kuwa ilifanya shambulio dhidi ya ngome za Marekani katika mji wa Kirkuk shambulio lililopelekea kuuliwa afisa mmoja wa Kimarekani.

Ni kwa kisingizio hicho ndipo ikatekeleza mashambulizi yake ya kinyama yaliyopelekea kuuawa na kujeruhiwa makumi ya wanamuqawama wa harakati hiyo ya wananchi.

Katika hatua nyingine serikali ya Trump na kwa kisingizio kwamba eti Jenerali Qassem Soleimani alikuwa anakusudia kupanga mashambulizi dhidi ya Wamarekani na taasisi za Kimarekani nchini Iraq, imemuua kigaidi na kwa namna ya kutisha yeye pamoja na watu aliokuwanao.

Katika uwanja huo akizungumza kwa njia ya simu na Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ametoa radiamali yake kuhusiana na jinai ya kumuua kigaidi Jenerali Qassem Soleimani na kubainisha kuwa kitendo hicho ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.

Suala lingine ni kwamba kufuatia hatua hiyo ya kinyama na ya ukiukaji wa sheria iliyofanywa na Washington katika jinai hiyo, Russia imekiona kitendo hicho kuwa kitakachokuwa na taathira hasi kwenye muundo wa usalama kimataifa.

Ijumaa iliyopita Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilitoa taarifa ambapo sambamba na kuashiria huduma chanya za Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC.

Katika mapambano yake dhidi ya makundi ya kigaidi likiwemo genge la ukufurishaji la Daesh (ISIS) nchini Iraq na Syria, ilisema kuwa kumuua kigaidi jenerali huyo kutapelekea kuwa mbaya zaidi hali ya kisiasa na kijeshi katika eneo la Asia Magharibi na kuwa na taathira hasi kwenye muundo wa usalama wa kimataifa.

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Russia ilibainisha kwamba: “Kumuua kigaidi Jenerali Qassem Soleimani kulikofanywa na Marekani, kutaifanya kuwa mbaya zaidi hali ya kisiasa na kijeshi eneo la Asia Magharibi kama ambavyo kutakuwa na taathira hasi kwenye muundo mzima wa usalama wa kimataifa. Mtazamo finyu wa Marekani ambao umepelekea kuuawa shahidi Soleimani, utavuruga zaidi hali ya eneo.” 

Hii ni katika hali ambayo kwa mara kadhaa Urusi imekuwa ikikosoa vikali siasa zinazotekelezwa na Marekani katika eneo la Asia Magharibi na kuzitaja siasa hizo kuwa zinachochea ghasia, kuzidisha mizozo na kuibua mapigano katika eneo.

Baada ya Marekani kujiondoa kwa upande mmoja katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA hapo mwezi Mei 2018, ilianzisha siasa za mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo moja ya hatua hizo ni kufikisha sifuri uuzaji mafuta wa nchi hii.

Vikwazo vikali vya kiuchumi ambavyo havijawahi kushuhudiwa na mashinikizo ya Washington dhidi ya taifa hili, vimeshadidisha mvutano wa nchi mbili ambapo moja ya matokeo ya hali hiyo ni kuongezeka mzozo katika Lango Bahari la Hormoz na Ghuba ya Uajemi.

Hivi sasa pia baada ya Marekani kushambulia kwa makusudi ngome za Harakati ya Hashdu sh-Sha’abi nchini Iraq na kuwaua kigaidi Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandes, Naibu Mkuu wa Hashdu sh-Shaabi, inakusudia kuliingiza eneo katika awamu mpya ya machafuko.

Ukweli ni kwamba tangu serikali ya Trump ilipoingia madarakani haijawa na kazi nyingine ghairi ya kuchochea ghasia na machafuko katika nyuga za kimataifa na katika eneo la Asia Magharibi.

Online Shopping in BangladeshCheap Hotels in Bangladesh